Masanja
JF-Expert Member
- Aug 1, 2007
- 5,319
- 10,416
Ndio kabisa nasikia hizi hotel wazawa wanalipwa laki na nusu au laki mbili halaf wageni wanalipwa pesa ndefu kweli hapo namuunga mkono
Normally local salaries zinalipwa kulingana na prevailing Market rates. Mfano, UN kigezo kikubwa wanachokitumia kulipa local staff ni best available local markets. kwa vile UN ni shirika la Umoja wa Mataifa (international staff wanalipwa kulingana na mishahara ya nchi mwanachama anayelipa vizuri watumishi wake serikalini). Mpaka leo nchi hiyo ni Marekani! Ndo maana mpaka leo mishahara ya International staff wa UN iko based kwenye salary scale za mishahara ya serikali ya USA (kwa national staff iko based kwa best locally prevailing rates)
Private sector/au makampuni binafsi ya kimataifa...... mara nyingi wanaangalia mishahara ya serikali (it is assumed-wrongly in my view) kwamba mishahara ya serikali ni kipimo kinachoakisi ubora wa maisha ya raia wake. Kwa hiyo akija Hyatt mfano ataangalia competitors wake wanawalipa vipi wafanyakazi wao (maana mishahara ya serikali ni midogo mno kufanya comparison). Sema sasa kwa sababu ya umasikini na availability of cheap labour..wanajua kabisa hata wakishusha..bado watu watafanya hizo kazi. Upande wa serikali ni ngumu kuingilia, maana huwezi uka-demand raia wako walipwe mishahara mikubwa ambayo hata wewe huwezi kuwalipa watumishi wako. At the end of the day ndo maana ni muhimu kufanya negotiation ya maslahi kabla ya kusaini mkataba.