Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Home boy ndio baba mtoto mwenyewe aliekuja nyumban kunishambulia kuwa namhonga mkewe nguo ili nimtafune. Sasa ataendaje kujishtaki.

Mimi mwenyewe naweza kwenda kukilipua muda wowote. Yeye si amemwaga mboga, na mimi nitamwaga ugali tuone nani atapotea uraiani.
Usiende wewe aende huyo rafiki yenu wewe na "homeboy ", Kwa sababu tayari wewe una mgogoro na "homeboy". Lakini pia muwe na ushaidi wa kuthibitisha kwamba kweli uyo mtoto ananyanyaswa. ONGELA KWA KUJALI
 
Minadhani ulikosea mapema kutomweleza ukweli
Mimi niliogopa fitna katika ndoa za watu mkuu. Kuna midume mingine unaweza kuileza matatizo ya mke wake, badala lichunguze lenyewe linakwenda kumweleza mkewe kila kitu ulichomwambia.

End of the day unakuja kusutwa mbele ya watu nyumbani kwako. So niliamua nimsaidie yule mtoto kimya kimya tu.
 
Ni kweli bimadamu hubadirika,ila kununua nguo za mtoto na kumpa ni kosa pia.

Ungemchana live tu oya mbona dogo nguo zake zimechakaa hivi.Afu dogo mbina anakosa raha hebu fuatilia kitu juu ya dogo kama kipo sawa.
Hapo kweli hata mimi najilaumu, sema ndo ishatokea. Kilichobakia ni jamaa kuja kujua kinachoendelea. Wanasema dalili ya mvua ni mawingu.

So hii ni dalili ya jamaa kukaribia kujua ukweli hata kama sio kwangu basi ataujua hata kupitia mtu mungine. Wanasema safari moja huanzisha nyingine. So mimi nimeanza, kuna mungine atamalizia na siri kubumbuluka.
 
Ni juma hili walikuja watu wa wizara job ,Sasa nilikuwa kwenye kamati ya mapokezi hivyo hata vyumba vya kulala nilihusika Mimi ,si wamekuja na gumama guzuri ,gunene ,gweupe alafu ni gushangazi gwa kwenda huku na huku katika harakati zangu gukanipa namba .

Usiku wa pili baada ya vikao uchwara vya serikali visivyo na kichwa Wala minyoo si nikamtumia meseji Mimi nakupenda sana since day one nilipokuona Kama hutajali naomba tupate sehemu nzuri tuzungumze kwa kina . Hapo ilikuwa saa nne usiku ,meseji nilituma WhatsApp ,aliona na alisoma meseji kabisa .

Ila masikitiko yangu ni kuwa hakujibu chochote ,kazini kwangu nilikuwa mgeni naingia nanyata ,kwenye vikao siwezi kutizama watu sura ,gushangazi gunapendelea kunihoji Mimi maswali ,najibu huku nimeangalia chini ,yaani itoshe kusema nateswa kisaikolojia ,naiona ijumaa kuwa mbali huyu mama aondoke ,mwenzenu nitakufa kwa presha na aibu .

Sasa kuwa makini na mishangazi haifai
Nipe namba yake nikuonyeshepo jinsi ya kudeal na hayo madude
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Jirani na hapa nnapoishi mimi kuna home boy fulani ambae tumetokea kuzoeana, kushauriana na hata sometimes kutembeleana. Tulitokea kujuana nae miezi 6 iliyopita baada ya yeye na familia yake kuhamia hapa. Kwa Tanzania ni mzaliwa wa Kinondoni, wakati mimi mzaliwa wa Magomeni Dar es salaam, hivyo tunaishi kama ndugu.

Kabla ya kuishi na mke alie nae sasa hivi, alikuwa ashaoa mke wake wa kwanza ambae alizaa nae mtoto mmoja wa kiume. Lakini kwa bahati mbaya mkewe alifariki miaka 3 iliyopita na kuacha mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 4.

Baada ya mkewe kufariki, mwamba hakuchelewa, akakutana na huyu mkongo, akatangaza ndoa na kuanza maisha mapya (kumbuka hapo jamaa alikuwa na mtoto wa miaka 4), baadae na mkongo akamletea mtoto mungine wa kike, so jumla jamaa ana watoto wawili. Maisha yao huko walipokuwa haswa kwa upande wa mtoto wa kambo sijui yalikuaje, ila baada ya kuhamia jirani yetu na kufahamiana na jamaa, ndo nikaanza kuona mateso anayopitia mtoto.

Japo imezoeleka kuona mama wa kambo wengi ni makatili, lakini huyu aisee ni zaidi ya shetani. Hana chembe ya huruma, utu wala ubinadam. Anaweza kumpa mtoto adhabu ya kuweka miguu juu (ukutani) mikono chini (mfano wa sarakasi) kwa muda mrefu zaidi, bila kushusha miguu chini, na akishusha anakula kipondo ambacho anatakiwa kupigwa mwizi huko polisi.

Yote tisa, kumi ni pale anapomshindisha na njaa, alafu akigundua kuwa alikuja kwangu na wenzake (watoto wangu) akala, basi atachokutana nacho atajuta ni kwanini alimpoteza mama yake akiwa bado mdogo. Atapigwa, atapewa adhabu ya kuweka miguu juu, na kushindishwa na njaa.

Kila nlipotaka kumwambia jamaa kuhusu mateso anayopitia mwanae, moyo ulisita, nisije kuharibu ndoa ya watu au kusababisha matatizo zaidi kwa mtoto mwenyewe. So niliamua kushona mdomo wangu tu kama sijui kinachoendelea.

Huyu mama mwanzoni alianza kuwa karibu na mke wangu, kutokana na ukaribu uliopo mimi na mumewe. Lakini alipogundua kwamba mke wangu huwa na tabia ya kumpa chakula mtoto anaeteswa, na sometimes kumpa hela pamoja na watoto wangu ili wanunue vitu vidogo vidogo vya kula, basi yule mama wa kambo akakata mawasiliano na mke wangu, na madam nae akampotezea kwa kufuata ule msema wa "akunyimae kunde, anakupunguzia kuja...m..ba.

Mtoto bado mdogo (miaka 7) kumweleza baba yake anashindwa, na mama huwa hampi nafasi ya kumsogelea baba yake akae nae mwenyewe. Halaf mtoto nguo, na viatu vimemuishia mpaka aibu naona mimi.

Juzi alhamisi nikaona upuuzi, wakati natoka mihangaikoni kwangu nikaingia dukani nikanunua nguo suruali 5, T'shirt 5, mashati mawili, jacket za baridi 3, viatu pea 3 na sandroz pea 1. Nikaenda mpaka kwa home boy nikamkabidhi mkewe nikamwambia kuwa zile nguo na viatu nilikuwa nimemnunulia mwanangu, lakin kwa bahati mbaya nimekuta havimtoshi, so ndomaana nikaona nimpe yeye ambae vinaonekana kumtosha, alaf mimi nitaenda na mtoto wangu town nikamnunulie vingine. Yule mama akapokea, lkn ni kwa shingo upande (kumbuka ni shemej yangu) halaf sina ugomvi nae yeye wala mumewe. So hakuwa na nguvu ya kukataa uso kwa uso.

Kumbe na yeye jana alienda town, akanunua nguo zake kadhaa, na kuja nazo nyumban kwa malengo yake binafsi. Usiku mumewe alipofika akaanza kumwambia kuwa mimi nimekuwa nikimtongoza na kumtaka kimapenzi muda mrefu bila mafanikio, na kwamba nilifikia hadi hatua ya kumnunulia yeye na mtoto (wa kambo) nguo ili anikubali, lakini bado alinikwepa na kuchukua tu nguo ili aje amuonesha (mumewe) nk.

Home boy alipotaka ushahidi yule mama akaenda kutoa zile nguo alizoenda kununua jana town, akajumlisha na zile nilizopeleka kwa ajili ya kumpa mtoto wa kambo anaeteseka. Aisee sijui jamaa alikuwa katika hali gani usiku ule na sijui alilalaje.

Asubuhi naona home boy anakuja nyumban bila salam anaanza kunibwatukia mbele ya mke wangu na watoto wangu. Namuuliza tatizo nini, anabwaga zile nguo mbele yangu na kusema eti ashajua kila kitu kuhusu mpango wangu wa kumtongoza mkewe.

Eti natongoza kishamba sana kwa kukimbilia kuhonga nguo. Yani nikashindwa kumuelewa vizuri, mpaka alipofafanua kwamba nilikuwa namtongoza mkewe, nilipoona hakubaliani na mimi ndo nikaenda town kununua vijinguo vya kumlaghai ili nimpate kiurahisi nk.

Nikataka kutumia ukaribu wetu kumueleza kile kinachoendelea katika familia yake mpaka mimi kufikia hatua ya kununua zile nguo za mtoto wake, lakini bingwa hakunielewa, akawa mtata mwisho nikamuacha aongee akichoka aamue mwenyewe anachotaka kufanya.

Baada ya kuona lengo lake la kunichafua mbele ya familia yangu limefeli akaondoka akidai kuanzia leo mimi na yeye ni maadui. Nisimjue, asinijue, nisiende kwake, na hatokuja kwangu, kila mtu aangalie maisha yake, nikamwambia poa.

Kwa bahati nzuri mke wangu anajua kila kinachoendelea, so ile complain ya kumtongoza mkewe haikumuingia akilini.

Namuonea huruma sana home boy, ni kama mapenzi yamemfanya asifatilie kinachoendelea katika nyumba yake. Damu yake inateswa, na sisi tunaosaidia tunaonekana wabaya. Mateso anayopitia yule mtoto hakuna mtu yoyote mwenye huruma hapa JF anaweza kuyaona akayavumilia.

Nilikuwa na mpango wa kwenda ku report swala hili katika mamlaka husika, lakini kuna rafiki yetu (mimi na yeye) amesema nisubiri kwanza jamaa hasira ziishe hata week 1 au 2, halafu aite kikao kati yangu na home boy kwa ajili ya maridhiano, halaf hapo kwenye kikao ndo nitumie chance hiyo kumueleza home boy kile kinachoendelea katika familia yake, na sababu ya mimi kumpelekea yule mtoto zile nguo na viatu.

Huyu rafiki mimi nimemuelewa, lkn sielewi ni vipi mpaka leo jamaa haoni kuwa mtoto wake anateseka hata kwa muonekano tu wa macho. Ama kweli tenda wema uende zako. Na sio kila mwenye macho huona kilichopo mbele yake. Jamaa haoni na hasikii.

Dah...
Sijui hii Ina ukweli kiasi gani, kama ni kweli, tegemea yafuatayo. Mtoto huyo atapata udumavu wa kukua, ulemavu wa kudumu, tatizo la akili na mwisho kifo. Usipotoa taarifa sehemu husika, utakuwa umeshiriki kumuumiza
Ukitaka kufanya jambo lolote na mke wa rafiki yako, wasiliana na rafiki yako kwanza sio unamgongea shemeji yako na zawadi mumewe akiwa hayupo.
Haya mawazo ya ngono muda wote hata kwa mambo ya msingi tutafika ?
 
Zipo tena huku ndio balaa mkuu. Nafikiri muda wowote kuanzia sasa nitalifikisha swala hili mahali husika, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.
Kaka nenda karipoti.

Mostly abusers hua wanaongeza adhabu nikimaanisha anaona adhabu hii huyu kashaiona ndogo so inapanda.

Huu muda unaosema muda wowote kuanzia sasa huyo abuser anaongeza adhabu kisha dogo anapoteza uhai au anakua kilema.

Utaishia kujiuliza nafsi ikiwa ungeripoti asingefikia huko.

Kama dogo anasoma shule ilibidi wawe wa kwanza kuona makovu na majeraha na kuripoti kwa social welfare. Kama hasomi wewe jirani hilo ni jukumu lako.

Muokoe mtoto
 
Nipe namba yake nikuonyeshepo jinsi ya kudeal na hayo madude
😀😀 Nilifuta siku ya pili yake baada ya kuwa tupo lunch tunakula eti ananiuliza mbele ya watu ,
Mshangazi gaidi :kijana umeshiba ? Maana huko ndani sitaki miayo 🙃

Mnyonge Mimi wa mapenzi : Nimeshiba mkuu .

Mshangazi gaidi: Basi sawa tukafanye kazi sasa
 
Kaka nenda karipoti.

Mostly abusers hua wanaongeza adhabu nikimaanisha anaona adhabu hii huyu kashaiona ndogo so inapanda.

Huu muda unaosema muda wowote kuanzia sasa huyo abuser anaongeza adhabu kisha dogo anapoteza uhai au anakua kilema.

Utaishia kujiuliza nafsi ikiwa ungeripoti asingefikia huko.

Kama dogo anasoma shule ilibidi wawe wa kwanza kuona makovu na majeraha na kuripoti kwa social welfare. Kama hasomi wewe jirani hilo ni jukumu lako.

Muokoe mtoto
Shukran mkuu ngoja niufanyie kazi ushauri wako 🙏
 
mijike mingine ina roho mbaya ,sasa chakula kanunua baba yake mpe ale ili akue akupishe hapo ebo!
Mingine kama hili limetoka katika nchi ya vita na njaa, sasa limefika katika amani na chakula kedekede linasahau na kuanza kumtesa mtoto wa mwenzake.

Hili ndio tatizo la jitu jeusi, likishiba tu linasahau shida 🤣🤣🤣
 
Yaani wewe jamaa hufai, mtoto anateswa na kunyanyaswa katika umri huo ushindwa kuchukua hatua? Eti ulikuwa ukiongopa kumwambia homeboy wako? Kama kweli ulikuwa na nia ya kusaidia ulishindwa kureport Police kimya kimya? Ulishindwa kutoa taarifa ustawi wa jamii? Serikali za mitaa hukujui? Acha hizo za kuja kutafuta huruma hapa, wewe kama mzazi ulipaswa kuvaa viatu vya huyo mtoto na ungechukua hatua
 
Kama hii story ni ya kweli, basi kuna mahali ulikosea kabla ya kufanya maamuzi ya kununua nguo. Ulipaswa umweleze baba wa mtoto hizo changamoto tena mbele ya huyo mama mlezi.
Ungetumia mbinu za kipelelezi kujua nini hasa sababu za hizo adhabu

Ungewatoa out watoto wote, wako na wale wengine wawili, na kuwanunulia hizo zawadi kwa pamoja.

Hata hivyo zama za leo chanagamoto za malezi ni nyingi sana. Wazazi/walezi wengi wana msongo wa mawazo unaosababisha changamoto ya afya ya akili. Mtu mwenye akili timamu huwezi kumuadhibu mtoto kupita kiasi
Asante kwa ushauri mzuri mkuu. Inaonesha una moyo wa upendo sana, na unaweza kulea mtoto ambae sio wa kwako.

Mungu akubariki na kukuongoza kwa kila jambo zuri unalofanya.
 
hongera umefanya kazi nzuri ila ni vema ukiona ngumu kulikamilisha kumsaidia mtoto, tumua asasi za kiraia zinazohusika na masuala ya kijamii,mtoto atasaidiwa na ukweli utajulikana.
 
Back
Top Bottom