Rafiki yangu alitaka Tufe, Dereva wa Lorry akakubaliana naye, Mungu akamtumia Dereva mwingine Kutuokoa

Haya msingejua kuwa chizi maarifa has passed away.
Ni kweli kabisa, mimi gari yangu haendeshi mtu tofauti na mimi. Licha ya safarini hata hapa mjini tu huwa sipendi mtu aendeshe sababu gari yangu dynamics zake nazijua mimi mwenyewe.

Hata wewe pia madhaifu yote na handling ya gari yako unaijua mwenyewe. Sasa umpe mtu mgeni ni lazima akae nalo kwa muda kidogo alizoee. We unampa mtu gari highway kweli ndio maana lilimshinda.
 
Kumekuchaaaa
Mana imenibidi kuangalia mwisho wa post.. kuna neno ntaendelea au la...
 
Nimefarijika sana kwa kumsaidia Richard kiasi kwa ajili ya matibabu ya Mama. Huu ndio ubinadamu tunaouhitaji.

Pengine kupona kwa mama wa mwenzetu ni kwa sababu yenu ambao kama asingekuwa ni ubinadamu katika nusura ile ya ajali leo msingekuwepo na mama yake pengine asingepona kwa sababu wasingepatikana watu wa kunusuru maisha yake kwa hicho kiasi kidogo ambacho leo huenda ndicho kinaokoa maisha ya Mama Richard.

Katika hatua zetu zote hapa duniani tujitahidi kuwa wema kwa wengine bila kujali malipo. Papo Mahali sahihi Mungu ataonesha malipo yake.

Lipo somo tumejifunza.
Barikiwa sana Chizi Maarifa
 
Sema gari haina madhaifu yoyote ndo maana sikuona shida. Ipo vizuri sana na imetembea kms chache sana 13,000+ toka imetengenezwa.
 
Sema gari haina madhaifu yoyote ndo maana sikuona shida. Ipo vizuri sana na imetembea kms chache sana 13,000+ toka imetengenezwa.
Sawa ila ukumbuke kila gari ina handling ya tofauti barabarani. Mtu kashazoea Handling ya Benz GLS uje umpe Harrier unaeza shangaa mko kwenye mashamba ya Mkonge chap ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Dah story iko touching mwishoni hapo, next time usihatarishe maisha yako hata kama ni best yako sana hawezi ni hawez barabara kubwa so sehem ya majaribio. Salute kwa Richard madereva wa magari makubwa baadhi yao wanajikutaga bara bara ndo yao kweli
 
since i lost my lovely cousin sitawahi enda road trip na dereva asiye mzoefu
 
Bora huyo wa manual,mi kuna mjinga mmoja gari auto kabisa ilikua mida ya sa mbili usiku tunaenda kyela namimi ilikua first time akasema njia anaijua apige mashine nikamwambia kama kuna road signs napiga mashine jamaa kang'ang'ania aendeshe eti kuna kona kibao... Nikamuachia gari sabab ni mwenyeji kumbe jamaa learner. Tumekutana na gari ikawa inatuwashia taa kuashiria tutoe full naona jamaa yangu hata haelewi nikamwambia toa full jamaa lilivyolijinga likazima taa kabisa afu gari iko mafuta..aisee tukajikuta nje ya barabara uzuri hakukua na korongo.
Nikamuuliza why akasema gari yangu iko tofauti nikajua huyu chenga kabisa

Ukiona mtu anaham sana ya kuendesha gari na anang'ang'ania ujue huyo learner na sio dereva
 
Sawa ila ukumbuke kila gari ina handling ya tofauti barabarani. Mtu kashazoea Handling ya Benz GLS uje umpe Harrier unaeza shangaa mko kwenye mashamba ya Mkonge chap ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
ndo mambo ya kuvunjana mabega haya๐Ÿ˜‚
 
Mi mara mia niendeshwe na dereva mlevi lakini mzoefu wa gari aina izo kuliko lena asie na uzoefu na anaeng'ang'ania gari,katika kuondoka tu manual nitamtizama kwa makini usharp wake wa process nikiona mpaka aangalie gia sijui nini hapo hapo namwambia ndugu kaa huku, yani manual kwa mzoefu ukiweka mkono ktk gear unajua ipo namba ngapi the way how hand joint flex
 
Pole kwa mkasa ambao hutokea mara nyingu kule mbugani barabarani.
Scenario uliyoelezea inatisha sana.
Kule mbugani si kwa ma learner na wakati mwingine ni umwamba, maana hakuna trafiki kila mahali.

Lakini katika uzoefu wangu, madereva wa malori kwa ujumla ni wastaarabu sana , isipokuwa wachache.
Kama unaendesha gari kwa kusita sita mbugani, hatari ni nyingi sana.
 
Angekumaliza tu,huwezi ukatuacha kule hujamaliza uzi alafu unakimbilia huku tena,ww mpuuzi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ