Rafiki yangu analazimisha akatumie kitambulisho changu kupata simu ya mkopo, hii haitaniletea shida?

Pelly

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
287
Reaction score
370
Habari zenu wana JFA,

Kuna rafiki yangu anajifanya mjanja mjanja kaniomba nikatumie kitambulisho changu kukopa simu kampuni fulani nimemkwepakwepa sana lakini naona ananishikia bango, leo kanipigia tena nimemwambia tukutane j5 posta mjini Dar es salaam.

Sasa naomba kuuliza kama atashindwa kulipa deni si litakuja kwangu? Msaada kwa wenye kujua janja wanayofanya wanaokopa simu au nimsaidie tu?
Asante
 
Atakayekua amekopa na anadaiwa simu hapo itakuwa ni wewe ndugu.
 
Hayo mamikopo, mdhamini anahusishwa moja kwa moja mkopaji anaporuka ahadi za marejesho.

Katika kesi hiyo, hakuna mahali unapoweza kukwepa kudhalilishwa.
 
Ukimuomba ushauri huyo rafiki yako anakushaurije?
 
Asante, nilikuwa nataka kujiridhisha maana nasikia sikuhizi ukikopa simu kuna wajanja wanafuta inakuwa haifungwi na deni sijui inakuaje
Kwa hiki ulichoandika inaonyesha alikuambia akakope Kwa kitambulisho chako then wajanja watafanya jambo ili deni lisifatiliwe, itoshe kusema ww nae hujitambui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…