SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi


Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)


Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University


Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 

Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Wewe si uliomba msamaha mbona kichwa kinawaka moto tena asee[emoji848][emoji848][emoji848]

Sasa akishindana we kinakuuma nini?
 
As a man una lia lia sana bhana hadi nahisi kama mimi ndo napoteza viungo
[emoji16][emoji16][emoji16] asee anatia aibu kinoma....kibaya zaidi aliomba radhi...heee mara kawaka tena

Haya mahasira na uwendazimu mostly tunayo sisi wanawake sio wanaume mweeh[emoji848]
 
Mbona kama naona id mbili za mtu mmoja mmoja ke mwingine me, zinakushambulia mleta uzi[emoji848][emoji849][emoji849]
 
Daaa inasikitisha sana. Kuna mtu aliwahi kusema wherever you go utawakuta watu watakaokushika mkono ambao watafanyika ndugu au wazazi wako huko ulipo.

Hongera sana ulipata mtu wa kukushika mkono na alipomaliza kazi yake alitokomea kama mshumaa gizani. Its painful hasa kwako ambae ulimfaham na JF members wote pia.

Sis tu wapitaji tu katika haya maisha, amemaliza kazi yake tumruhusu apumzike lakini najua nawe una deni la kulipa pia kwa JF,family ya ip- mob na jamii kwa ujumla. Get strong move on🇹🇿
 
May he rest in peace, vizuri havidumu Mungu aendelee kumlaza mahali pema peponi. Ukipata chansi pia usisite kumshika mkono mtu anayehitaji msaada iwe chain aliyoianzisha Ip.
 
Mkuu nimesoma uzi kwa masikitiko sana ila wewe umenifanya nikachekaa, kwani ulikuwa na shida gani aisee?? Je ulishinda hilo shindano maana ulikuwa unamsagia sana kunguni mwenzio uliona ni threat kwako au?
 
Pumzika kwa Amani brother,
Ulifeli kushindwa kuwa na mawasiliano naye nje ya JF, alikuwa mtu muhimu sanaa lkn hukuonyesha Nia yakuwa karibu nae zaidi
 
Rip ip bob... Kiukwel JF ni jukwaa la msaada kwa members... Lkn saiv kuna kundi la vijana ambao always wanacommet upuuzi tu mtu akiomba msaada wa mawazo... Ila ndio kizazi kipya kina changmoto nyingi... Pia tuige mfano wa ip bob tuache ujinga wa fb na insta
 
Watu kama nyie ndio mlitufanya watu kama sisi tunyamaze humu JF..unamkosea mwenzio kwasababu ya upeo wako mdogo ..na kwasababu huelewi unalazimisha kwa akili yako hiyo hiyo ndogo...akubaliane na ujinga wako
 
Huu uzi nimeusoma japo kwa kuchelewa,maoni yangu kwakuwa una mambo mazuri kimaisha sasa nashauri jitahidi kuitafuta familia yake hasa watoto wake kisha angalia changamoto zao tangu kuondoka kwa baba yao kisha toa mchango wako kama shukurani ya kumuenzi tena ikiwezekana mpaka nao wafanikiwe hasa kielimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…