Rafiki yako anaweza kukutetea hata kama anajua wewe ndiye mkosaji?

Rafiki yako anaweza kukutetea hata kama anajua wewe ndiye mkosaji?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kuna baadhi ya marafiki wanateteana kwa kila kitu mpaka ujinga, akikuta rafiki yake ana msala atasimama kutetea hata kama anajua rafiki ndiye mkosa kisha atamlaumu baadaye tatizo likiisha.

Umewahi kupata rafiki kama huyo?
 
Ndio, nilishapata rafiki kama huyo lkn tulikuwa tunatetea kwenye issue za kazi yaani ofisin, ikitokea nimeharibu anasimama kunitetea kibarua kisiote nyasi.
 
Mbona hiyo ni kawaida sana Mkuu, rafiki hata akizingua una mchana tu white mwenyewe, ila msala wake mna usolve wote.
Ingawa hauwezi muunga mkono kwenye ujinga, lakini akishachuma janga, kikanuni kabisa mnalila wote.
Ila akizidi sasa, ina maana hamuendani, bora uachane nae tu
 
Kuna baadhi ya marafiki wanateteana kwa kila kitu mpaka ujinga, akikuta rafiki yake ana msala atasimama kutetea hata kama anajua rafiki ndiye mkosa kisha atamlaumu baadaye tatizo likiisha.

Umewahi kupata rafiki kama huyo?

Marafiki wa hivyo nimekuwa nao wengi TBH
Nyumbani kwetu alikuwepo dada(dada wa kazi) , yule dada alikuwa ananitetea kwa kila msala pale nyumbani

Nina bahati ya kutetewa mara nyingi kuliko kupigwa mawe
 
Mimi ndio nna tabia ya kuwakingia kifua marafiki zangu😂 kipindi nipo shule akionewa rafiki hata sijui chanzo nauvaa ugomvi halafu baadae ndio nikikaa naye namuuliza ilikuwaje🙆🏽‍♀️
 
Back
Top Bottom