Tatizo liko kwa mtonyaji! Nia labda ilikuwa nzuri, lakini madhara yake yanaweza kuwa makubwa. Sasa huyo mtonyaji awe fair,akimuona mme wa huyo mke nae anachepuka amtonye!
Nakumbuka mwaka fulani, niliingia Shinyanga nikitokea Musoma! Nilivofika nilienda kutafuta sehemu ya kulala, kwa bahati mbaya au nzuri chumba nilichokuwa natizamana nacho kulikuwa na jamaa mmoja nafahamu, japo yeye alikuwa anifahamu! Alikuwa Mtumishi mpya katika hospital ya mission iliyopo kijijini kwetu!
Jioni, natoka kula, nikaona anaingia na mwanamke, ambaye ni mke wa ndugu yangu, ameaga anaenda Msibani kumbe ameenda shinyanga kula raha na mchepuko!
shemeji hakuwa ameniona, so kipindi anaingia ndani, huku ameshikwa kiuno, mi Uvumilivu ukanishinda! Nikaanza kumfikiria ndugu yangu, nikaanza kumfikiria anavyojigamba juu ya utulivu wa mke wake!
Basi ikabidi tu, nimwite Mama chitimbo, akshituka, nikamuita na yule jamaa kwa Jina, Dr. Chikelembwe, wakaduwaaaa!
Nikawaambia siyo sawa kabisa, shemeji mi namwambia ndugu yangu! Ooh shemeji ,hapana! Shemeji tafadhali! Nikamwambia njoo, tuzungumze, nikamhoji, akasema alivyodanganya, na blah blah nyingi! Nikamwambia hata Picha ninazo, akasema shemeji nisamehe, nipo radhi nikupe ila usniseme! Watoto wangu watateseka!
To cut the story short, nikamwambia yule jamaa, nitamlaza ndani maana, picha na ushahid ninao! Mwisho wa siku jamaa akaniomba msamaha. Akaamua na kuondoka, shemeji akalala Asubuhi akaondoka!
Hadi leo sijamwambia mme wake, wako na wanaendelea na maisha yao vizuri na mme wake! Lkn ningemtonya brother, wangelikuwa wameshatengana! Huwa naenda kuwatembelea, shemeji anafikir nitamsemea, sijui maana anakosa amani!
So wakt mwingine, utonyaji si deal! Maana we are all part of that stuff!
Sent using
Jamii Forums mobile app