SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png

Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png

Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png

Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 
Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Nashukuru sana mkuu, nimefurahi pia kufahamiana na wewe.

Maana kwenye hizi fake IDs tuna marafiki kaka na ndugu. Mungu akubariki, nimekucheki PM
Siwez ku disclose informations. Ni kujaribu ku justify uwezo wako
 
Watu tunajua kuna misiba Kumbe ni chai bhana account fake kibao hapo na nyingi ni zako na ndizo zimekupigia kura fake account wewe
 
Kwani wewe unaongelea shindano gani mbona una hila kwa mwenzio?

Watu wako obsessed sana na mashindano, wanadhani kila mtu anashinda humu ndani kufuatilia mashindano. Ukipost kitu wanadhani unashindana nao.

Wengine ni jf expert members humu, tuna miaka mingi ila tuna nyuzi chache tumeandika, ila tunaingia mara moja moja, huo mda mwa kusoma maelekezo ya kila jukwa hatuna. Tunapost mada tuna comment chachw tunasepa.

Ss hawa teenagers wameingia juzi humu, wanashinda wanazulula kusoma kila kitu majukwani na kuanzisha nyuzi kila saa wanadhani kila mtu yuko kama wao

Ukishamjua mtu na akili yake unamu ignore tu
 
Kumbe upo humu tangu miaka kumi nyuma alafu huoni aibu unasema umekosea kupost alafu mpaka sahivi unasema ujui heti kama kunashindano who are you!!!

sisi tupo serious kwenye shindano, ungekuwa utaki kukosolewa usinge weka andiko za misiba kwenye jukwaa hili nakuona tangu Jana unasisitiza kufuta chapisho alafu ufuti inamaana wewe unashindana kwenye shindano kwa visingizio vya misiba hili uonewe huruma.

Kama utaki kukosolewa futa chapisho usubiri shindano lihishe kwanza ndiyo upost usichanganye watu sisi tupo serious humu na Nina haki ya kulinda kura zangu na kuhoji machapisho yote humu.

Kwahiyo mpaka chapisho lako lime pitishwa na moderators inamaana wewe ni mshiriki wa shindano moja kwa moja alafu acha unafki bado unatwambia ujui kama kuna shindano naomba nikueleze sisi tupo kwenye shindano na lengo letu ni ushindi kuna machapisho tumeona yana eleza mambo ya kuhuzunisha ili zitrend usilazimishe tukuamini na nilazima tukuhoji.
 
Okay
 
I know you more than you think.
I know you since the day you started your ordinary level at seminary, a level at the same seminary. And first degree at mzumbe and masters at muhimbili.

Guys napenda kuwaambia huyu dogo mutu murefu is real genius I know him, yuko fit kichwani namfahamu sana Sina mengi ya kueleza lakini Mimi ndiye ninamjua he is very talented more than you think.
I agree,,, Nakumbuka pale Seminary kwenye mahafari, wakati Mimi nasoma Pre form five (EGM). Alishusha bonge moja la Shairi. He is genius.. Sisi tunaokujua na kukufahamu hatuna Shaka. Hasa uwezo mkubwa ulionao.
 
Ha ha ha mkuu umenikumbusha mbali sana, those days.. poems za „to my daughter, shaped woman etc“

Kumbe mkuu nnavomaliza form 6 we nilikuacha pre - form 5… umesoma na akina leah mpogole?
 
I agree,,, Nakumbuka pale Seminary kwenye mahafari, wakati Mimi nasoma Pre form five (EGM). Alishusha bonge moja la Shairi. He is genius.. Sisi tunaokujua na kukufahamu hatuna Shaka. Hasa uwezo mkubwa ulionao.

Nakuja PM mkuu kama hutojali, i miss those days seminarini. Tujikumbushe the moments
 
Machozi yamenitoka asee[emoji26][emoji26]

Huyu jamaa alikuwa anapenda kunitania ( but utani wenye heshima)

Kumbe kafa daah[emoji26][emoji848]
 
Back
Top Bottom