SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png

Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png

Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png

Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 
Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Ndio maana mi sisaidiii watu... Tukisaidia tu hatudumu.

Mkuu usiache kusaidia watu, kama umejaaliwa kwa namna yoyote usisite kufanya hivo. Kusaidia mtumwenye uhitaji ni sadaka bora zaidi kuliko hata ile unayotoa kanisani akala mchungaji
 
Najuta kusoma hii! Nimepata huzuni sana asubuhi asubuhi! RIP man of God.

Binadamu tubadilike, tufanye mambo mazuri, fanya jambo zuri hata kwa mtu mmoja tu.. Si lazima financially, Morally or emotionally inatosha, utakua umeacha alama katika maisha ya stranger na hakika utabarikiwa wewe na uzao wako.

Hakika kuna wakati ntu hauhitaji msaada wa kifedha, bali hata ushauri na kuonyeshwa njia pita hapa na pale na kutiwa moyo. Hakika Ip mob atabarikiwa uzao wake
 
Mkuu Morismoris kutokana na vile ulivyomuelewa mtoa mada uko sahihi sana kumkosoa ila ndugu nami nakukosoa pia , mtoa mada kaeleza kuwa alipokea taarifa za msiba muda toka mwezi wa tatu

Ila amekuwa kimya ila leo kaamua kuutambua mchango wa rafikiye kiasi cha kuamua kushare na jamii forum maana ndiko walikokutana lakini pia nikujulishe kuwa si kila mtu anajua uwepo wa shindano la stories of change hivyo ndugu yetu mtoa mada kaposti habari hizo ili tujifunze wema na ubinadamu ya kuwa bado kuna watu wanaumiliki

Ila pasipo kujua ya kuwa hivi sasa katika stories of change kuna shindano .

Hivyo msamehe tu ila yuko sahihi ila wewe utakuwa haujamuelewa vizuri ndugu

[emoji120][emoji120]
 
Pole sana mkuu,lakini unaweza kufaidisha matunda yako kwa wanae kama hakubahatika mtoto jaribu kuwatafuta wazazi wake uwasaidie shida zao.

Asante mkuu umetoa wazo zuri sana, nilikua nimefikiria jambo hili, nataka niweke mambo yangu vizuri then nitafute familia (kama ana mke au watoto) au wazazi nikatoe chochote kitu au msaada wangu kulingana na situation nitakayowakuta nayo.

Maadam kuna member mmoja anamfahamu, its a good start
 
Niombe radhii jamani [emoji120] lakini jukwaa hili linahusu shindano na ninaruhusiwa kumtingisha mshiriki yoyote atakaye post mada humu kwa muujibu wa muongozo wa shindano kwahiyo mimi niombe radhi jamani mnisamehe sana. !!!
Usijali ni sehemu katika mashindano na ni haki yako kuhoji .
 
Iache inaweza kuwa bahati yako,hizo hela ukawachangia jamaa zake marehemu.

Asante kwa mawazo haya mkuu, umenipa idea nyingine nzuri hapa.

Maadam iko kwny jukwaa la mashindano (nimesoma terms na conditions sidhani kama nime qualify, kuna vigezo wameweka pale, mimi niliandika bila kujua kuna shindano hence kuna vigezo nahisi sijatimiza)

Ila kama ikitokea ikishinda, na Nitaomba JF hio pesa iende kwa familia (mke/watoto) kama hana mke na watoto basi kwa familia yake.

Na tutafanya mchakato hapa kwa uwazi kabisa tukishirikiana na JF wenyewe.

Asante sana mkuu umenioa idea hii nzuri
 
Asante mkuu umetoa wazo zuri sana, nilikua nimefikiria jambo hili, nataka niweke mambo yangu vizuri then nitafute familia (kama ana mke au watoto) au wazazi nikatoe chochote kitu au msaada wangu kulingana na situation nitakayowakuta nayo.

Maadam kuna member mmoja anamfahamu, its a good start
Fanya hivyo mkuu na Mungu atakubariki zaidi.
 
Mkuu ulifanya juhudi zozote at least kutoa rambi rambi kwa familia

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

Nakiri nimekosa katika hili, nimeongelea pia pale juu. Na pia nilikua katika mapito fulani ambayo yalinitoa nje ya reli. But now am good

Ingawa haiwez badilisha the fact kwamba nmemkosea sana jamaa. But, Binadam tunakosea, na kuna wakati tukikaa tuna realize the mistakes ambazo tunafanya, na tunachukua hatua. Nimeongelea kwa post zilizopita nafanya process nionane na familia (mke/watoto) au wazazi nikatoe chochote kitu.
 
Mkuu Morismoris kutokana na vile ulivyomuelewa mtoa mada uko sahihi sana kumkosoa ila ndugu nami nakukosoa pia , mtoa mada kaeleza kuwa alipokea taarifa za msiba muda toka mwezi wa tatu

Ila amekuwa kimya ila leo kaamua kuutambua mchango wa rafikiye kiasi cha kuamua kushare na jamii forum maana ndiko walikokutana lakini pia nikujulishe kuwa si kila mtu anajua uwepo wa shindano la stories of change hivyo ndugu yetu mtoa mada kaposti habari hizo ili tujifunze wema na ubinadamu ya kuwa bado kuna watu wanaumiliki

Ila pasipo kujua ya kuwa hivi sasa katika stories of change kuna shindano .

Hivyo msamehe tu ila yuko sahihi ila wewe utakuwa haujamuelewa vizuri ndugu

[emoji120][emoji120]

Nashukuru mkuu wa kufanya clarification. Barikiwa sana
 
Pole sana mkuu. Mimi pia kupitia JF nilipata msaada mkubwa sana wa fundi wa magari toka kwa member mshana jr. Sikuwa namjua kwa kuonana naye . JF ni msaada ukiitumia vzr.
 
Shukran mkuu, hongera sana pia, JF ni kisiwa cha maarifa, kuna watu wema humu na watu wenye msaada wa kila aina.

Mtu akiwa serious kutafuta maarifa na msaada, hakika hawezi kukosa humu JF
 
Nashukuru kwa mchango wako mkuu, mimi sina interest na shindano lolote, sikujua kama kuna shindano humu mpaka member mmoja alivo nishambulia ikabidi nifuatilie vizuri jukwaa hili, mimi niliingia nikapost tu bila kujua nikachagua jukwaa nikaandika. Nakiri kukosea katika hili

Nimeomba mods katika posts za nyuma wahamishe uzi huu kwenda majukwaa mengine. Again sina interest yoyote na mashindano ya hili jukwaa
Sawa mkuu binafsi nakushukuru Sana Kwa hekima uliyotumia ktk kuliendea hili Jambo......mambo mengine ni ya kibinadamu Tu hakuna aliye kamilika.

Na hongera Sana Kwa kupambana na kutimiza ndoto zako......kuna kitu umetufundisha hapa Jf kwamba Katu tusirudi nyuma wala kukata tamaa ktk kutimiza malengo yetu.

Na tunakushukuru vile vile kushare nasi jitihada alizo zifanya marehemu ktk kusaidia kufanikiwa kwako....naamini kwako binafsi itaponya walau kidogo majeraha ya kuondokewa na jemedari aliyekuwa mstari WA mbele kuhakikisha unafanikiwa......na ni hamasa kwetu pia kusaidiana Kwa moyo wote Bila kujali tunafahamiana au hatufahamiani maadamu wote ni binadamu.
 
Naomba unisamehe nimewakosea sana 🙏
Kwanza umesamehewa Kwa moyo mkunjufu kabisa na inahitaji courage kubwa kuomba msamaha na hongera Sana Kwa Hilo.

Binafsi nakuona ulikuwa na hoja muhimu ya kusema lkn bahati mbaya hukuiwakilisha vizuri,ulitumia jazba na hasira kitu ambacho kilikufanya upoteze lengo la hoja yako....Mimi nilikuwa na hoja kama yako na bahati nzuri hata mhusika mwenyewe amekiri kuwa hakujua kama kuna shindano na ameomba Uzi wake utolewe ktk shindano.

Wakati mwingine jitahidi kutumia Busara katika kuwakilisha hoja zako....kuwa na Amani kabisa mkuu.
 
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
View attachment 2324415

Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
View attachment 2324417

Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
View attachment 2324421

Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
View attachment 2324422
Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
View attachment 2324430
Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
Inauma sana pale unapotaka kumuonyesha mtu matunda ya msaada wake kwako halafu hayupo tena [emoji24][emoji24][emoji24], inatokea mara nyingi, RIP ip_mob, tupo na hizi ID za kuficha hata mmoja wetu akiondoka inakuwa ngumu kujua siajabu unaweza hudhuria hata mazishi yake na bado usijue kwamba ni member mwenzako

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom