Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Mpaka nakuwa mkubwa na umri wangu huu sijawai shuhudia mama wa kambo mzuri kwa mtoto wa mwanaume pindi wanapo ishi nyumba moja.
Mimi nimeshuhudia mmoja bongo, alikuwa mpangaji wetu. Alimpenda binti yake wa kambo kama ampendavyo mwanae, hadi ilikuwa ngumu kujua kama yule binti sio mwanae. Japo sina uhakika kama wema huo uliendelea mpaka ukubwani, au alikuja kumbadilikia.

Maana walihamaga home wakahamia maeneo ya kigogo barafu.
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Jirani na hapa nnapoishi mimi kuna home boy fulani ambae tumetokea kuzoeana, kushauriana na hata sometimes kutembeleana. Tulitokea kujuana nae miezi 6 iliyopita baada ya yeye na familia yake kuhamia hapa. Kwa Tanzania ni mzaliwa wa Kinondoni, wakati mimi mzaliwa wa Magomeni Dar es salaam, hivyo tunaishi kama ndugu.

Kabla ya kuishi na mke alie nae sasa hivi, alikuwa ashaoa mke wake wa kwanza ambae alizaa nae mtoto mmoja wa kiume. Lakini kwa bahati mbaya mkewe alifariki miaka 3 iliyopita na kuacha mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 4.

Baada ya mkewe kufariki, mwamba hakuchelewa, akakutana na huyu mkongo, akatangaza ndoa na kuanza maisha mapya (kumbuka hapo jamaa alikuwa na mtoto wa miaka 4), baadae na mkongo akamletea mtoto mungine wa kike, so jumla jamaa ana watoto wawili. Maisha yao huko walipokuwa haswa kwa upande wa mtoto wa kambo sijui yalikuaje, ila baada ya kuhamia jirani yetu na kufahamiana na jamaa, ndo nikaanza kuona mateso anayopitia mtoto.

Japo imezoeleka kuona mama wa kambo wengi ni makatili, lakini huyu aisee ni zaidi ya shetani. Hana chembe ya huruma, utu wala ubinadam. Anaweza kumpa mtoto adhabu ya kuweka miguu juu (ukutani) mikono chini (mfano wa sarakasi) kwa muda mrefu zaidi, bila kushusha miguu chini, na akishusha anakula kipondo ambacho anatakiwa kupigwa mwizi huko polisi.

Yote tisa, kumi ni pale anapomshindisha na njaa, alafu akigundua kuwa alikuja kwangu na wenzake (watoto wangu) akala, basi atachokutana nacho atajuta ni kwanini alimpoteza mama yake akiwa bado mdogo. Atapigwa, atapewa adhabu ya kuweka miguu juu, na kushindishwa na njaa.

Kila nlipotaka kumwambia jamaa kuhusu mateso anayopitia mwanae, moyo ulisita, nisije kuharibu ndoa ya watu au kusababisha matatizo zaidi kwa mtoto mwenyewe. So niliamua kushona mdomo wangu tu kama sijui kinachoendelea.

Huyu mama mwanzoni alianza kuwa karibu na mke wangu, kutokana na ukaribu uliopo mimi na mumewe. Lakini alipogundua kwamba mke wangu huwa na tabia ya kumpa chakula mtoto anaeteswa, na sometimes kumpa hela pamoja na watoto wangu ili wanunue vitu vidogo vidogo vya kula, basi yule mama wa kambo akakata mawasiliano na mke wangu, na madam nae akampotezea kwa kufuata ule msema wa "akunyimae kunde, anakupunguzia kuja...m..ba.

Mtoto bado mdogo (miaka 7) kumweleza baba yake anashindwa, na mama huwa hampi nafasi ya kumsogelea baba yake akae nae mwenyewe. Halaf mtoto nguo, na viatu vimemuishia mpaka aibu naona mimi.

Juzi alhamisi nikaona upuuzi, wakati natoka mihangaikoni kwangu nikaingia dukani nikanunua nguo suruali 5, T'shirt 5, mashati mawili, jacket za baridi 3, viatu pea 3 na sandroz pea 1. Nikaenda mpaka kwa home boy nikamkabidhi mkewe nikamwambia kuwa zile nguo na viatu nilikuwa nimemnunulia mwanangu, lakin kwa bahati mbaya nimekuta havimtoshi, so ndomaana nikaona nimpe yeye ambae vinaonekana kumtosha, alaf mimi nitaenda na mtoto wangu town nikamnunulie vingine. Yule mama akapokea, lkn ni kwa shingo upande (kumbuka ni shemej yangu) halaf sina ugomvi nae yeye wala mumewe. So hakuwa na nguvu ya kukataa uso kwa uso.

Kumbe na yeye jana alienda town, akanunua nguo zake kadhaa, na kuja nazo nyumban kwa malengo yake binafsi. Usiku mumewe alipofika akaanza kumwambia kuwa mimi nimekuwa nikimtongoza na kumtaka kimapenzi muda mrefu bila mafanikio, na kwamba nilifikia hadi hatua ya kumnunulia yeye na mtoto (wa kambo) nguo ili anikubali, lakini bado alinikwepa na kuchukua tu nguo ili aje amuonesha (mumewe) nk.

Home boy alipotaka ushahidi yule mama akaenda kutoa zile nguo alizoenda kununua jana town, akajumlisha na zile nilizopeleka kwa ajili ya kumpa mtoto wa kambo anaeteseka. Aisee sijui jamaa alikuwa katika hali gani usiku ule na sijui alilalaje.

Asubuhi naona home boy anakuja nyumban bila salam anaanza kunibwatukia mbele ya mke wangu na watoto wangu. Namuuliza tatizo nini, anabwaga zile nguo mbele yangu na kusema eti ashajua kila kitu kuhusu mpango wangu wa kumtongoza mkewe.

Eti natongoza kishamba sana kwa kukimbilia kuhonga nguo. Yani nikashindwa kumuelewa vizuri, mpaka alipofafanua kwamba nilikuwa namtongoza mkewe, nilipoona hakubaliani na mimi ndo nikaenda town kununua vijinguo vya kumlaghai ili nimpate kiurahisi nk.

Nikataka kutumia ukaribu wetu kumueleza kile kinachoendelea katika familia yake mpaka mimi kufikia hatua ya kununua zile nguo za mtoto wake, lakini bingwa hakunielewa, akawa mtata mwisho nikamuacha aongee akichoka aamue mwenyewe anachotaka kufanya.

Baada ya kuona lengo lake la kunichafua mbele ya familia yangu limefeli akaondoka akidai kuanzia leo mimi na yeye ni maadui. Nisimjue, asinijue, nisiende kwake, na hatokuja kwangu, kila mtu aangalie maisha yake, nikamwambia poa.

Kwa bahati nzuri mke wangu anajua kila kinachoendelea, so ile complain ya kumtongoza mkewe haikumuingia akilini.

Namuonea huruma sana home boy, ni kama mapenzi yamemfanya asifatilie kinachoendelea katika nyumba yake. Damu yake inateswa, na sisi tunaosaidia tunaonekana wabaya. Mateso anayopitia yule mtoto hakuna mtu yoyote mwenye huruma hapa JF anaweza kuyaona akayavumilia.

Nilikuwa na mpango wa kwenda ku report swala hili katika mamlaka husika, lakini kuna rafiki yetu (mimi na yeye) amesema nisubiri kwanza jamaa hasira ziishe hata week 1 au 2, halafu aite kikao kati yangu na home boy kwa ajili ya maridhiano, halaf hapo kwenye kikao ndo nitumie chance hiyo kumueleza home boy kile kinachoendelea katika familia yake, na sababu ya mimi kumpelekea yule mtoto zile nguo na viatu.

Huyu rafiki mimi nimemuelewa, lkn sielewi ni vipi mpaka leo jamaa haoni kuwa mtoto wake anateseka hata kwa muonekano tu wa macho. Ama kweli tenda wema uende zako. Na sio kila mwenye macho huona kilichopo mbele yake. Jamaa haoni na hasikii.

Dah...
Kosa lako ni kununua nguo na kumpa mke wake badala ya kumpa muwe wake basi.

Mengine ulikua sahihi kabisa
 
Wewe nimuokozi unacho fanya najua huwezi kukiacha kwakua by nature upo kwaajiri ya jambo hilo kamwe usiache hata kidogo👈
Siwezi kuacha mkuu, halafu uzuri nina backup ya mke pamoja na watu wengine wanaoona mateso ya yule mtoto. Ikishindikana nitachukua hatua zaidi mkuu.
 
Minadhani ulikosea mapema kutomweleza ukweli
 
Kwa jinsi tulivyokuwa tunaishi na mumewe, sikutegemea kama tungefikia huku aisee.
Ni kweli bimadamu hubadirika,ila kununua nguo za mtoto na kumpa ni kosa pia.

Ungemchana live tu oya mbona dogo nguo zake zimechakaa hivi.Afu dogo mbina anakosa raha hebu fuatilia kitu juu ya dogo kama kipo sawa.
 
Na hapa kuna sheria zinazofanana na nyumban mkuu. Lakini hapa tulipo mtu kukutumia watu waje kuchukua roho yako ni sekunde tu.

So hii inanifanya nikubaliane na ushauri wa rafiki yetu kutukutanisha na kuliongelea swala hilo mbele yake. Maybe he will do something better to his son.
Pole sana kwa changamoto, Mungu anaona nia yako. Mshauri aweke cctv ndani kwake kwa siri ajionee mwenyewe, siku hizi si jambo geni kuwa na camera nyumbani kwako
 
Mtafute rafiki yake mwingine amfikishie ujumbe wa mtoto wake kuteswa kabla ya kikao chenu. Ikifanyika hivi na huku amekubali kuwepo kikaoni, itakuwa rahisi kwako kumfikishia ujumbe kwa mapana yake. Lakini mkimshitukiza kikaoni, kuna uwezekano akaanzisha fujo nyingine, ambayo haitakuwa na afya kwenye nia yako ya maridhiano.

Kila la kheli..!!
Shukran mkuu kwa ushauri wako 🙏
 
Kuna theory inasema abuser hawezi kuacha abuse hadi anakufa, na abuser hawezi kulenga mtoto tu hata huyo bwana I believe huko ndani anapitia mazito, wanaume wa kiafrika hatunaga ujasiri wa kujitokeza kusema na kujifanya tupo stoic sana na hasa akiwa mke mzuri wa sura au ana kipato zaidi. Lazima kila rangi humo ndani anakutana nayo na bahati mbaya sana watoto ndio huwa wanakuwa victims kutoka kwa parties zote. So naamini hatapata ushirikiano wowote kutoka kwa home boy na pia huyo mama anamjua sana bwana wake ndio maana alifanya alichofanya ili jamaa aondoke kwenye maisha yao.
Inawezekana ulichoandika kina ukweli ndani yake mkuu.
 
Ni kweli, lakini abuser wengine huwa hivyo kwa kukosa information fulani. Na kwa msingi huu ndo nimeona kabla ya kikao, homeboy apewe taarifa na rafiki mwingine. Ili kama kuna kukataa, basi atakataa hata kuwepo kikaoni, na hapo ndipo jamaa msamalia mwema atatakiwa kuachana na jambo hili. Au la kama anaweza, jamaa yetu awatonye watu wa dawati.
Kwa sasa nasoma upepo mkuu, nikiona mpaka home boy na yeye haeleweki basi nalifikisha swala hili mahali husika. Potelea mbali liwalo na liwe.
 
Huko unapoishi hakuna social welfare departments?

Nenda karipoti anonymously
Zipo tena huku ndio balaa mkuu. Nafikiri muda wowote kuanzia sasa nitalifikisha swala hili mahali husika, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.
 
We mushangazi huwa nakuamini sana kwa ushauri wako,i love yuo mshangazi
Ni juma hili walikuja watu wa wizara job ,Sasa nilikuwa kwenye kamati ya mapokezi hivyo hata vyumba vya kulala nilihusika Mimi ,si wamekuja na gumama guzuri ,gunene ,gweupe alafu ni gushangazi gwa kwenda huku na huku katika harakati zangu gukanipa namba .

Usiku wa pili baada ya vikao uchwara vya serikali visivyo na kichwa Wala minyoo si nikamtumia meseji Mimi nakupenda sana since day one nilipokuona Kama hutajali naomba tupate sehemu nzuri tuzungumze kwa kina . Hapo ilikuwa saa nne usiku ,meseji nilituma WhatsApp ,aliona na alisoma meseji kabisa .

Ila masikitiko yangu ni kuwa hakujibu chochote ,kazini kwangu nilikuwa mgeni naingia nanyata ,kwenye vikao siwezi kutizama watu sura ,gushangazi gunapendelea kunihoji Mimi maswali ,najibu huku nimeangalia chini ,yaani itoshe kusema nateswa kisaikolojia ,naiona ijumaa kuwa mbali huyu mama aondoke ,mwenzenu nitakufa kwa presha na aibu .

Sasa kuwa makini na mishangazi haifai
 
D

Dudumizi mwambie akupe weye umlee dogo akikataa ndio mpatie kichambo chake kama anateswa sana.
Katika watu walionishauri vizuri, na wewe pia ni mmoja wapo. Huu ushauri wako siwezi kuuacha. Lazima niiufanyie kazi kama ulivyoshauri 🙏
 
Meseji nimeipata hapo kuwa wanawake asilimia kubwa ya wanawake wana uwezo mdogo wa kuchanganua mambo yanayokuja mbeleni. Sasa hapo kaenda kujinunulia nguo ili aseme umemuhonga wakati ipo siku itafamika kwamba alidanganya na hapo muwe wake ataoneka mke wake ni mfitinishaji wa kiwango cha tp mazembe.
Huyu alijua akifanya hivi atanikomoa mimi katika ndoa yangu, na atatufitinisha na mumewe. Kwa bahati mbaya au nzuri katika ndoa yangu hajafanikiwa hata robo.

Na kwa mumewe nina hakika siku akija gundua kama ulivyosema, atapata aibu na hatoaminika tena katika ndoa yake.
 
Ustawi wa jamii ndio mwisho wa Hilo tatizo ila usiende wewe aende hata uyo rafiki yenu, ww na huyo unae mwita "homeboy"
Home boy ndio baba mtoto mwenyewe aliekuja nyumban kunishambulia kuwa namhonga mkewe nguo ili nimtafune. Sasa ataendaje kujishtaki.

Mimi mwenyewe naweza kwenda kukilipua muda wowote. Yeye si amemwaga mboga, na mimi nitamwaga ugali tuone nani atapotea uraiani.
 
Back
Top Bottom