Palina
JF-Expert Member
- Oct 9, 2021
- 3,551
- 9,522
Wakuu wazima humu ndani? Dah siku ya jana mida kama hii mchana. Rafiki yangu wa kike mmoja alikuwa akitokea ferri kwa usafiri wa mwendokasi akiwa ameweka simu yake kwenye beg la mgongoni lakini kabla ya kufika alipokuwa akienda alikuja kushtuka beg lake likiwa wazi na simu yake aina ya iPhone 7 ikiwa imeshaibiwa maeneo ya Fire [emoji22]
So sad... Simu sio ya kwangu but imeniuma sana maana simu kanunua mwezi machi tu hapa ikiwa mpya na haijamaliza ata miezi mingi tayari imeibiwa [emoji2359]
Hawa wezi wa Dar bhana... Binafsi tokea nimezaliwa mpaka leo hii sijawai kuibiwa kitu changu popote pale nitakapoenda na sitamani ije itokee kwangu kitu kama hicho.
Je wakuu hapo hakuna namna nyingine inaweza kurudi?
Poleni, Kama anakumbuka Apple ID username na password yake a log in kwa PC kule aende ikaizime simu
yule alieiba haezi ifungua labda aiuze na atakae nunua ni hivohivo
Heri tupate hasara wote asee