SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png


Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png


Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png


Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 

Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
This is the lesson to respect people even in unknown ID.
RIP ip_mob
Naungana na wewe kabisa....@mods hatuwafundishi kazi lkn nadhan kuna haja ya kusimamiwa nidhamu humu ndani ya @jf .....wkt mwingine ktk baadhi ya nyuzi kuna watu hawana adabu wanatukana ovyoo hii sio nzuri kwani inashusha hadhi ya @jf
 
Sio kama JF inakataza kutuma hadharani Mazungumzo yaliyofanyika Faragha almaarufu kama PM [emoji848]
Ama hii sheria ilibadilishwa tuanze kulipuana humu, [emoji2]

Maxence Melo ufafanuzi wako tafadhali.

Mkuu nimesema hapo awali, sijui hio sheria sio kila mtu anasomaga sheria

Kama hairuhusiwi nimesema kabisa mods wanapitia wataufuta uzi au kufanya maamuzi wao
 
Kuna watu humu wanatuchezea vimchezo hili wapate trending mimi kama mshiriki wa shindano nilipo hoji hili suala watu walinijia juu kwamba sikutakiwa kumuhoji !!!!!

Kwakuunganisha vitu hivi hata tukienda mahakani sasa hivi namfunga huyu jamaa yeye ni JF expert kabisa siyo mgeni alafu anasema kwamba kakosea kupost kwenye shindano la uandishi wakati ukiingia tu kwenye home page ya stories of change lazima kuna muongozo na muongozo siyo kwenye jukwaa hili tu ni kwenye majukwaa yote kwahiyo kwa level yake ya JF expert mimi akiniambia kakosea nakataa sasa alipostije wakati kwenye majukwaa yote yana matangazo yaliyo baniwa juu kabisa.


Cha pili jamaa chapisho lake lina maneno mia 800 ambayo ni maneno yanayo itajika kwenye hili jukwaa alafu yeye anasema hajui kama kuna shindano kwahiyo aliwezaje kuandika maneno yote haya na story yote hadi ya private chat katuonyesha alafu anasema hajui kama anashiriki shindano kwahiyo nakataa siange andika tu kwa ufupi kwamba RIP flani kwahiyo mimi napinga.



Alafu anasema taarifa ya kifo cha rafiki yake kapata mwaka 2018 alafu taarifa za msiba anatangaza 2022 kwenye shindano alafu anasema yeye wala hashindani inamaana miaka yote hiyo alikuwa wapi kwahiyo mimi nimepinga kwamba huu ni unafki.


Alafu anasema huyo rafiki yake anaye dai amefariki kuwa yeye hajawai kumuona amesikia tu kwa mtu kuwa amefariki na hana ushahidi kuwa yupo hai au amekufa kwahiyo mimi nikisema anamsingizia nitakuwa nakosea ? Mimi nikikataa kuwa jamaa hajafa nitakuwa nakosea ?

We jamaa una tatizo la kisaikolojia, na una shida sana kichwani kwako.

Kuna taarifa hapa unasema either kwa kupotosha au uko blinded na shindano kiasi kwamba unashindwa kufanya judgement yako vizuri.

Wapi nimesema taarifa za kifo nimepata 2018? Nimekuwekea na evidence hapo ila unashupaza shingo. Soma tena chats tuliza akili kijana. Na soma uzi ule wa 2019

Nimekwambia kwamba uzi ni wa 2019, taarufa za kifo ame comment mdau mwezi wa 3 mwaka huu kuwa jamaa emfariki mwaka jana 2021.

Tatizo vijana mnakurupuka tu mnadhani kila mtu yuko obsessed kama nyie? Sio kila mtu anasoma terms sjui maelekezo ya jukwaa, sijawah soma maelekezo ya jukwaa. Acha kulazimisha mambo kijana.

Hili suala liliisha na ukaomba radhi, nikadhani ni mtu mstaarabu na unajielewa, kitendo cha kuendelea nalo kina reflect namna gani bado hauko matured.

Sitabishana na wewe tena, hili suala. All the best
 
Aah huyo anakuchezea akili tu, nilipoona amepost mazungumzo ya faragha nimeshtuka na nimeshangaa pia kuona uzi upo hadi muda huu wakati nakumbuka kabisa sheria za JF haziruhusu na kifungo chake chaweza kua cha Maisha,


Eenh, amesema huyo Ip amefariki na taarifa kazipata tangu mwaka 2018 ila mwaka 2022 ndio ameamua kuzileta humu!! Kwanini achelewe?? Na tofauti na mazungumzo yao ya PM walishawahi kuzungumza kwa simu ama kukutana?? Amejihakikishia vipi aliyemwambia taarifa za kifo alimpa taarifa kamili???

Anyway, nikutoe tu wasi wasi bwana Moris kama wewe ni Mshiriki wa Shindano na huyu bwana Mutu Murefu anashiriki pia shindano hilo basi hana tishio kwako, ajaribu tena kuleta habari inayobeba ujumbe mzito na kubadili Maisha ya wengi na sio habari za kutilisha huruma wakati Kifo wote ni njia yetu LAZIMA TUFE,

Ngoja nikafagie banda la Kuku mie,

Wasalaam.

Naomba soma tena uzi sijasema taarifa za kifo ni 2018, naomba msipotoshe mada tafadhali
 
Mimi nakushangaa sana kaka, unauhakika huyu jamaa ka graduate ? Kaka ujashtuka kuona chapisho la misiba kwenye jukwaa la shindano ?


Kaka huyo mtoa post kasema kwamba rafiki yake hajawai kumuona wala hawajuani na taarifa za misiba kapata 2018 inamaana hana ushahidi na msifanye sifa kwa sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutangaza misiba kwenye majukwaa ya watu bila uthibitisho wa watu wawili watatu ni kosa la jinai !!!!

Unapotosha kwa makusudi kabisa kijana, kuhusu msiba soma tena post yngu

Kuhusu vyeti nakutumia hapa hapa jf, nakuonesha nimegraduate mwaka 2019

Usipende kupotosha maada kwa sababu zako za kijinga
 
Kwa sasa umeshapata kaz umejenga,una usafiri, na ofisi pia Kwanini siku uliyopata kazi hukumtafuta na kumpa hata taarifa tu? Maana kwa mafanikio yako haiwezekani yawe ya ndani ya miez mitatu tu na Jamaa wala hajafariki siku nyingi lakin hakuna hata sehem uliyomtafuta kumjulisha.

Jamaa apumzike kwa amani katufundisha pia siyo kila utakae msaidia atakukumbuka baada ya mafanikio yake, watasubiri ufe ndo wa Tangaze wema wako hali ya kua itakua haina maana tena.
 
Mimi nakushangaa sana kaka, unauhakika huyu jamaa ka graduate ? Kaka ujashtuka kuona chapisho la misiba kwenye jukwaa la shindano ?


Kaka huyo mtoa post kasema kwamba rafiki yake hajawai kumuona wala hawajuani na taarifa za misiba kapata 2018 inamaana hana ushahidi na msifanye sifa kwa sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania kutangaza misiba kwenye majukwaa ya watu bila uthibitisho wa watu wawili watatu ni kosa la jinai !!!!

Na wewe kwanini unatupotosha? Mtoa Mada wapi kasema taarifa alizipata 2018 wakati maongezi yao yanaonesha yalianzia mwaka 2019 kwa mujibu wa hizo screenshots,

Kama upo kwenye shindano kwanini usijikite kuandika Mada nyingi zaidi zenye mashiko kuliko kushinda kwenye bandiko la mwenzio kumsagia kunguni???

Kwenye Shindano Mtu hutumia njia zozote ili ashinde, hukuona juzi kwenye Darby Morisson alidondoka na kujifanya yu hoi taabani walivyombeba kumtoa nje akaruka na kurudi uwanjani hiyo ni baada ya dakika 4 za nyongeza na aliporudi mpira ukaisha, hizo ni mbinu za ushindi,

Ushauri wangu endelea kujipanga upambanie ushindi wako na sio kutolea macho wengine.
 
Hongera sana. Hukumuangusha Mwamba, tofauti na vijana wengi akishakuzoea tu Ni mizinga. Niliwahi kumsaidia dogo Fulani scholarship ya LLM -Syracuse University, tukapambana akapata baadae akaiacha eti home wamemuambia US watu wanauana Sana

Aisee nashukuru sana kaka

Uyo dogo kwa kweli alichezea sana bahati, yani alitoa excuse ya kijinga mno

Lakini nakupongeza mkuu ulipambana nae, ulitimiza wajibu wako
 
Futa tu hizo picha,
Huyo unayekazana kumuhakikishia hana kitu zaidi ya chuki na njaa ya ushindi,

Linda Faragha yako usijiweke wazi sana, Inatoshaaaaaaaa

Sawa mkuu nashukuru sana

Ngoja niziondoe sasa.
 
Hahaha thanks!
how did u know my name, ukute ww ni classmate wangu pale MUHAS
I know you more than you think.
I know you since the day you started your ordinary level at seminary, a level at the same seminary. And first degree at mzumbe and masters at muhimbili.

Guys napenda kuwaambia huyu dogo mutu murefu is real genius I know him, yuko fit kichwani namfahamu sana Sina mengi ya kueleza lakini Mimi ndiye ninamjua he is very talented more than you think.
 
Kwa sasa umeshapata kaz umejenga,una usafiri, na ofisi pia Kwanini siku uliyopata kazi hukumtafuta na kumpa hata taarifa tu? Maana kwa mafanikio yako haiwezekani yawe ya ndani ya miez mitatu tu na Jamaa wala hajafariki siku nyingi lakin hakuna hata sehem uliyomtafuta kumjulisha.

Jamaa apumzike kwa amani katufundisha pia siyo kila utakae msaidia atakukumbuka baada ya mafanikio yake, watasubiri ufe ndo wa Tangaze wema wako hali ya kua itakua haina maana tena.

Nimekiri hapo juu kuwa nilifanya mistake, jamaa last time kuwasiliana ilikua mwaka jana mwanzoni na ndipo alipofariki,

Sijapata mafanikio ndani ya miezi 3, kipindi alipokua ananiunganisha nilikua nimefikia hatua fulani kwnye miradi yangu (ila sikua nimetimiza ndoto ya kuajiriwa kwenye international organizations) baada ya kupata huku wanalipa salary ndefu sana yani sana, kujenga ni rahisi tu

Mwaka jana nikapata kwnye int organisation na wakati huo nilikua namtafuta simpati, kumbe ndo alikua amefariki, taarifa nimezipata mwaka huu mwez wa 3
 
I know you more than you think.
I know you since the day you started your ordinary level at seminary, a level at the same seminary. And first degree at mzumbe and masters at muhimbili.

Guys napenda kuwaambia huyu dogo mutu murefu is real genius I know him, yuko fit kichwani namfahamu sana Sina mengi ya kueleza lakini Mimi ndiye ninamjua he is very talented more than you think.

Mkuu nakujia PM tufahamiane, naomba usiendelee ku disclose information humu
 
Mungu amuweke anapostahilk

Ila tujifunze nidhamu ya kuwa tunatoa shukurani na pongezi kwa watu ilhali bado wapo hai na wanaona.

Ile hatua ya kwanza tu uliyopiga, yaani ku graduate vizuri. Ulipaswa kuandika uzi wa shukurani humu.

Mawasiliano ya mara kwa mara hata salamu tuu, pia yalikua ni ya muhimu sana.

Tujifunze kujifunza ndugu zangu namna ya kumaintain mahusiano.
Kilichobaki sasa ni wewe kufanya chini juu kuitafuta familia yake na kama ana watoto sio mbaya ukajitolea kiwa sehemu ya maendeleo yao.

Naamini hii itasaidia sana, napia kuwafariji mno

Utakua umetimiza ule msemo

" Matendo mema huwa yanaishi siku zote"

Haya ni maoni yangu, and i stand to be corrected.

Pole

Amina nitafanya hivo mkuu barikiwa
 
Back
Top Bottom