Rachel dangwa ilibidi akamatwe Mapema sana maana alikua anatumia matusi ya nguoni

Rachel dangwa ilibidi akamatwe Mapema sana maana alikua anatumia matusi ya nguoni

Habari

Hatukatai kwamba kwa sasa serikali inafanya mambo mengi ambayo wananchi hawayafurahii na kiwango cha uungwaji mkono ni kidogo sana kulingana na aina ya utawala uliopo

Matukio mengi yanayoripotiwa kama ukosefu wa uwajibikaji ,vitendo vya rush wa, utekaji ,mauaji ya raia wasiokua na hatia pamoja na kutoheshimika kwa raia hasa wa ngazi ya chini ni vielelezo tosha kufanya watu wasipendezwe na utawala uliopo

Lakini utawala uliopo hata kama sio wa haki lakini upo kisheria na serikali ikishaundwa inatakiwa kuiheshimu na kufanya nayo kazi nzuri ya kuilinda na kuisadia kuleta maendeleo yanayohitajika.

Kupinga au kutetea haki ni jambo zuri lakini lazima utumie Postive constructive crtisizim katika kuonesha madhaifu na kuishauri serikali namna nzuri ya kufanya ili kuleta maendeleo au kujenga nchi pamoja.

Harakati alizokua anafanya mwanadada Rachel ni za kishamba maana alikua anatumia lugha za matusi ya nguoni ,anazungumza bila kuwa na facts ,anatweza na kudhalilisha Viongozi jambo ambalo sio zuri hata kidogo.

Endapo atakua amekamatwa itatakiwa iwe funzo kwa wengine kufanya harakati za kistaarabu huku tukiheshimu utu na hadhi za wenzetu na kufanya ukosoaji wenye faida na wenye lengo la kujenga nchi moja yenye upendo amani na maendeleo.
Binafsi siungi mkono lugha ya matusi na udhalilishaji kwenye ukosoaji wa viongozi wa chama na serikali; lakini bado kibongo bongo hata utumie positive constructive criticism, bado utashughulikiwa tu. Jambo ambalo linaonesha kuna tatizo mahali.

Ifikie wakati watawala wakubali mawazo mbadala.
 
Back
Top Bottom