Rafiki wa shule ya msingi akumbushia stori hii mbele ya mchumba wake

JaxenDL

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2022
Posts
221
Reaction score
495
Akiwa darasa la 5 katika moja ya shule ya msingi huko Arusha Republic John alikumbana na tukio kuingiliwa kinyume na maumbile kwa nguvu na wanafunzi wa darasa la 7 [wa kiume pia].

Baada ya kushtaki kwa mwalimu wa darasa kesi ilifika kwa mkuu wa shule, taratibu za uwajibishwaji zilifanyika kwa wahusika na kikao cha pamoja kuwaelemisha wanafunzi wote juu ya swala hilo.

Athari za kimtazamo na madhara ya saikolojia aliyopata John kwa mazingira yale ikawa ngumu kujumuika pamoja na wanafunzi na jamii , hivyo mjomba wake alimchukua kuishi nae Dar na kuendelea na masomo..

Miaka mingi sasa imepita John ni muajiriwa katika moja ya taasisi za serikali, alibahatika kukutana na rafiki yake wa utotoni Samson katika moja ya mitandao ya kijamii na kuweka appointment kwani walikua mkoa mmoja.

Jumapili tulivu John aliongozana na mchumba wake katika mgahawa ambapo anakwenda kukutana na rafikiye wa utotoni (walisoma wote shule ya msingi) na kumkuta tayari alishafika.

Baada ya salamu John alimtambulisha mchumba wake kwa rafikiye, waliagiza vyakula na kuendelea kupiga soga za kipindi cha nyuma.

Katikati soga Alice (mchumba wa John) aliuliza kwanini John alihama Arusha kwenda Dar kusoma ilhali familia yake ilibaki Arusha. Samson alimuelezea Alice tukio zima😂😂😂mbele ya John japo katika hali ya utani juu ya kile kilichomtokea John wakiwa darasa la 5

NINI KILITOKEA, HATUA GANI JOHN ALICHUKUA BAADA YA HAPO MIMI SIFAMU ila nilisikia Samson amelazwa hospitali baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani (kiti) na amevunjika baadhi ya mifupa ya mbavu
😂😂😂
 
Sio kila kitu nicha kuuliza au kusema kila wakati na kila mahali unaweza zua taharuki, majonzi na vilio bila kukusudia au kupenda.
 
Usimkaribishe nyumbani kwako ama mahala pa kazi rafiki uliyesoma naye utotoni.

Kwanini? Mbali na kisa cha mleta mada. Kuna jamaa alionana na rafiki aliesoma naye kitambo kidogo (miaka 8) akadai kaja kwa matembezi tu ktk mkoa wa rafiki yake.

Kwa kuwa walishibana sana huko nyuma akampeleka mpk nyumbani kwake.

Kumbe huyu mgeni kishabadilika amekuwa ni jambazi sugu linalotafutwa ndani na nje ya nchi.

Nisiwachoshe. Kilichofuata ni wote wawili kukamatwa na kuwekwa rumande. Huyu mwenyeji kuja kuthibitisha kuwa hawako chama kimoja akawa amesota ndani miezi 6 na ushee.
 
Daaa
 
Daaah mkuu hii hatari sana...
 
Back
Top Bottom