Rafiki yangu alitaka Tufe, Dereva wa Lorry akakubaliana naye, Mungu akamtumia Dereva mwingine Kutuokoa

Pana jamaa walikuwa na v8 wameovertake semitrela wamefika kwenye cabin mbele linakuja semi wangu wangu wakaingia kushoto mbele cabin ya semi wanayoovertake ile wameovertake semi A kuingia kushoto Ile kukwepa semi B ya inayokuja.Semi A ikawapush kwa nyuma semi B ikaja wakandamiza kwa mbele yaani walipigwa nyuma na mbele kwa semi zote mbili jamaa v8 awakuomba maji pale pale wote israel aliondoka nao,akawaacha madereva wa masemi.
Kumbe semi A angepunguza au kuminya brake angewaokoa.
 
Kuna dereva mwingine wa lori alivyoona gari limemshinda breki mwenzake wa nyuma mto Ruvu pale akaona ajititie na mibreki ili amtumbukize mwenzie mtoni na akafanikiwa.
lengo lake ilikuwa jamaa aje apige nyuma yake asimame, maana hakukuwa na ujanja wa kumkwepa au kuongeza speed amuache.

bahati mbaya mhanga(marehemu) hakumwelewa mwenzake akamkwepa,na kuingia mtoni.
 
Kuna mahali niliona ajali kama hii
 
Madereva wa matruck uwa wastaarabu lakini usiombe ukutane na madereva wa fuso na vicanter vya kubeba nyanya na vitungu wakitokea zao iringa na mbeya,jamaa kavu sana wale,mida ya usiku uwa wana mchezo wa kupiga full light gari ndogo
 
Usije wapa tena Marenad gari hasa katika masafwa marefu,mtageuka majina kwa mda mfupi tu.
 
Pple!! Ila hamna sehemu ulojibu kuhusu kutelekeza uzi wa kusaka utajiri! Acha uhuni we jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe tapeli ulieleta huu uzi hauaminiki unatabia ya kuiba story za wengine halafu unajidai za kwako.
 
Wewe tapeli ulieleta huu uzi hauaminiki unatabia ya kuiba story za wengine halafu unajidai za kwako.
Hahaaa huyu jamaa ni tapeli kiukweli hata huu uzi haumuhusu yeye.
 
Kwenye ndege, marubani wawili walibishana. Kijana na mzee. Yule kijana alibisha madai ya mzee kwamba anaweza kutua lidege lile huku akiwa amefumba macho.

"Kwa nini tuandikie wino na mate yapo?" Tutakapotua onyesha manjonjo yako!

We acha tu!

(Itaendelea 😉 )
 
[emoji3][emoji3]nakumbuka kipind najifunza gari muhuni/rafik wangu mmoja alikua anasukuma scania 113 gear 8 Jamaa alikua anapanga gia Kama Hana akili nzuri na vile vinanda vya injin ya scania mzee had unataman ule ugali mkavu alaf mboga iwe ile sauti, nikamwambia Jamaa niachie na mm nimsukume msweeden

Jamaa akaweka chuma pembeni akanikabidhi jiko kundoka nikaondoka frsh shida ikaanza pale nimemaliza gear 4 natakiwa nipandishe button nianze kupeleka Hadi 8 jasho lilinitoka ikawa naacha kuangalia mbele naangalia gear lever nikirudishaa macho mbele naona tu vi ist vikiingia kwenye mashamba ya mahindi ya watu huko maana nlikua nayumba njia nzima inabid wao ndo wanikwepe la sivyo wanaingia kwenye uvungu alaf nipo kibati laana, muhuni mwenyewe ali sanda akaniambia pangua gear weka chuma pembeni[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Duuh mkuu mimi nilishawahi kwenda kwa jamaa yangu na chuma ya manual ilikuwa mwaka jana tu hapa.
Yeye ana gari pia ila ni Auto na hawezi manual sasa akaniambia alisomea chuo cha driving na alikiwa anasukuma Manual akalazimisha akumbushie.

Asee nilikuwa nimeipaki karibu na ukuta wa getini kwa jamaa anapokaa halafu nilizimia kwenye gear ili isisogee mbele mana haikuwa na handbrake nzuri.

Basi bwana jamaa akakurupuka kuiwasha iko kwenye gear aliingia na ukuta ndani ikawa msala kwa baba mwenye nyumba iikabidi alipishwe na mimi gari iliumia japo si sana nilimkaushia tu.

Mtu kama hujawahi kumuona uendeshaji wake usimpe gari.
 
Kama naviona vile vi ist vikiingia mashambani [emoji23][emoji23] dadeq
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…