Saidama
JF-Expert Member
- Jun 10, 2022
- 598
- 1,151
Kuna rafiki yangu amekutwa au naweza kusema anasumbuliwa na jambo ambalo dalili zake zinaonyesha kua huenda akawa na jini mahaba ndani yake. Kwaio ameniombea kupitia jukwaa hili la ma great thinkers niweze kumuulizia jambo hili.
Dalili zenyewe ambazo kwa maelezo yake ameziona ni kama zinaendana na mtu mwenye jini mahaba ni pamoja na KUOTA AKIFANYA MAPENZI na kubwa zaidi KUPOTEZA HAMU YA KUFANYA MAPENZI katika maisha yake ya kawaida. Na hili la pili sasa ndo limepelekea hali kua ya wasiwasi mpaka kufikia kuniomba kuja kwenu wajuzi wa mambo kuulizia swala hili.
Jamaa stori yake huko nyuma ni kua amewai kua kwenye mahusiano na wanawake watatu nyakati tofauti tofauti, na wote sababu za kuachana nao ni kuwachoka na kutowahitaji tena muda mchache tu baada ya kukutana nao kimwili kwa mara mbili au tatu tu.
Nyakati hizo za nyuma alikua akihisi huenda alikua hajatokea kuwapenda ndomana pengine alikua akiwachoka haraka na kutowahitaji tena ila ni mpaka sasa ambapo yupo kwenye mahusiano na mwanamke mwingine ambae yeye anadai anampenda lakini katika hali ya ghafla amekua hana tena hamu ya kufanya nae mapenzi hata akiwa nae utupu chumbani, hali ambayo sio ya kawaida kabisa kwa sababu hana tatizo lolote la kiafya na ni mtu wa mazoezi.
Kwa dalili hizi moja kwa moja tumeona inawezekana ikawa huenda ana kitu tofauti kinachomsababishia hali hiyo. Na katika kujaribu kuuliza kwa mtu mmoja mwenye kufahamu mambo mengi kidogo, aliweka tiki pia kua dalili hizo zinakuaga ni za mtu mwenye jini mahaba.
Sasa lengo la uzi huu ni kutaka kufahamu zaidi kuhusu jini huyu mahaba, yani namna ya kumtoa na kuweza kujikinga nae wakati mwingine. NATANGULIZA SHUKRANI.