SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

SoC02 R.I.P ip_mob, JF member aliyebadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za leo wakuu.

Siku ya leo nimeguswa sana kutambua mchango wa member mwenzetu ip_mob aliyetangulia mbele za haki. Ame play part kubwa sana katika mafanikio yangu, kwa bahati mbaya ametangulia hata kabla hajasuhudia matunda ya mchango wake kwangu.

Kama mnakumbuka around mwaka 2018 na 2019 niliandika nyuzi kadhaa humu ndani kuhusiana na Master’s degree in Public Health (MPH)

Lengo la kuandika uzi ule ni kwa sababu nilikua na stress sana, kipindi naenda kusoma nilikua na malengo ya kufanya kazi kwenye international organizations. Kipindi niko naendelea na masomo watu walianza kunivunja moyo, nikakata tamaa na ndipo nikaamua kufungua uzi humu ili nipate uhakika.

Nakumbuka kuna watu walinikejeli kwenye uzi huo, na kuna baadhi ya watu walinitia moyo, kipekee zaidi ip_mob alinifuata inbox, akaniambia yeye pia ni alumni wa Muhimbili University kwa kozi ya MPH, kwamba anafanya kazi UN. Nilifurahi sana, tukaongea mengi sana kuhusu MUHAS na ma professor watata akina Kazaura Dr. Simba etc. ip_mob akawa ananielekeza mambo mengi sana kuhusiana na kozi yangu. Hapa chini baada ya ku defend proposal alinitafuta INBOX kuulizia nimefikia wapi
4C18755E-056A-462E-AD84-EC73A68065DA.png

Baada ya hapo aliendelea kunitafuta DM, na kila mara akinielekeza mambo mbalimbali, akinitia moyo na kunifundisha. Wakati wa ku defend dissertation yangu pia alinitafuta, akaniambia namna panel inavyokua na kunielekeza mambo mengi (see the attachment below)
05F4BCFD-6FC9-4CCC-94F0-44BD62ACED69.png

Nika defend dissertation yangu vizuri sana na walinisifia nikapata A, nilifurahi sana, nikampa taarifa ip_mob. He was so proud of me. Zikakaribia siku za graduation akanitafuta kuniuliza kama nina graduate pia (see the attachment below). Nikampa taarifa nime graduate tayari lakini pia nilikua mwanafunzi bora kwa mwaka 2019 Muhimbili University
887AD3AD-9FBB-4FDF-9E25-01728EC14C73.png

Baada ya ku graduate nikarudi mtaani tena, ramani hazisomeki nilikua najitolea kufundisha chuo huku njombe. ip_mob alikua akinitafuta mara kwa mara kujua naendeleaje akinitia moyo na kuniambia iko siku na mimi nitafika level kama yeye kufanyia UN (see the attachment)
078015BF-8F64-4692-A365-F9B1932F4E11.png

Lakini pia hakusita kunisaidia katika kunipa connection za kazi, mara kwa mara alikua akini direct sehemu za kuomba kazi, tulipambana sana pamoja, then ghafla nikaona kimya kingi, kila nikimtafuta hajibu.
1EA4A70B-AFFC-466D-B7B4-FFAABD15A11C.png

Basi nikajua labda yuko busy au kaamua kukata mawasiliano maana tulikua ni strangers tu, sijawahi kumjua kwa sura. Nikaendelea na mapambano na sikukata tamaa kila nikikumbuka mawazo yake na namna alivofika UN nilikua motivated sana. Nakumbuka nilimuahidi kuwa siku moja atakuja kushuhudia kwa macho yake when i make it na alinijibu short tu YES YOU CAN DO IT, SEE YOU AT THE TOP

Miaka ikapita Mungu akanibariki nikapata kazi kwenye shirika moja la kimataifa, pia nafundisha part time kama assistant lecturer na pia nimefungua research and consultancy office. Kiufupi maisha yanaenda vizuri nimejenga nina usafiri etc. Nilimtafuta ip_mob bila mafanikio.

Siku moja member mmoja Gallius ali comment kwenye uzi wangu, kwamba ip_mob alifariki kwa ugonjwa wa moyo (ni rafiki yake). Dah niliumia sana, siku ile hata usingizi sikupata, Why ip_mob why?? Nilitamani sana siku aone matunda ya mchango wake kwangu, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI NIMEPAMBANA KUWA KAMA YEYE, I WANTED TO SHOW HIM NAMNA GANI MBEGU AKIYOPANDA IMECHIPUA NA KUZAA MATUNDA. But ip_mob ulitangulia hata kabla hujaona matunda yako, naumia sana kwa ajili yako brother.

Nimejikaza kwa muda mrefu sana ila sasa nimeshindwa kaka, nimeona ni vema jamii forum ingekua mchango wako kaka, ili hata watu wengine humu waelewe kuwa good people like you still exist, watu ambao anamsaidia stranger bila malipo yoyote.

Kaka pumzika kwa amani, nimeandika uzi huu nikitokwa na machozi, kaka umeniumiza mno.

R.I.P ip_mob
 
Attachments

  • 63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    63468957-97D4-4743-8FB8-C5F04CDCE4FB.png
    596.2 KB · Views: 84
Upvote 102
Naomba soma tena uzi wangu, jamaa hatujawah kufahamiana simjui hata sura yake, na sijawahi kuwasiliana nae nje ya JF, alipofariki mimi ningejuaje?

Nimepata taarifa mwezi wa 3 na mdau anaemfahamu hapo kama ilivyo kwenye uzi nimekuweke evidence

Kama jamaa asingenipa taarifa nisingejua kama ametangulia

Mimi nakumbuka wema wake ndio maana nime acknowledge hapa, sasa kuniita mnafiki unanikosea sana mkuu
Taarifa ya msiba umepata mwezi wa 3 alafu msiba wa rafiki yako unakuja kutangaza mwezi wa 8 ? Are you serious ,,,,,,!!!!!

Ndiyo maana nime kuuliza wewe ni rafiki au unafki tu aiwezekani tangu mwezi wa 3 wewe uje kutengeneza mahudhui mwezi wa 8 alafu kwenye shindano ni wazi kwamba wewe ni mnafki.
 
Mimi sijaja kutangaza msiba hapa, mimi nina acknowledge contribution yake katika maisha yangu. Nimekuja hapa baada ya kufanikiwa na kumkumbuka mtu aliyechangia katika mafanikio hayo.

Hayo mambo ya mashindano unayajua wewe
 
Hebu ingia kwenye home page ya stories of change alafu uje uniambie kwamba nili siyo shindano unajua wewe kijana wa hovyo sana bado unadhihirisha wewe ni mnafki inamaana ujui kuna shindano kwenye nili jukwaa ?
 
Mimi sijaja kutangaza msiba hapa, mimi nina acknowledge contribution yake katika maisha yangu. Nimekuja hapa baada ya kufanikiwa na kumkumbuka mtu aliyechangia katika mafanikio hayo.

Hayo mambo ya mashindano unayajua wewe
Samahani kwa kuingilia mjadala wenu. Uzi wako umeuposti kwenye jukwaa la stories of change ambapo kwa sasa kuna shindano . Makala zitakazo shinda kuna uwezekano wa kujipatia kitita.
 
Samahani kwa kuingilia mjadala wenu. Uzi wako umeuposti kwenye jukwaa la stories of change ambapo kwa sasa kuna shindano . Makala zitakazo shinda kuna uwezekano wa kujipatia kitita.

Oh nashukuru mkuu sikujua kama kuna shindano. Kwa uelewa wangu nilivoona jukwaa la story of change nikadhani ni jukwa la habari za watu zilizofanya mabadiliko katika maisha yako

Mods nawaomba kama mnapitia uzi huu muihamishe hii mada kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko au jukwaa linalofaa na hii habari

Asante
 
Mpaka sasa una votes 20, Unaweza ukaiacha pia. Maana makala yako ni inspirational
 
Nashukuru sana mkuu wacha nikae kimya sasa
Niki kiangalia ID yako wewe ni JF expert siwezi kusema labda umekosea hadi ukapost kwenye jukwa la shindano la uandishi ingali wewe ushafanikiwa kimaisha alafu unanimbia taarifa za msiba umepata mwezi wa 3 alafu unakuja kutupostia mwezi wa 8 acha kiki mimi ninaposikia msiba hua naheshimu sana ila wewe ulicho Fanya ni unafki kwahiyo napinga kwa sababu tupo kwenye challenge hapa.

Kijana acha ushamba mambo ya misiba na mashindano wapi na wapi mfano mimi baba yangu alifariki mwaka Jana na amenisaida kunisomesha vipi nikileta maudhui hapa kwenye shindano ya misiba nitakuwa na akili timamu kweli ?
 
Naomba soma tena uzi wangu, jamaa hatujawah kufahamiana simjui hata sura yake, na sijawahi kuwasiliana nae nje ya JF, alipofariki mimi ningejuaje?

Nimepata taarifa mwezi wa 3 na mdau anaemfahamu hapo kama ilivyo kwenye uzi nimekuweke evidence

Kama jamaa asingenipa taarifa nisingejua kama ametangulia

Mimi nakumbuka wema wake ndio maana nime acknowledge hapa, sasa kuniita mnafiki unanikosea sana mkuu
Hii ni JF acha kubishana na huyu mtu atakuharibia siku. RIP MWANAJF
 
Mpaka sasa una votes 20, Unaweza ukaiacha pia. Maana makala yako ni inspirational
Huyu yupo humu tangu 2018 alafu anasema hajui kama kuna shindano inamaana alivyoingia home page ya stories of change hajaona kuna nini ? Kwa member ambaye yupo tangu 2018 ?
 
Back
Top Bottom