Quran ya Allah ni kitabu kisichokuwa na shaka

Quran ya Allah ni kitabu kisichokuwa na shaka

Uislamu ni tamko la mwisho la ujumbe wa asili wa Umoja wa Mwenyezi Mungu. Maana yake ni kujisalimisha kikamilifu kwa Mola Mmoja wa haki, Mlezi wa viumbe vyote, Mwenye uwezo wote, aliyeko kila mahali, na Msimamizi wa dunia na wanadamu. Anayejisalimisha kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu huitwa Muislamu.

Uislamu unasisitiza kwamba Mwenyezi Mungu (Allah) ndiye Muumba na Mtawala wa kila kitu, na mwanadamu ni khalifa Wake duniani. Hali hii humuinua mwanadamu hadi katika cheo cha heshima na utu, akiwa ni naibu wa Mwenyezi Mungu katika ardhi, na huipa maisha yake kusudi tukufu: kutekeleza mapenzi ya Mwenyezi Mungu duniani. Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, Mwenyezi Mungu alimuumba mwanadamu awe msimamizi wa dunia. Mwanadamu hupata uwezo juu ya maumbile na ulimwengu kwa njia ya elimu na juhudi, yaani kwa maarifa na matendo.

Uislamu unafundisha kuwa wanadamu wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu na ni sawa mbele Yake. Ubaguzi wowote unaotokana na rangi, tabaka, kabila au eneo hauna msingi wa haki, bali ni dhana ya upotofu iliyosalia kutoka zama za ujinga zilizowafunga wanadamu katika minyororo ya utumwa.

Mwenyezi Mungu ameteremsha uongofu Wake kupitia Manabii Wake na Vitabu Vitakatifu kwa baadhi ya Mitume Wake. Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ndiye Mtume na Nabii wa mwisho, na Qur’ani Tukufu ni ufunuo wa mwisho kwa wanadamu wote.

Mafundisho ya Uislamu ni mepesi, wazi na yanayoeleweka, hayana khurafa wala imani zisizo na mantiki. Umoja wa Mwenyezi Mungu ( One ness au Tawhid), Utume wa Muhammad (s.a.w), na imani ya maisha ya Akhera ni misingi mikuu ya imani ya Kiislamu. Mafundisho yote ya Uislamu hutokana na misingi hiyo. Hakuna daraja la makasisi, hakuna nadharia tata zisizoeleweka, wala ibada nzito na ngumu.

Uislamu ni mfumo kamili wa maisha, si dini kwa maana finyu iliyozoeleka, kwani hauishii katika maisha binafsi pekee, bali unatoa mwongozo kamili katika kila nyanja ya maisha ya mwanadamu.

Mwenyezi Mungu hana mshirika wala msaidizi katika Uungu au mamlaka Yake. Yuko juu ya maumbile Yake, hana umbo la kimwili, wala hayupo katika kitu chochote cha kimaada.

Katika Uislamu, hakuna mfano unaolingana na Yeye, japokuwa wanadamu wanaweza kujitahidi kuakisi baadhi ya sifa Zake kama haki, rehema na uadilifu. Mwenyezi Mungu hana mtoto, hana kabila, hana jinsia, hana mwili, wala haguswi na sifa za maisha ya kibinadamu.

Wanadamu kwa asili yao ya kiroho wameumbwa katika hali ya Uislamu (fitra), lakini kwa kuwa wamepewa akili, uamuzi na hiari, wanaweza kubaki katika njia ya uchamungu na uongofu kuelekea radhi na thawabu za Mwenyezi Mungu, au wanaweza kupotoka kutokana na malezi na chaguo zao za maisha. Qur’ani Tukufu inasisitiza kuwa hakuna kulazimishwa katika dini.

Jukumu la Muhammad (s.a.w) kama Nabii wa mwisho lilikuwa kuthibitisha mafundisho ya kweli ya Manabii waliomtangulia, na maisha yake ni mfano mkamilifu wa kuufuata Uislamu kwa ukamilifu.

Waislamu wanaamini Malaika, viumbe wasioonekana wanaomuabudu Mwenyezi Mungu na kutekeleza amri Zake katika ulimwengu mzima.

Waislamu pia wanaamini kwamba Siku ya Kiyama, wanadamu watahukumiwa kwa matendo yao ya duniani. Ujuzi wa wakati wa siku hiyo uko kwa Mwenyezi Mungu pekee; hakuna ajuaye isipokuwa Yeye (Qur’ani 7:187).

Qadar (makadirio ya Mwenyezi Mungu), ambayo ni miongoni mwa nguzo za imani, ina maana kwamba kila linalompata mwanadamu limo ndani ya elimu na maamuzi ya Mwenyezi Mungu. Muumini anapaswa kuyapokea mema kwa shukrani na mabaya kwa subira. Dhana hii haipingani na hiari ya mwanadamu, kwani wanadamu hawajui makadirio ya Mwenyezi Mungu kabla ya kutokea, hivyo wana uhuru wa kuchagua.

Qur’ani Tukufu inasema: “Mwenyezi Mungu haibebeshi nafsi mzigo unaozidi uwezo wake.” Hivyo, Uislamu hauhimizi kujitenga na dunia au useja wa lazima. Dunia si ufalme wa Shetani, wala mwili si makao ya dhambi.
Katika Injili za Kikristo, Mungu huitwa Baba; katika Qur’ani Tukufu, Yeye ni Mola.
Kauli Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkuu) inathibitisha kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.

Maelezo mareeefu.
Haujajibu hata hoja moja.
 
usigeuke CCM au wewe ni Abdul mtoto wa Samuyu unatoa amri tu 😛 kama hujui english tafuta mkalimani .

Hakuna Mungu wa kuabudiwa ila Allah . ikiwa wakati wa Adam itakuwa walitamka Hakuna Mungu ila Allah na Adam ni mtume wa Allah , wakati wa Noah ita kuwa ni Noah rasulullah na wakati wa Yesu itakuwa yesu rasulullah na wakati wa Muhammad ni Muhammad rasulullah <<<<<< Amani iwaendee wote
Kumbe na mimi nikishahadia
Ash-hadu an la ilaha illa Allah, Wa ash-hadu anna Yashua Hamashiach -Allah.
Nakua tayari Mwislamu,sasa kwanini mnalazimisha tumwamini mtume wenu Muhammad na sisi ni wafuasi wa Yesu?
😁😁😁
 
Quran imejaa visa vya wanawaisrael Kwa sababu wao ndio walikuwa wanaenda Kwa mtume na kumpa challenge Kwa kumuuliza mambo ya manabii wa wazamani na mambo ya wachamungu wa zamani

Alafu kitu ambacho nyinyi wagalatia hamkijui ni kuwa hakuna muisraeli anayepinga kuwa Muhammad sio mtume wa Mungu

Shida ipo kwenu wagalatia na ni Kwa sababu Wazungu wamekudanganyeni sana

Bila shaka hapa unajibu hoja yangu ya kwanza.
Ila heb irudie kuisoma tena.

Umakini weka kwenye kitabu cha torat. Ambacho quran inasema kapewa Mussa.
Je visa ving mfano cha Yona au Yunus kiko kwenye torat?.
Jibu ni hakiko.
Kwahiyo na hivo Visa mohamed alishushiwa Wahyi?😁😁😁😁
 
Yaan saa 6 hii usiku ndio nafika home. Nimetoka kwenye kadamsee.

Bro. Utetezi wako una mashaka.
Lakini Nitasoma comment huko mbelebi . Ila kwakuwa hii ni comment ndio ya kwanza nasoma . Na umejibu swali moja .

La kwamba nani Muislam wa kwanza.

Na ambalo hujajibu kwa Quran kwamba je ? Unaweza kuwa muislam kama haujafanya
1. KISILIMU
2. SHAHADA

AU ww unapingana na huu mstari wa Quran ambayo hauna shaka .

Kasome

Surah Al-An'am (6:163)
: "Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu (walio jisalimisha kwa Mwenyezi Mungu)."

Surah Az-Zumar (39:12)
: "Na nimeamrishwa niwe wa kwanza wa Waislamu."

Surah Al-An'am (6:14)
: "Sema: Je, nimfanye mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi? Naye ndiye anaye lisha wala halishwi. Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu..."

2. Nionyeshe mtume yoyote zaid ya Mohamed aliyefanya SHAHADA.
Kwa Biblia na Quran.

(Ukinjonyesha Ntakutumia 1 Million Tsh. Ambayo iko kwa uwezo wangu. Tuwasiliane PM)

Nguzo ya kwanza ya Uislam ni Shahada
Na Shahada ni hii

"Ash-hadu an la ilaha illa Allah, wa ash-hadu anna Muhammadan Rasulu-Allah.
Maana: "Nashuhudia kuwa hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu (Allah), na nashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Sitak maneno. Niwekee kwa Biblia au Quran nani alisema haya nje ya Mohamed.

Nalala sasa . Nikiamka. Ntajibu comment zote.
Umeamka sasa wamekujibu?
😁😁😁
 
Hii narrative ipo lakini si ya kweli
Quran 25:4-5 imeonesha mtume alisimamia uandishi wa Quran

Nionyeshe wap Mtume amesimamia Quran.

Quran 25 : 4-6
Aya ya 4: "Na wamesema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uzushi alio uzua, na wamemsaidia kwa haya watu wengine! Hakika hawa wamekuja na dhulma na uwongo."
Aya ya 5: "Na walisema: Ni hadithi za watu wa kale alizo ziandikisha, naye anasomewa asubuhi na jioni."
Aya ya 6: "Sema: Ameteremsha (Qur'ani hii) yule anaye jua siri zilizomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu."

Kumbuka aliyeandika Quran sio Mohamed. Yeye hakujua kusoma wala kuandika. Na ilikusanywa na kuwekwa pamoja kwa miaka 20 baada ya yeye kufariki.
 
Ila ukisoma Quran utakutana na vituko vya Allah ku ji self diffence ,yaani anasema kitu kwa kujikingia kifua kama asihojiwe vile hii inathibitisha Allah ni mungu wa mchongo yaani ambaye hata matukio aliyoyafanya zamani zile hana kumbukumbu nayo anakopi kwa old text hamna Allah hapo!
😁😁😁
 
Jagina tuachane na swali la kwanza. Hebu nijibu la 3.

Kwanini ikichukua miaka 23 kukamilika wakat Quran ilishushwa yote kwa siku moja kwenyw mbingu ya kwanza.?.

Quran ni janja janja tu ya mohamed. Hakuwah kupata wahyi ila ni ndoto zake .
Akiamka anasema nimeoteshwa
 
Ila ukisoma Quran utakutana na vituko vya Allah ku ji self diffence ,yaani anasema kitu kwa kujikingia kifua kama asihojiwe vile hii inathibitisha Allah ni mungu wa mchongo yaani ambaye hata matukio aliyoyafanya zamani zile hana kumbukumbu nayo anakopi kwa old text hamna Allah hapo!
😁😁😁

Allah anayemuomba Allah.

Qurani 33:56
"Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu."

Na eti ukimsalia mtume unaondolewa dhambi za siku 10 😁😁😁😁 yaan mtume anaswaliwa. Kwanini aswaliwe?.
Yeye si mtume? Au ana madhambi? .
 
Hua nashindwa kuelewa Quran mpangilio wake na visa vyake yaani ni kichekesho aisee!
😁😁
 
Uislamu ni dini ambayo Allaah ameichagua kama mfumo sahihi wa maisha kwa Wanadamu wote na tokea Nabii wa kwanza Baba yetu Aadam (Peace be upon Him ) alikuwa Muislamu na Manabii wote Musa , Yesu , Nuhu , Ibrahimu , Yakubu nk (Amani iwe juu yao wote ) dini yao ilikuwa ni Uislamu na walilingania katika Uislamu .

Sheria tu zilitofautiana kutoka na zama lakini misingi mikuu ile ile ambapo msingi mkuu unawaunganisha wote kuwafanya wawe Waislamu ni Tawheed maana yake kumpwekesha Mola muumba pekee kwa kumuabudia yeye tu bila kumshirikisha . Ndio maana hakuna Nabii akiyekuja kudai kuwa yeye ni Mungu au kiabudiwe kingine kinyume na Mungu muumba (Allaah)

Manabii wote walikuja kukingania watu waachane na maovu , wafanye mema kwa kumtii mola wao huo ndio Uislamu . Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah mola muumba kwa kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha kufuata maarisho yake na kuacha makatazo kama jinsi alivyoolekeza kupitia Manabii na wajumbe wake.

Ndio maana tunasema Uislamu ukikuwepo tokea mwanzo na Manabii wote walikuwa Waislamu sababu walikuwa kwenye misingi hiyo , tofauti ipo kwenye baadhi ya Sheria tu sawa na Leo I phone zote ni I phone zina sifa za kipekee kuitwa I phone pamoja na kuwa na matoleo tofauti kutokana na maboresho ila sifa za kipee zinazofanya kuwa I phone lazima zitabaki kama msingi
Tumia akili wewe mbuzi .. dini gani hiyo ni ushirikina mtupu DINI INAYO TEGEMEA KIARABU NDIYO UMUOMBE NA KUMCHA MUNGU KWA HIYO LUGHA 👉💩💩
 
Allah ni Mzimu wa kabila la Kiarabu tu:
Ukitaka kuwasiliana na Mzimu wa Kabila Fulani ni lazima utumie Lugha ya Hilo Kabila:
Mfano
Kabila la Wanyakyusa huongea na Mzimu wao kwa Lugha ya Kinyakyusa tu:
Na ni Mwiko (Haramu) kutumia Lugha yoyote Ile isipokuwa Kinyakyusa:

Waarabu wakaandika kitabu Cha namna ya kumwabudu Mzimu wao na kushawishi na kulazimisha makabila mengine wamwabudu:

Mzimu ambao ili ukuelewe ni lazima uwasiliane nao kwa Lugha ya Kiarabu tu, na pia ni lazima Uusujudie ukitizama Uarabuni Saudi Arabia:
Ukiongea Kiarabu huku umesujudu kuelekea Malawi haukusikii:

Ukisoma hapa kwa kuweka ushabiki pembeni utaelewa vizuri:
 
Uislamu ni dini ambayo Allaah ameichagua kama mfumo sahihi wa maisha kwa Wanadamu wote na tokea Nabii wa kwanza Baba yetu Aadam (Peace be upon Him ) alikuwa Muislamu na Manabii wote Musa , Yesu , Nuhu , Ibrahimu , Yakubu nk (Amani iwe juu yao wote ) dini yao ilikuwa ni Uislamu na walilingania katika Uislamu .

Sheria tu zilitofautiana kutoka na zama lakini misingi mikuu ile ile ambapo msingi mkuu unawaunganisha wote kuwafanya wawe Waislamu ni Tawheed maana yake kumpwekesha Mola muumba pekee kwa kumuabudia yeye tu bila kumshirikisha . Ndio maana hakuna Nabii akiyekuja kudai kuwa yeye ni Mungu au kiabudiwe kingine kinyume na Mungu muumba (Allaah)

Manabii wote walikuja kukingania watu waachane na maovu , wafanye mema kwa kumtii mola wao huo ndio Uislamu . Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah mola muumba kwa kumuabudu yeye pekee bila kumshirikisha kufuata maarisho yake na kuacha makatazo kama jinsi alivyoolekeza kupitia Manabii na wajumbe wake.

Ndio maana tunasema Uislamu ukikuwepo tokea mwanzo na Manabii wote walikuwa Waislamu sababu walikuwa kwenye misingi hiyo , tofauti ipo kwenye baadhi ya Sheria tu sawa na Leo I phone zote ni I phone zina sifa za kipekee kuitwa I phone pamoja na kuwa na matoleo tofauti kutokana na maboresho ila sifa za kipee zinazofanya kuwa I phone lazima zitabaki kama msingi
Ila Mudi ana vituko. Alienda mbinguni kumshauri allah alegeze kuswali mara 50 kwa siku it's too much afanye mara 5. Eti allah akaridhia.

Dah islam
 
Allah ni Mzimu wa kabila la Kiarabu tu:
Ukitaka kuwasiliana na Mzimu wa Kabila Fulani ni lazima utumie Lugha ya Hilo Kabila:
Mfano
Kabila la Wanyakyusa huongea na Mzimu wao kwa Lugha ya Kinyakyusa tu:
Na ni Mwiko (Haramu) kutumia Lugha yoyote Ile isipokuwa Kinyakyusa:

Waarabu wakaandika kitabu Cha namna ya kumwabudu Mzimu wao na kushawishi na kulazimisha makabila mengine wamwabudu:

Mzimu ambao ili ukuelewe ni lazima uwasiliane nao kwa Lugha ya Kiarabu tu, na pia ni lazima Uusujudie ukitizama Uarabuni Saudi Arabia:
Ukiongea Kiarabu huku umesujudu kuelekea Malawi haukusikii:

Ukisoma hapa kwa kuweka ushabiki pembeni utaelewa vizuri:

Una hoja . Usikilizwe.

Alaf kulibusu jiwe jeusi ni mistake nyingne wamefanya.
Jiwe lililokuwa lina busiwa na wapagan wa Kikurshi.
Mashemej zake na Mohamed
 
Ila Mudi ana vituko. Alienda mbinguni kumshauri allah alegeze kuswali mara 50 kwa siku it's too much afanye mara 5. Eti allah akaridhia.

Dah islam

Na aliwaongoza mitume iliyopita kuswali 😁😁😁😁
Hadi Yesu alikuwepo anafundishwa na kuongozwa swala na Mohamed.
Dah.

Alaf wao kutwa kucha wanatunanga wakristo kumbe kwao kumejaa upupu wa karne.
 
Ndugu yangu Covax .
Haujaonekana na haujajibu hoja zangu siku nying sana.

Najua unasoma na unapita kimya kimya.

Najua unasubiria upepo utulie ili uje na hoja zako.
Nikuambir tu kuwa Ukiendelea kuchambua Biblia na sisi tutaendelea kuchambua Uislam.

Maandishi haya yatakuwepo na watu watasoma na kuona dini ipi ni ya magumashi.
 
Nina hoja nyingne 2. Nazitunza for future use.
Save the best for the Last.
 
Mtoa mada kasome surat al-hajj 2:20 (hapa utaona utofauti kati ya masinagogi na misikiti), pamoja na surat al-anaan 6:14 (hapa utajua binadamu wa kwanza kuwa muislam)

Sisi wakristo tunaamini kuwa yesu alikuwa na mapokeo ya kikristo au kiyahudi ndiyo maana alifuata dini ya kiyahudi tazama luka 2:27, alishiriki pasaka iliyokuwepo enzi na enzi tazama yohana 2:13, 23; luka 22:7-8, vile vile alishiriki siku kuu ya vibanda tazama yohana 7:2, 10.
-yesu ndiye mwanzilishi wa kanisa tazama mathayo 16:18.

Nauliza, paul mnayempinga kila siku naye alikuwa muislamu kisa tu aliingia kwenye sinagogi? Tazama matendo ya mitume 17:1-2

1. Tuonyeshe hapa kwenye biblia au quaran ni siku kuu gani ya kiislamu ambayo yesu aliishiriki kama muislamu?
2. Kama quaran ni kamilifu kwa nini mnaagizana huko majarubani kuwa mkishindwa kuelewana muwatafute wale waliowatangulia katika kitabu? Na ni nani hao na ni kitabu gani?
 
Back
Top Bottom