Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Huyo jamaa kama yupo hapa JF habari zitakuwa zimemfikia. Mapenzi ni upofu wa kijinga sana.
 
Imekaa kama chai ya baridi ila inafikisha ujumbe na mafunzo.

By the way hivi inakuaje mtoto anateseka na hawezi kusema Kwa Baba?
.na wewe kama unataka kumsaidia si Bora ungetoa taarifa Kwa Mtendaji Ili afuatilie yeye kama Ofisi na sio wewe Kwa Ajili ya kuepusha mizozo ya majirani?

Mwisho wanaume wa hivyo wanakuaga wamerogwa Wala sio mapenzi
 
Mwanamke anaweza ua mtoto wake wa kumzaa Ili aolewe endapo atapewa sharti la mtoto aende kwa baba yake na Jamaa Mpya mwenye mkwanja na akahisi anampenda.

Mwanamke anaweza ua Watoto wake eti akifa wasipate shida nimewahi sikia haya maneno Kwa Mke wangu mwenyewe (shida zenyewe ndio hizo za mama wa kambo)

Mwanamke(Anaweza muinea wivu mtoto wake wa kike) kisa kaolewa pazuri

So inatakiwa kuishi na wanawake Kwa akili saaana na Kwa umaskini but ukiona haivumiliki Bora kuachana ila saidia Watoto huko huko mbali ,usione wanavyojilizaga ila walifikia mwisho Huwa wanakuwa wanyama.

Ndio maana binafsi mambo ya kusema eti napempenda mwanamke duu,kwangu ni magumu natimizaga wajibu ,sipendi mwanamke yeyote hapa Duniani na hayupo wa kunibabaisha hata ungekuwa mzuri kiasi gani,ukienda kinyume tuu na principle zangu ujue tunashindana.
 
Tuliopitia maisha ya mama wa kambo tunakuelewa...Wanaume sijui tunakwamaga wapi sijui ni madawa au mapenzi ya kupitiliza
Kiufupi ni kurogwa au ni wale wanaume wenye mioyo mwepesi wanaweza kujiliza Liza na kubabaishwa na muonekano wa mwanamke.
 
Pole sana, ila usijisikie vibaya kwani hamna kosa alilolifanya, kiufupi ni kuwa huyo homeboy wako kalogwa na mkongo kwahiyo hasikii haambiliki hapo, mpaka aje alevuke na mtoto atakuwa ameshaharibikiwa
 
Nahisi ni mapenzi tu. Jamaa akikunwa kunwa gololi zake, anacheka cheka tu na kusahau kufuatilia jinsi mtoto wake anavyoishi na mama yake wa kambo.
Huyo na wengine wa hivi hamna akili Wacha mfundishwe adabu.

Sijawahi penda na Wala haitakuja kutokea eti kupagawa na mwanamke sijui mzuri au viuno mara kukunwa,ni dalili ya kuwa na akili ndogo na weak emotional intelligence.
 

Mbinu aliyotumia ni sahihi, kasema alimnunulia mwanaye ila hazikumtosha ndio akatoa kama zawadi, angemnunulia moja kwa moja ingeibua timbwili lingine balaa.
Hapa itabidi ustawi jamii wahusishwe.
 
Wanaume wengi hawana muda wa kufuatilia mienendo ya watoto wao.

Binafsi nikirudi nyumbn kutoka kibaruani lazima niulize mtoto kashindaje, amekula nini na kama amekula vizur ama laah tena nikiwakuta hawajalala nawauliza wenyewe japo wanaishi na mama Yao mzazi.
 
Hili nalo ni tatizo,nikiona juzi kwenye Taarifa ya Habari ,mwanamama analaumu wazazi wa Kiume kutofuatilia mienendo ya Watoto.

Yule mama alitolea mfano wa Bwanake kwamba hajawahi fika shule Hadi mtoto anamaliza std seven ila anatoa ada tuu .

Wanaume wenzangu japo mara Moja Moja tuwe tunaenda kufuatilia miendendo ya Watoto Wetu shuleni na nyumbani ,hata hospital siku Moja unampa kampani mwanamke ,ni inatupa hatima nzuri uzeeni.

Mambo ya hela nk ni wajibu ila Kuna tuvitu unafanya kinaacha alama kwenye mioyo ya Watoto na wanawake.Fainali ni uzeeni.
 
Mwanamke mzuri na wa kumpenda kwa moyo wote ni mama mzazi tu aliekuzaa, akakuleta, kukusomesha na kukupambania katika maisha. Wengine wapo kwako kwa ajili ya something tu, hakuna cha zaidi ya hapo.
 
Mbinu aliyotumia ni sahihi, kasema alimnunulia mwanaye ila hazikumtosha ndio akatoa kama zawadi, angemnunulia moja kwa moja ingeibua timbwili lingine balaa.
Hapa itabidi ustawi jamii wahusishwe.
Asante mkuu kwa kumuelewesha jamaa ambae anaonekana hakuelewa vizuri nilichoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…