Rafiki yangu anasumbuliwa na jini mahaba. Je, ni namna gani ya kumtoa?

Nje ya mada kuu. Kipindi nabalehe na sina uwezo wa kukamata mademu nilikuwa naombea sana nopate huu ugonjwa wa kuwa na jini mahaba ila mikawa hata siyapati
Hauwezi kuyapata kwanza sio kitu cha kuombea na isije kuthubutu ya kukute ni hatari kubwa

Mara nyingi haya mambo huwa kuta watu wanaotokea ktk familia zenye mzizi wa mambo hayo wengi wa watu wanao patwa na hayo matatizo mababu na mabibi zao walikuwa na Hiyo asili
 
Kama jini huyo ana power kubwa na ni inborn character yako hauwezi kumuondoa Kwa style na anaweza kumuua
 
NIpe mawasiliano yake, anilink na huyo jini, binafsi nasumbuliwa na mahaba,tubadilishane uzoefu!
 
Mpeleke kwa ositazi amfanyie kisomo
 
Hakunaga vitu kama hivi sijui jini mahaba sijui popobawa. Ni story tu za vijiweni na mabarazani kupoteza muda na kusogeza siku watu wakishashiba kande na kuvimbiwa.

Msingi wa maisha ni kufanya kazi.
Mkuu kistaarabu iko hivi, hoja ama jambo lolote hukanushwa ama kubishaniwa kwa vielelezo vyenye mshiko.

Kuibuka tu na kusema: 'jambo hilo halipo' ni dalili za ubishi wa kiha.

Unakuta hata jambo lipo sahihi, ye'ababishana tu.

Kumbe nia ya ubishi huo lengo lake ni kutengeneza ligi ya kutafuta mshindi katika hoja inayoongelewa, yaani yeye mbishi hutafuta ubingwa kwa kubishana!

Mpaka leo hujiuliza, enhe ushindi anaoupata mbishi hulenga manufaa gani, maana hakuna mfadhili anayedhamini na kulipia ushindi wa ubishi huo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…