Rafiki yangu analazimisha akatumie kitambulisho changu kupata simu ya mkopo, hii haitaniletea shida?

Ipo siku atakuja kuomba hati ya nyumba yako akakope benki, pia mpatie ili ukalale nje.
 
Huyo rafiki yako ni mpumbavu,simu ya laki mbili na 50 unalipia laki sita kwa mwaka
 
Haina shida lazima alipie deni. Maana asipolipia marejesho ya deni simu inafungwa mpaka alipie. Kama rafiki yako kweli unamuamini haina shida.
 
Kwa uzi huu na "hoja" hizi itoshe kusema wewe ni mjinga.
 
Huyo rafiki yako ni mpumbavu,simu ya laki mbili na 50 unalipia laki sita kwa mwaka
Yamekutana majinga. What kind of questions is she asking? Kitambulisho ndio utambulisho wako; kitambulisho chako kikitumika means ni wewe. Simple logic!
 
Haina shida kabisa , kuwa na amani, msaidie mwenzako
 
Yaani unajitafutia tabu,kataa
 
Huyo rafiki naye wa kukaa naye kwa tahadhari. Rafiki wa kweli hawezi omba msaada katika vitu kama hivyo. Bora hata angekuwa anaumwa, anahitaji hela ya matibabu kweli unaweza jitoa. Katika maisha usiogope kufanya maamuzi eti kwa sababu watakuonaje. Sema tu siwezi kukupa full stop. Unavyomdanganya unampa matumaini ya uongo kitu ambacho sio sawa.
 
Kwani unamwogopa,hata km hujasafiri unamwambia tuu hapana
 
Anataka akufunge, kataa kabisa akinuna futa na urafiki wenyewe
 
We acha yakukute ya Ferouz na Wema wangu umeniponza; ukamatwe wewe rafiki yako akisepa na hilo deni
 
JIFUNZE KUSEMA HAPANA, JAMBO LA KAWAIDA UNASHINDWAJE KUSEMA HAPANA? SEMA HAPANA, TUMIA KITAMBULISHO CHAKO.
 
Ukweli haina shida kabisa maana hicho kitambulisho siyo chake hawezi kupata tatizo lolote aise halafu kule alikokopa picha na kitambulisho si vyake sasa tatizo liko wapi? Halafu haya makampuni ya kukopesha simu ni wapumbavu tuu ndiyo maana watu hawalipi simu za mkopo maana wanaokopa hawana vitambulisho na wanatumia vya watu wengine.!
 
Rafiki yangu analazimisha akatumie kitambulisho changu kupata simu ya mkopo, hii haitaniletea shida?
Utajuta, maana deni litakuwa lako 100%
Wewe ndo utakuwa unakumbushwa kuwasilisha rejesho daily. Hiyo kero utaiweza?

Mwambie aombe kupewa kitambulisho chake, ni rahisi tu, hadi kuna madalali/mawakala wa kupata vitambulisho chap chap.
 
Watafute wataalamu wa Mirembe watakusaidia tatizo lako.
 
Huyu kaja kutuenjoy kujua tutasemaje Sasa umekutana na comments unhinged pole sana
 
Huyo siyo rafiki. Na kwa kumsaidia tu na wewe umlazimishe achukue kitambulisho chake kama hana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…