Quran ya Allah ni kitabu kisichokuwa na shaka

Muumba mbigu , ardhi na vilivyomo ndani yake .

Mola mlezi wa viumbe wote na ambaye anapaswa kuabudiwa kwa haki
Huyo Mola mlezi wa viumbe vyote, akiabudiwa anafaidika nini?

Huyo Mola asipoabudiwa, anapungukiwa nini?

Huyo Mola yupo so insecure hadi anahitaji kuabudiwa?

Huyo Mola akisha abudiwa anapata nini zaidi?

Hivi huyo Mola anajielewa kweli?
 
uongo! kabla ya Muhamad hakukuwa na islam, middle east kulikuwa na Christians, wayahudi na wapagani tu …

Itakuwa hujui nini maana ya uislamu

Ayubu 22:21
New International Version (©1984)

"Jitayarishe mbele za Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hii ustawi utakuja kwako."

Kiarabu: تعرّف به واسلم. بذلك ياتيك خير.

Kama ulivyoweza kuona, kuna uongo katika tafsiri; hakuna sehemu inayosema Ta'araf (تعرّف) kwa Kiingereza, lakini ipo katika Biblia ya Kiarabu.

Kiebrania: הסכן נא עמו ושלם בהם תבואתך טובה׃
Hasken na immow USALM bahem tabowatka towbah

Hivyo, Uislamu ulikuwepo kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.).

Thibitisha

Allah" ni Jina la Mungu, na "Elaw" linamaanisha "Mungu" kwa Kiaramu. Je, zinafanana?

Hoja niliyopewa ni: Je, Kiarabu "Allah" linaweza kuwa sawa na Kiaramu "Elaw", wakati "Allah" ni jina la Mungu kwa Kiarabu, huku "Elaw" likimaanisha "Mungu"? Je, "Allah" halimaanishi "Mungu" kwa Kiarabu?

Jibu ni rahisi: "Elaw" au "ilah" kwa Kiaramu na Kiarabu linatokana na neno mama "Allah". Katika Uislamu, Mungu Mwenye Nguvu ana Majina/ Sifa 99: Mwingi wa Rehema, Mkuu, Mwingi wa Neema, n.k. "Allah" ni moja ya majina hayo matakatifu. Waislamu wanamuita Mungu Mwenye Nguvu "Allah" si tu kwa kuwa ni Jina Lake Tukufu, bali pia linamaanisha kuwa Yeye ndiye Mungu Mkuu.

Tukisoma aya ya Quran Tukufu:

"Qul huwa Allah ahad, Allah al-samad; lam yalid wa lam yuwlad; wa lam yakun lahu qufuwan ahad." (Quran 112:1-4)

Tafsiri ya Abdullah Yusuf Ali:

"Say: He is God, the One and Only; God, the Eternal, Absolute; He begetteth not, nor is He begotten; And there is none like unto Him."

Aya hii inaonyesha wazi kuwa "Allah" si tu jina, bali ni sifa au maelezo ya Mungu Mkuu. Hivyo, katika Kiarabu, "Allah" lina maana ya Mungu Mwenye Nguvu.
 
Huyo Mola mlezi wa viumbe vyote, akiabudiwa anafaidika nini?

Huyo Mola asipoabudiwa, anapungukiwa nini?

Huyo Mola yupo so insecure hadi anahitaji kuabudiwa?

Huyo Mola akisha abudiwa anapata nini zaidi?

Hivi huyo Mola anajielewa kweli?

Wasio na akili husema hivyo au thibitisha kuwa una akili
 
Mtume alishushiwa Quran miaka 600+ baada ya Uyahudi na Ukristo kuwepo.
Kwa mtindo wa Wahyi na mara 2 kwa kuonana ana kwa ana na Jibril.

Swali langu,
1. Imewezekanaje Quran kuwe na visa vya wana wa Waisrael. Ina maana na vywenyewe Mohamed alikuwa anaoteshwa?.

(Yona au Yunus, ibrahim , sodoma na gomora nk)
Hizi zote Jibril alimfunulia Mohamed sio? Kwamba hakuwa anazijua na waarabu walikuwa hawazifahamu?.

(Hapa Nina maanisha visa ambazo haviko kwenye Torati, ) je zilishushwa na Allah kwa wahyi?.
Na Kwa ufafanuzi zaid Tourat ni kitabu kimoja alichoshushiwa Musa
Al-Isra 17:2
"Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili...
Al-Ahqaf 46:12
"Na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilichokuwa kiongozi na rehema"

2. Ni kitabu gani ambacho Nabii Issa alipewa?.

Quran 19 : 30
"Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu na amenifanya Nabii."

Ilhali Injili iliandikwa na Wanafunz wa Yesu.

3. Kwanini ilichukua miaka 23 kukamilika wakat Quran yote ilishushwa siku moja usiku kwenye mwez wa ramadhan Laylatul-Qadr

(Lauhul-Mahfuz mpaka Baitul-'Izzah).

4. Ameshushiwa Mohamed ila walioiandika ni wafuasi wake baada ya yeye kufa.

Kwanini asingekusanya na kupanga aya zote na kukamilisha kitabu kamili yeye mwenyewe?.
Kama alivyodai kuwa amepewa Kitabu.

5. Muislam wa kwanza ni Mtume Mohamed.
Kama sio sahihi naomba mnijibu kwa kutumia Quran huku ukiweka pia akilini maana ya kusilimu na shahada.

Jagina Kazakh destroyer adriz gallow bird Covax hateeb10 na wengine niliowasahau naomba mnisaidie kujibu.

Pia kwasababu Quran ina amini kwenye Torati ,Zaburi na Injili.

Ina maana maneno yote ya vitabu hivi ni ya kweli kwasababu hauwez kuchagua baadhi na kuacha baadhi.

Kukataa haya naomba uniwekee aya ya Quran inayokanusha.

Quran imejaa visa vya wanawaisrael Kwa sababu wao ndio walikuwa wanaenda Kwa mtume na kumpa challenge Kwa kumuuliza mambo ya manabii wa wazamani na mambo ya wachamungu wa zamani

Alafu kitu ambacho nyinyi wagalatia hamkijui ni kuwa hakuna muisraeli anayepinga kuwa Muhammad sio mtume wa Mungu

Shida ipo kwenu wagalatia na ni Kwa sababu Wazungu wamekudanganyeni sana
 
Itakuwa hujui nini maana ya uislamu

Ayubu 22:21
New International Version (©1984)

"Jitayarishe mbele za Mungu na uwe na amani naye; kwa njia hii ustawi utakuja kwako."

Kiarabu: تعرّف به واسلم. بذلك ياتيك خير.

Kama ulivyoweza kuona, kuna uongo katika tafsiri; hakuna sehemu inayosema Ta'araf (تعرّف) kwa Kiingereza, lakini ipo katika Biblia ya Kiarabu.

Kiebrania: הסכן נא עמו ושלם בהם תבואתך טובה׃
Hasken na immow USALM bahem tabowatka towbah

Hivyo, Uislamu ulikuwepo kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w.).

Biblia haijaongelea wala kutaja neno islam popote pale, na sababu ni hiyo, kwamba islam ilianza karne ya 7 a.d. baada ya Muhamad ...
 
Uislamu ni dini ambayo Allaah ameichagua kama mfumo sahihi wa maisha kwa Wanadamu wote na tokea Nabii wa kwanza Baba yetu Aadam (Peace be upon Him ) alikuwa Muislamu na Manabii wote Musa , Yesu , Nuhu , Ibrahimu , Yakubu nk (Amani iwe juu yao wote ) dini yao ilikuwa ni Uislamu na walilingania katika Uislamu .

Sheria tu zilitofautiana kutoka na zama lakini misingi mikuu ile ile ambapo msingi mkuu unawaunganisha wote kuwafanya wawe Waislamu ni Tawheed maana yake kumpwekesha Mola muumba pekee kwa kumuabudia yeye tu bila kumshirikisha . Ndio maana hakuna Nabii akiyekuja kudai kuwa yeye ni Mungu au kiabudiwe kingine kinyume na Mungu muumba (Allaah)

Manabii wote walikuja kukingania watu waachane na maovu , wafanye mema kwa kumtii mola wao huo ndio Uislamu . Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah mola muumba kwa kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha kufuata maarisho yake na kuacha makatazo kama jinsi alivyoolekeza kupitia Manabii na wajumbe wake.

Ndio maana tunasema Uislamu ukikuwepo tokea mwanzo na Manabii wote walikuwa Waislamu sababu walikuwa kwenye misingi hiyo , tofauti ipo kwenye baadhi ya Sheria tu sawa na Leo I phone zote ni I phone zina sifa za kipekee kuitwa I phone pamoja na kuwa na matoleo tofauti kutokana na maboresho ila sifa za kipee zinazofanya kuwa I phone lazima zitabaki kama msingi
Kuna uislam Bila Quran?
 
Kuna uislam Bila Quran?

Inabidi uelewe nini Uislamu na nini Quran

1. Uislamu ni dini ya Mungu mmoja​

  • Neno Islamu linatokana na Kiarabu S-L-M, lenye maana ya kuwasilisha/kukabidhi maisha yako kwa Mungu.
  • Dini hii inahimiza ibada ya Mungu mmoja tu (Allah), na mafundisho haya hayajaanzishwa na mtu fulani.

2. Nabii Muhammad si mwanzo wa Uislamu​

  • Waislamu wanaamini kuwa Uislamu ulianza na mwanzo wa binadamu.
  • Mitume na manabii wote waliotumwa na Allah (kama vile Nuhu, Ibrahimu, Musa, na Yesu) walikuwa wanatoa mafundisho ya Uislamu: kumwabudu Mungu mmoja, kuishi kwa haki, na kufanya mema.
  • Mtume Muhammad (a.s.w.) alikuja kama Mtume wa mwisho, lakini hata kabla yake, mafundisho ya kweli ya Uislamu yalikuwa yamekuwa yanafundishwa.

3. Uislamu na Biblia​

  • Baadhi ya aya za Biblia zinaonyesha dhana ya Mungu mmoja na kusalimisha kwake (submission), jambo linalofanana na misingi ya Uislamu.
  • Mfano: Jobu 22:21 inasema:
    “Submit to God and be at peace with Him” (Jisalimishe kwa Mungu na uwe na amani naye).
  • Kiarabu cha Biblia: واسلم (waslim) kinatokana na mzizi sawa na Islam, kuonyesha dhana ya kuwasilisha maisha kwa Mungu.

Kwa ufupi: Uislamu ni dini ya Mungu mmoja iliyokuwa hai tangu mwanzo wa binadamu, na Mtume Muhammad (a.s.w.) alikuja kama Mtume wa mwisho kufundisha na kuhalalisha mafundisho haya kwa ulimwengu.
 
Kuna uislam Bila Quran?

Hapa kuna mfuatano wa baadhi ya Manabii waliotajwa katika Biblia na jinsi wanafanana na mafundisho ya Uislamu:

1.​

  • Biblia: Aliyechaguliwa na Mungu kuokoa familia yake na wanyama kutoka kwenye maji ya ghasia (Mwanzo 6-9).
  • Uislamu: Nuhu (a.s.) ni Nabii aliyefundisha ibada ya Mungu mmoja, na kuepuka uovu wa watu wake. Alikuja na amri ya kuwasalimisha maisha yao kwa Allah.

2.​

  • Biblia: Mzazi wa waamini, aliyeitwa kuabudu Mungu mmoja (Mwanzo 12, 15).
  • Uislamu: Ibrahim (a.s.) ni mfano wa Tauhidi. Alijenga Kaaba ili kuabudu Allah. Alisisitiza wafuasi wake kuabudu Mungu mmoja bila washirika.

3.​

  • Biblia: Mtume aliyeongoza Waisraeli kutoka utumwa na kupokea Sheria ya Mungu (Torah).
  • Uislamu: Musa (a.s.) ni Mtume wa Allah aliyefundisha wafuasi wake kufuata sheria za Allah na kuepuka maasi.

4.​

  • Biblia: Wanafundisha haki, kuabudu Mungu, na kuandika Zaburi.
  • Uislamu: Dawudi (a.s.) alipewa Zaburi na kuwa mfano wa haki. Sulaimani (a.s.) alijulikana kwa hekima na kusikiliza amri za Allah.

5.​

  • Biblia: Mtume na mwokozi aliyefundisha upendo, rehema, na haki.
  • Uislamu: Isa (a.s.) ni Nabii wa Allah, aliyefundisha Tauhidi. Hakujitambulisha kama mwana wa Mungu bali kama Mtume wa Allah.

6.​

  • Biblia: Hakutajwa kwa jina, lakini Uislamu unaamini kuwa nabii wa mwisho alitabiriwa katika maneno ya manabii wa awali (kama Musa na Isaya).
  • Uislamu: Mtume Muhammad (a.s.w.) alikuja kufundisha mafundisho yote ya awali ya Uislamu, na kuleta Quran kama kitabu cha mwisho cha Allah kwa wanadamu.

Hitimisho​

  • Uislamu haujaanza na Muhammad, bali ulianza na manabii wote waliotaka kuabudu Mungu mmoja.
  • Mtume Muhammad ni Mtume wa mwisho aliyehalalisha mafundisho haya na kuyakamilisha kwa ulimwengu wote.

Inabidi uelewe nini Uislamu na nini Quran

1. Uislamu ni dini ya Mungu mmoja​

  • Neno Islamu linatokana na Kiarabu S-L-M, lenye maana ya kuwasilisha/kukabidhi maisha yako kwa Mungu.
  • Dini hii inahimiza ibada ya Mungu mmoja tu (Allah), na mafundisho haya hayajaanzishwa na mtu fulani.

2. Nabii Muhammad si mwanzo wa Uislamu​

  • Waislamu wanaamini kuwa Uislamu ulianza na mwanzo wa binadamu.
  • Mitume na manabii wote waliotumwa na Allah (kama vile Nuhu, Ibrahimu, Musa, na Yesu) walikuwa wanatoa mafundisho ya Uislamu: kumwabudu Mungu mmoja, kuishi kwa haki, na kufanya mema.
  • Mtume Muhammad (a.s.w.) alikuja kama Mtume wa mwisho, lakini hata kabla yake, mafundisho ya kweli ya Uislamu yalikuwa yamekuwa yanafundishwa.

3. Uislamu na Biblia​

  • Baadhi ya aya za Biblia zinaonyesha dhana ya Mungu mmoja na kusalimisha kwake (submission), jambo linalofanana na misingi ya Uislamu.
  • Mfano: Jobu 22:21 inasema:
    “Submit to God and be at peace with Him” (Jisalimishe kwa Mungu na uwe na amani naye).
  • Kiarabu cha Biblia: واسلم (waslim) kinatokana na mzizi sawa na Islam, kuonyesha dhana ya kuwasilisha maisha kwa Mungu.

Kwa ufupi: Uislamu ni dini ya Mungu mmoja iliyokuwa hai tangu mwanzo wa binadamu, na Mtume Muhammad (a.s.w.) alikuja kama Mtume wa mwisho kufundisha na kuhalalisha mafundisho haya kwa ulimwengu.
Bro nijibu Tu kifupi, kuna uislamu Bila quran? Ndio au hapana. Kwamba hivyo vitu viwili havina ulazima wa kuwa pamoja.
 
Si tayari ulisema mimi sina akili.

sasa unataka nini zaidi wewe kichwa maji?

Huthibitishi kama una akili.

Umeshindwa kuthibitisha kama una akili. Una rukaruka tu kama chura.

Mimi sijasema hakuna Mungu wanaosema hakuna mungu wote hawana akili
 
Mtume alishushiwa Quran miaka 600+ baada ya Uyahudi na Ukristo kuwepo.
Kwa mtindo wa Wahyi na mara 2 kwa kuonana ana kwa ana na Jibril.

Swali langu,
1. Imewezekanaje Quran kuwe na visa vya wana wa Waisrael. Ina maana na vywenyewe Mohamed alikuwa anaoteshwa?.

(Yona au Yunus, ibrahim , sodoma na gomora nk)
Hizi zote Jibril alimfunulia Mohamed sio? Kwamba hakuwa anazijua na waarabu walikuwa hawazifahamu?.

(Hapa Nina maanisha visa ambazo haviko kwenye Torati, ) je zilishushwa na Allah kwa wahyi?.
Na Kwa ufafanuzi zaid Tourat ni kitabu kimoja alichoshushiwa Musa
Al-Isra 17:2
"Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya kuwa ni uongofu kwa Wana wa Israili...
Al-Ahqaf 46:12
"Na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilichokuwa kiongozi na rehema"

2. Ni kitabu gani ambacho Nabii Issa alipewa?.

Quran 19 : 30
"Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu na amenifanya Nabii."

Ilhali Injili iliandikwa na Wanafunz wa Yesu.

3. Kwanini ilichukua miaka 23 kukamilika wakat Quran yote ilishushwa siku moja usiku kwenye mwez wa ramadhan Laylatul-Qadr

(Lauhul-Mahfuz mpaka Baitul-'Izzah).

4. Ameshushiwa Mohamed ila walioiandika ni wafuasi wake baada ya yeye kufa.
Hii narrative ipo lakini si ya kweli
Quran 25:4-5 imeonesha mtume alisimamia uandishi wa Quran

Kwanini asingekusanya na kupanga aya zote na kukamilisha kitabu kamili yeye mwenyewe?.
Kama alivyodai kuwa amepewa Kitabu.

5. Muislam wa kwanza ni Mtume Mohamed.
Kama sio sahihi naomba mnijibu kwa kutumia Quran huku ukiweka pia akilini maana ya kusilimu na shahada.
Wakati wa Muhammad penye Muhammad utaweka Muhammad, shahada wakati wa Ibrahim utaweka Ibrahim kama firauni baada ya kuzama alisema/toa shahada '..nimemuamini Mungu wa Musa na haruni'
Jagina Kazakh destroyer adriz gallow bird Covax hateeb10 na wengine niliowasahau naomba mnisaidie kujibu.

Pia kwasababu Quran ina amini kwenye Torati ,Zaburi na Injili.
Hivi vitabu vilikuwepo ila kwa sasa havipo,injili ni ya issa bin Maryam na si ya matayo wala marko
Ina maana maneno yote ya vitabu hivi ni ya kweli kwasababu hauwez kuchagua baadhi na kuacha baadhi.

Kukataa haya naomba uniwekee aya ya Quran inayokanusha.
Haya tushajibu sana humu
 
Bro nijibu Tu kifupi, kuna uislamu Bila quran? Ndio au hapana. Kwamba hivyo vitu viwili havina ulazima wa kuwa pamoja.

Mbona uislamu ulikuwepo kabla kushuka Quran

1766866141434.png
 
Uislamu ni dini ambayo Allaah ameichagua kama mfumo sahihi wa maisha kwa Wanadamu wote na tokea Nabii wa kwanza Baba yetu Aadam (Peace be upon Him ) alikuwa Muislamu na Manabii wote Musa , Yesu , Nuhu , Ibrahimu , Yakubu nk (Amani iwe juu yao wote ) dini yao ilikuwa ni Uislamu na walilingania katika Uislamu .

Sheria tu zilitofautiana kutoka na zama lakini misingi mikuu ile ile ambapo msingi mkuu unawaunganisha wote kuwafanya wawe Waislamu ni Tawheed maana yake kumpwekesha Mola muumba pekee kwa kumuabudia yeye tu bila kumshirikisha . Ndio maana hakuna Nabii akiyekuja kudai kuwa yeye ni Mungu au kiabudiwe kingine kinyume na Mungu muumba (Allaah)

Manabii wote walikuja kukingania watu waachane na maovu , wafanye mema kwa kumtii mola wao huo ndio Uislamu . Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah mola muumba kwa kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha kufuata maarisho yake na kuacha makatazo kama jinsi alivyoolekeza kupitia Manabii na wajumbe wake.

Ndio maana tunasema Uislamu ukikuwepo tokea mwanzo na Manabii wote walikuwa Waislamu sababu walikuwa kwenye misingi hiyo , tofauti ipo kwenye baadhi ya Sheria tu sawa na Leo I phone zote ni I phone zina sifa za kipekee kuitwa I phone pamoja na kuwa na matoleo tofauti kutokana na maboresho ila sifa za kipee zinazofanya kuwa I phone lazima zitabaki kama msingi

Yaan saa 6 hii usiku ndio nafika home. Nimetoka kwenye kadamsee.

Bro. Utetezi wako una mashaka.
Lakini Nitasoma comment huko mbelebi . Ila kwakuwa hii ni comment ndio ya kwanza nasoma . Na umejibu swali moja .

La kwamba nani Muislam wa kwanza.

Na ambalo hujajibu kwa Quran kwamba je ? Unaweza kuwa muislam kama haujafanya
1. KISILIMU
2. SHAHADA

AU ww unapingana na huu mstari wa Quran ambayo hauna shaka .

Kasome

Surah Al-An'am (6:163)
: "Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu (walio jisalimisha kwa Mwenyezi Mungu)."

Surah Az-Zumar (39:12)
: "Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa Waislamu."

Surah Al-An'am (6:14)
: "Sema: Je, nimfanye mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi? Naye ndiye anaye lisha wala halishwi. Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu..."

2. Nionyeshe mtume yoyote zaid ya Mohamed aliyefanya SHAHADA.
Kwa Biblia na Quran.

(Ukinjonyesha Ntakutumia 1 Million Tsh. Ambayo iko kwa uwezo wangu. Tuwasiliane PM)

Nguzo ya kwanza ya Uislam ni Shahada
Na Shahada ni hii

"Ash-hadu an la ilaha illa Allah, wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulu-Allah.
Maana: "Nashuhudia kuwa hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu (Allah), na nashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Sitak maneno. Niwekee kwa Biblia au Quran nani alisema haya nje ya Mohamed.

Nalala sasa . Nikiamka. Ntajibu comment zote.
 
Huyo Mola mlezi wa viumbe vyote, akiabudiwa anafaidika nini?

Huyo Mola asipoabudiwa, anapungukiwa nini?

Huyo Mola yupo so insecure hadi anahitaji kuabudiwa?

Huyo Mola akisha abudiwa anapata nini zaidi?

Hivi huyo Mola anajielewa kweli?
Ukisikia Mola Mlezi:
Jua kuwa ni Jini:
Mola atakuwaje Mlezi wakati hana mwana:
Analea nini sasa:
Au analea Majini
 
Mimi sijasema hakuna Mungu wanaosema hakuna mungu wote hawana akili
Thibitisha Mungu yupo.

Thibitisha una akili.

Ulisema mimi sina akili, Sawa.

Sasa wewe mwenye akili, ithibitishe hiyo akili uliyonayo.
 
Yaan saa 6 hii usiku ndio nafika home. Nimetoka kwenye kadamsee.

Bro. Utetezi wako una mashaka.
Lakini Nitasoma comment huko mbelebi . Ila kwakuwa hii ni comment ndio ya kwanza nasoma . Na umejibu swali moja .

La kwamba nani Muislam wa kwanza.

Na ambalo hujajibu kwa Quran kwamba je ? Unaweza kuwa muislam kama haujafanya
1. KISILIMU
2. SHAHADA

AU ww unapingana na huu mstari wa Quran ambayo hauna shaka .

Kasome

Surah Al-An'am (6:163)
: "Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu (walio jisalimisha kwa Mwenyezi Mungu)."

Surah Az-Zumar (39:12)
: "Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa Waislamu."

Surah Al-An'am (6:14)
: "Sema: Je, nimfanye mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi? Naye ndiye anaye lisha wala halishwi. Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu..."

2. Nionyeshe mtume yoyote zaid ya Mohamed aliyefanya SHAHADA.
Kwa Biblia na Quran.

(Ukinjonyesha Ntakutumia 1 Million Tsh. Ambayo iko kwa uwezo wangu. Tuwasiliane PM)

Nguzo ya kwanza ya Uislam ni Shahada
Na Shahada ni hii

"Ash-hadu an la ilaha illa Allah, wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulu-Allah.
Maana: "Nashuhudia kuwa hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu (Allah), na nashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Sitak maneno. Niwekee kwa Biblia au Quran nani alisema haya nje ya Mohamed.

Nalala sasa . Nikiamka. Ntajibu comment zote.
Jagina pita na hapa mkuu
 
Back
Top Bottom