SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png

Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png

Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png

Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 
Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Ajaliwe pumziko la milele, watu kama hawa huja kwa makusudio maalau na athari chanya wanazo ziacha kwenye jamii ni kubwa sana, letu ni kumuombea Rehema kwa Mungu amjalie nuru ya milele.
 
Oh nashukuru mkuu sikujua kama kuna shindano. Kwa uelewa wangu nilivoona jukwaa la story of change nikadhani ni jukwa la habari za watu zilizofanya mabadiliko katika maisha yako

Mods nawaomba kama mnapitia uzi huu muihamishe hii mada kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko au jukwaa linalofaa na hii habari

Asante

Pole sana mkuu nimekuelewa vizuri na kiukweli kitendo cha kutambua mchango wa member ambae ametangulia mbele ya haki na alikushauri vyema kuhusu mustakabari wako wa kitaaluma na matamanio yako ya kimaisha ( kufanya kazi kwenye international organizations) ni jambo jema na la busara mno maana limetusaidia wengineo kujua kumbe pamoja na yote lkn Dunia bado ina watu wema

Kuhusu member anae kupinga na kuonyesha umeleta hii mada kwa minajiri ya mashindano yaliyopo naona kabisa anakosea na hasa akisoma vzr ulivyoleta maelezo yako na ushahidi wako wa maelezo unayompa tena kwa utaratibu , tafadhali muache tu huyo na akili yake ya mashindano na kuona vitu kwa uhasi
 
Ajaliwe pumziko la milele, watu kama hawa huja kwa makusudio maalau na athari chanya wanazo ziacha kwenye jamii ni kubwa sana, letu ni kumuombea Rehema kwa Mungu amjalie nuru ya milele.

Kabisa wanaacha alama katika maisha yetu na kutufundisha nasi pia kusaidia wengine. Amina
 
Pole sana mkuu nimekuelewa vizuri na kiukweli kitendo cha kutambua mchango wa member ambae ametangulia mbele ya haki na alikushauri vyema kuhusu mustakabari wako wa kitaaluma na matamanio yako ya kimaisha ( kufanya kazi kwenye international organizations) ni jambo jema na la busara mno maana limetusaidia wengineo kujua kumbe pamoja na yote lkn Dunia bado ina watu wema

Kuhusu member anae kupinga na kuonyesha umeleta hii mada kwa minajiri ya mashindano yaliyopo naona kabisa anakosea na hasa akisoma vzr ulivyoleta maelezo yako na ushahidi wako wa maelezo unayompa tena kwa utaratibu , tafadhali muache tu huyo na akili yake ya mashindano na kuona vitu kwa uhasi

Nashukuru sana mkuu kwa uelewa wako mpana na kulitazama jambo hili katika upande chanya. Barikiwa sana
 
Nashangaa huyu member ambaye anamshambulia mwanzisha uzi...

So kama kapost kwenye stori of change shida yako ni nini?kuna kitu kapotosha?ukiona haifai just "ignore" tu.
Pita vile usichanganye watu...
Uzi huu una mafunzo mengi sana...

Sema mkuu na wewe umezingua, ip mob yeye ndio anakutafuta kila mara,badilika.

Hizi sifa alitakiwa azipate akiwa hai.
 
Kwanza tunajivunia Kwa marehemu ip_mob Kwa mchango mkubwa alio utoa Kwa member mwenzetu na iwe chachu Kwa wengine wote ambao Kwa namna moja au nyingine ambao mko ktk position za kutoa connection au msaada ambao unaoweza hitajika Kwa member wenzenu.

Nakubaliana na hoja ya Morismoris .....hii post itakuwa sio fair ikiwa sehemu ya shindano kwasababu itavuta hisia za wengi kutokana na tukio lenyewe na watu kuvutwa kihisa ktk tukio zima....Mimi Etugrul Bey sipo sehemu ya shindano mseme kuwa labda Nina defend my interest lkn ktk akili ya kawaida....washiriki wengine hawata tendewa haki.

Naamini watayarishaji wa hili shindano kama itawapendeza mtumie Busara ktk kutafuta namna ya kufanya ushindani uwe wa haki.

Shukrani.
 
Naomba unisamehe nimewakosea sana 🙏
 
Nashangaa huyu member ambaye anamshambulia mwanzisha uzi...

So kama kapost kwenye stori of change shida yako ni nini?kuna kitu kapotosha?ukiona haifai just "ignore" tu.
Pita vile usichanganye watu...
Uzi huu una mafunzo mengi sana...

Sema mkuu na wewe umezingua, ip mob yeye ndio anakutafuta kila mara,badilika.

Hizi sifa alitakiwa azipate akiwa hai.

Nashukuru mkuu, ninakiri kuwa nina hatia katika hili, nina huu udhaifu hasa katika communication na watu, kutokana na experience nilyopitia utotoni (ila hii haiwezi kuwa justification ya kosa nlililofanya) … naahidi kujirekebisha kuanzia sasa
 
Nashangaa huyu member ambaye anamshambulia mwanzisha uzi...

So kama kapost kwenye stori of change shida yako ni nini?kuna kitu kapotosha?ukiona haifai just "ignore" tu.
Pita vile usichanganye watu...
Uzi huu una mafunzo mengi sana...

Sema mkuu na wewe umezingua, ip mob yeye ndio anakutafuta kila mara,badilika.

Hizi sifa alitakiwa azipate akiwa hai.
Braza naomba unisamehe nimekosa 🙏
 
Kwanza tunajivunia Kwa marehemu ip_mob Kwa mchango mkubwa alio utoa Kwa member mwenzetu na iwe chachu Kwa wengine wote ambao Kwa namna moja au nyingine ambao mko ktk position za kutoa connection au msaada ambao unaoweza hitajika Kwa member wenzenu.

Nakubaliana na hoja ya Morismoris .....hii post itakuwa sio fair ikiwa sehemu ya shindano kwasababu itavuta hisia za wengi kutokana na tukio lenyewe na watu kuvutwa kihisa ktk tukio zima....Mimi Etugrul Bey sipo sehemu ya shindano mseme kuwa labda Nina defend my interest lkn ktk akili ya kawaida....washiriki wengine hawata tendewa haki.

Naamini watayarishaji wa hili shindano kama itawapendeza mtumie Busara ktk kutafuta namna ya kufanya ushindani uwe wa haki.

Shukrani.

Nashukuru kwa mchango wako mkuu, mimi sina interest na shindano lolote, sikujua kama kuna shindano humu mpaka member mmoja alivo nishambulia ikabidi nifuatilie vizuri jukwaa hili, mimi niliingia nikapost tu bila kujua nikachagua jukwaa nikaandika. Nakiri kukosea katika hili

Nimeomba mods katika posts za nyuma wahamishe uzi huu kwenda majukwaa mengine. Again sina interest yoyote na mashindano ya hili jukwaa
 
Pole sana mkuu nimekuelewa vizuri na kiukweli kitendo cha kutambua mchango wa member ambae ametangulia mbele ya haki na alikushauri vyema kuhusu mustakabari wako wa kitaaluma na matamanio yako ya kimaisha ( kufanya kazi kwenye international organizations) ni jambo jema na la busara mno maana limetusaidia wengineo kujua kumbe pamoja na yote lkn Dunia bado ina watu wema

Kuhusu member anae kupinga na kuonyesha umeleta hii mada kwa minajiri ya mashindano yaliyopo naona kabisa anakosea na hasa akisoma vzr ulivyoleta maelezo yako na ushahidi wako wa maelezo unayompa tena kwa utaratibu , tafadhali muache tu huyo na akili yake ya mashindano na kuona vitu kwa uhasi
Braza unisamehe sana 🙏
 
Asante kwa kuni samehe maana mimi nilichukulia chapisho lako kama miongoni mwa washiriki wa shindano kwahiyo mimi nilitaka kukutikisa kama muongozo wa shindano linavyo jieleza kwahiyo nisamehe[emoji120]

Wala usijali, ni mambo ya kawaida. Peace[emoji3577][emoji3577]
 
Pole mwambaa, soo sad

ila malipo ni hapa hapa duniani , hukumu kwa Mwenyezi Mungu...IP...mob rest in peace, , tutafuata mazuri yako
 
Back
Top Bottom