Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari Wakuu!
Kukaa miaka mitano tuu ndio ujifanye Mzungu?
Kukaa miaka mitano tuu ndio ushindwe kuongea Kiswahili bila kuchanganya na kimombo?
Ati mjanja! Ati anajiita Civilized, Mpuuzi tuu!
Kitu kidogo utasikia; yaani wabongo hampo civilized! Mara ataje Ridiculous! Na msamiati mingine migumu migumu akidhani nitamuogopa. Taikon haogopi mtu hata angekuwa anaongea kingereza cha Biblia.
Mwanzoni nilikuwa namvumilia lakini nahisi hasira zangu zinanishinda, na wote mnajua hasira za Taikon zilivyo, Mimi sipendi dharau za kijinga jinga.
Naiomba serikali imuonye huyu rafiki yangu, msije sema nijiepushe naye wakati mnajua bado anavihela alivyokuja navyo. Bado navihitaji.
Wiki iliyopita nilimpokea Rafiki yangu pale uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, tayari nilikuwa nimebook Bolt hivyo rafiki yangu alivyofika tuu tukaanza safari ya kuelekea KIJITONYAMA kwenye moja ya Hotel ya Nyota tatu hivi.
Sitasema mambo ya Barakoa hapa, labda badae hasira zangu zikipanda kadiri ninavyoandika.
Njiani tulipigia Stori za hapa na pale tukicheka na kukumbushana mambo yote ya Chuo kikuu tuliyokuwa tuliyafanya Enzi zile tunasoma. Ni mpaka tunafika Hotelini ndipo Stori zilipokoma.
Fred akaniambia amemisi Kiepe mayai na vigondi vya uswahili. Unajua saa ngapi hiyo, Saa mbili usiku inaelekea saa tatu, tukaita Bolt, hao mpaka Tandale Uzuri pale Sweet Corner, watu wote wanatushangaa na hapo ndipo kero ilipoanzia.
Watu wote hatujavaa barakoa, Fred pekeake na barakoa yake utadhani Daktari wa upasuaji. Hilo nikakausha, lililokuwa linaniudhi ni Kauli yake ya kila mara kuwa Pananuka, mara mmh pachafu basi ilimradi tu, tukachukua Kiepe yai, kuku pamoja na vigondi bila kusahau firigisi.
Tukarudi Hotelini baadaye nikamuacha nikarudi Geto langu.
Kesho yake ilikuwa jumatatu akanipigia Asubuhi Asubuhi nimfuate, si unajua Vijana wa mjini wengi wetu hatuna mbele wala nyuma, hatuna Ratiba wala Kalenda, tupotupo tu.
Sina kazi! Sina kibarua maisha Kama ya Kunguru vile. Huyo nikaenda KIJITONYAMA, hapo nikamkuta Fred ameshajiandaa, Bolt ikaja hao mpaka Posta, tukaenda kwenye ofisi ya kukodishia magari, tukakodisha Gari Fred akiacha Passport Yale na Dola za kimarekani Kama 3000 hivi Kama rehani.
Tukaondoka. Sasa tukiwa ndani ya Gari. Muda wote Fred akiwa nyuma ya barakoa yake.
Msije mkadhani tulichukua Gari ya kipuuzi, tulichukua Gari haswa, Ilikuwa Sijui Toyota Fortunes ya kijivu iliyokolea.
Tumefika Kariakoo, tukatafuta sehemu ya kuegesha Gari, tukaliegesha.
"Watanzania wanatembea Sana Dololo, yaani akili zao zipo Dololo Kama Kobe" Fred huyo akasema.
Nikavumilia, ni kweli Watanzania wengi wetu tukitembea tunatembea Dololo lakini nikajiuliza tutembee haraka kwani tunapenda wapi, hatuna Jambo la maana huko tuendako, huko tuendeko sio kazini, sio ibadani, hakuna la muhimu lolote lile, sasa Kwa nini tujitese.
Nikatamani nimuulize, Mimi mwenyewe Taikon nimekuja Kariakoo sijui nimekuja kufanya nini zaidi ya kumsindikiza yeye, Fred. Sasa nitatembeaje harakaharaka.
Wengi wetu tuwapo barabarani tunaenda kwenye vijiwe vya Umbeya na majungu, labda tunaenda kuangalia mpira au kubet hivi kweli hayo ndio yatufanye tutembee harakaharaka.
Haraka hiyo viipi. Haraka huna pesa ukijikwaa ukatoa kucha huna hata pesa ya kwenda Hospitali, Bima ya Afya Nani angekuwa nayo Kama Sisi wenyewe makabwela.
Haraka natembeaje Kwa mfano ili nikanyage bidhaa za watu nipewe kichapo cha mbwa Koko!
Kwanza kutembea haraka haipo kwenye ilani ya Vyama vya Siasa, wala haipo kwenye Sera ya nchi, wala haipo kwenye katiba, hata kwenye sheria za halimashauri hakuna, sasa tunatembeaje haraka haraka.
Fred amekomalia tupo Dololo, mitembeo Dololo, Dololo! DOLOLO!
Fred hata Kama pesa zako nazivizia pasipo uzia, nazitaka Pasi na Shaka! Lakini matusi yako yamefika ukingoni mwa yordani,
Nitaihimiza serikali ikufunze adabu Kwa adhabu Kali.
Tukatoka huko huku kinyongo likiwa bado kipo shingoni Kama Rovu. Mvumilivu hula mbivu, Fred akanipa laki moja kama Shukrani ya kumsindikiza na kutoa muda wangu.
Mambo si ndio hayo. Akaniuliza naishi wapi, nikamwambia naishi Tandale Kwa Mtogole, Ati hakujui! looh! Hakumbuki miaka hiyo tupo Chuo tulipokuwa tunakuja mitaa hiyo kushangaa madadapoa wa pale uwanja wa fisi, ati hayo kasahau. Sikumjali.
Tulipofika Kwa mtogole nikamuomba aniache barabarani tuu nitafika mwenyewe, lakini akakataa katakata, nikaona huu msala Kama sio msalaba.
Nikamuambia Gari haiwezi ingia mpaka ninapoishi, akasema tutaliegesha sehemu nikamuambia huku kuna vibaka wanaweza iba chochote katika Gari, akang'angana wee! Nikasema liwalo na liwe
Hao tukaegesha gari, safari ya kuelekea Ghetto la Taikon ikaanza, watu wote walikuwa wakitushangaa, ungejiuliza tulikuwaje, si nibarakoa ya Fred ambayo ipo kiwadhifa hivi, sip hizi barakoa za Mia tano, yeye anadai ati aliinunua Dola 20 pale London. Haya bhana!
Njiani akawa ananiuliza ilikuwaje nikawa naishi sehemu Kama Ile, ati kijana msomi, mwenye nguvu na akili timamu hawezi ishi Maeneo Kama Yale.
Kidogo nighairi kumpeleka lakini tayari tulikuwa tumefika. Ghetto la Taikon mlango wake wa kitasha. "sijui kama mademu pisi Kali wanaingiaga humu" Fred huyo akasema.
"Hii picha inafanyaje humu?" Fred akauliza. Akiangalia moja ya picha kubwa za stika nilizobandika ukutani.
Ilikuwa picha kubwa inayomuonyesha Bob Marley akiwa anavuta Sigara, upande mwingine ilikuwepo picha ya mwanamke mzuri wa kizungu aliyevalia kichupi na sidilia ya Rangi ya waridi.
Nikamjibu HAO ni rafiki zangu, Fred akacheka Sana.
Yaani msomi mzima unaishi kwenye Ghetto Baya Kama hili, alafu unabandika mapicha yasiyoeleweka ukutani ya wavuta bangi, na huyu mcheza Pono hapa.
Akaendelea; Taikon nimekudharau.
Ghetto Kama la msela mavi.
Nikamwambia wananchi karibia wote wa Tanzania wanaishi Kama Mimi, tafadhali usitutukane,
Maisha yetu yakisela muda wowote jela.
Kama hutakuta picha ya Bob Marley basi utamkuta Tupac, usijemsahau Ronaldo au Messi, utamuona pia Diamond au alikiba, pia kuta zetu za kisela utakuta Timu ya Simba au yanga, ndio maghetto yetu hayo.
Labda ningesahau picha za manabii kina Gwajiboy na Mwaimpoboy, ndivyo tunavyoishi hivyo.
Akaishia kusema nyie ni wajinga Sana.
Nikamjibu ujinga ndio Biashara ya Wakubwa!
Subirini!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
DAR ES SALAAM