SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png


Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png


Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png


Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 

Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Nakumbuka kuna Sister flani alimtumia Bro flani CV sasa imepita kama miezi kadhaa akazidi kumtumia email bila kujua alishafarikii..Siku hiyo ikawa kumbukumbu yake nikampost aaha yule manzi hakuaminiik yani kama jamaa alifariki kweli alimtegemea sana kwa connection. Mungu atupe mwisho mwema

Taarifa za kifo huwa zinaumiza sana hasa ukiwa mtu bado unamhitaji.. RIP
 
Naomba nisibishane nawe, mimi nitafute trending nifaidike nini… trending ya JF ina faida gani?

Na nimedanganya nini? Angalia tarehe ya hizo chats kwnye screenshot, fuatilia na uzi ule wa 2019 utaona ip mob ema comment pale, na taarifa za kifo mdau ame comment pale kwny uzi hivi karibuni

Na unasema Wajumbe wa shindano gani? Mbona sikuelewi.

Na kuhoji unaruhusiwa sijakukataZa
Samahani, Kwani ujui kwamba kunashindano ?
 
Asante kwa kuniruhusu tuweke mjadara.

Sasa Kwani ujui kwamba hapa tupo kwenye shindano ?

Kama jibu likija ndiyo tupo kwenye shindano kwa uelewa wako unaona ni sahihi kushiriki kwa kutumia visingizio vya andiko la msiba wa rafiki yako ? Je, ni sahihi kufanya hivyo ?


Naomba nisibishane nawe, mimi nitafute trending nifaidike nini… trending ya JF ina faida gani?

Na nimedanganya nini? Angalia tarehe ya hizo chats kwnye screenshot, fuatilia na uzi ule wa 2019 utaona ip mob ema comment pale, na taarifa za kifo mdau ame comment pale kwny uzi hivi karibuni

Na unasema Wajumbe wa shindano gani? Mbona sikuelewi.

Na kuhoji unaruhusiwa sijakukataZa

Kabla ya kukurupuka kutoa false accusations ni vema ukaupitia uzi ule wa 2019 utaona ip mob kanielekeza vitu vingi sana mule, na katika uzi huo huo angalia comments za 2022 utaona taarifa za mdau ananipa kuhusu kifo cha jamaa

Then kuja kwny screenshot nmepost za DM yangu na ip mob, angalia tarehe tumeanza kuwasiliana 2019 mpaka 2021 akapotea

Naomba usinikwaze ndugu yangu, sipendi kukwazana na watu
 
Braza naomba kuuliza hivi ni sahihi kutumia andiko la msiba wa rafiki yako kipenzi kama kitega uchumi kwenye shindano ?

Mkuu unakua hauko consistent, umenihukumu kuwa mimi ni muongo, nmekupa evidence unasema nimeweka kitega uchumi.

Why do you see negativity in everything?
 
Kwahiyo wewe ni rafiki au mnafki

Naomba soma tena uzi wangu, jamaa hatujawah kufahamiana simjui hata sura yake, na sijawahi kuwasiliana nae nje ya JF, alipofariki mimi ningejuaje?

Nimepata taarifa mwezi wa 3 na mdau anaemfahamu hapo kama ilivyo kwenye uzi nimekuweke evidence

Kama jamaa asingenipa taarifa nisingejua kama ametangulia

Mimi nakumbuka wema wake ndio maana nime acknowledge hapa, sasa kuniita mnafiki unanikosea sana mkuu
 
Back
Top Bottom