Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Hahaaa we noma[emoji119][emoji119]
 
Ushawahi kua na kesi hata ya madai luck?
 
Yupo mwingine namjua
Mgogoro wa ndoa na kesi za mahakamani, alikua na maisha mazuri nasikia now kapoteza kila kitu hadi nyumba yake anatembea anaongea mwenyewe barabarani.
Wanawake tuwe na huruma
Mgao wa 30/70 ama sio huyo?
 
,"nliongeza nyumba za kupangisha tu nkiwa nae"
Unaijua the so called the law of marriage Act? Nenda ukasome s. 160
Inshort chochote ulichokifanya ukiwa nae haijarishi alichangia au lah lazima mgawane.

Afu usiwe na kinyongo na mali zako oa mwanamke anaejitambua na anajua sheria inasemaje, mambo ya mali ukishakufa wanakula watakao baki.

Omba uwe na mke anaejielewa hizo mali hata uandike majina ya wazazi wako haina mantiki

Think about living a happy life thats all.
 
Tatizo vijana wengi wanasubir wapate mali nyingi ndo waoe. Cha kushangaza sasa hawajui kama mke aliyenae amempenda yeye au mali zake. Wanakujua kugundua mwishoni kabisa baada ya kupitia magumu flani. Usiwaambie wafu wasioe kwasababbu unakosea na unahamasisha watu wazini.. bali washaur watu watafute wenza sahihi watao wapenda kwa hali yoyote.
 
Haawa viumbe bwana ...wakikupanda lazma utakuwa chizi ...
Mimi it was half way nilipandwa walionizunguka wakijua Hilo ..Mimi pekee yangu ndo nilijiona najua kubembeleza ndoa...

Siku Moja niliwaza siku nzima mpaka saa Kuni usiku nimekaa bar napiga via mdo mdo .huyu mwanamke hata kuniuliza uko wapi hakuna Ila yupo online nk...na hapo kulikuwa na ma skendo mengi niliyapuuzia ... Nikaamua siku hiyo hiyo navunja ndoa TU kiroho safi nimuombe tuachane maisha yasonge

Akaelewa kwel kiroho safi

ASE long story short week baada ya hii transition nikawa natafuta sehem ya kupanga Ila nalala chumba Cha wagen ..hata watoto wahaelewi mchezo...bwana bwana jioni asimlete uyo jamaa niliesikia ana chepuka nae..kaja kusalimia..
Mimi huwa kikaz nipo mkoa jirani..Kwa mwez unakuta nashinda kama week TU...
Aseee nikaliita jembe langu first born kumuuliza vyema..uyu anko mnamfaham..akasema anakujaga kusalimia..afu alituletea tv baada ya Ile kuvunjika(Kuna tv Walivunja madogo..nilimuagiza mama Yao atafute nyingine nitume Hela akapata nikalipia direct Sasa uyu mwanamke alimshtua mwamba apitie apeleke home )

Aahhh niliagiza watoto waende Kwa shangazi na dada wa kazi...
Yule jamaa nikamwambia ntakuua sepa..kwakuwa sikuwahi kupiga yule mwanamke..alijiamini kabisa hatoguswa...
Mtume walaiii hatokuja sahau...nilimtwanga yule mwanamke siku Ile...aliuguzwa mwezi mzima..nilitoka nikaenda polis nikakaa kama siku tatu...mpaka msala umeisha talaka juu ...

Nikasepa nikaanza upya..marafiki na ndugu walinitia moyo Sana ..niliacha Kila kitu ..

Miaka mitano baadae nimebarikiwa mtoto mwingine kakiwanja na gari Yan maisha matam Nina ka mwanamke kabich mno Hela hizi ..yule chizi nae kazaa uko na yule mpuuz wake..wanangu mmoja nakaa nae mmoja anakaa nae .Ila naona nae anamshinda ntamchukua tu
 
1. Utamjuaje anakupenda huku una Mali?
2. Unajua kuwa wanawake wengi huficha makucha kabla ya kuolewa?
3. Kama sio pesa nitayawezaje makujumu ya familia?

ANY WAY; hivi unajua dunia ya sasa haina upendo TOTALLY?

#YNWA
 
Hongera kwa KUVUKA.

#YNWA
 
Depression inaua mkuu
Inapelekea denial , then confusion then kinachofwata hapo bila msaada wa kitabibu tunakusahau
Huyo hakuwa na family support
Social cohesion ilikuwa chini sana...
Stress zipo tu ila kama una wanafamilia na jamii iliyoupande wako unavuka tu mbona
Siku hizi raia wako bizee na kutafuta hela na kusahau wenzao.

Hata Mimi huwa najishangaaga tu, naamka saa 10 alfajiri kwenda kazini na kurudi saa 3 usiku.
Nikirudi nianze kupika na kufanya staffs za home.

Hapo sasa ndio Nina ndugu wa kuhitaji kampani, aisee anaweza kufa bila kuniona.

#YNWA
 
Omba uwe na mke anaejielewa.
Kumpata huyo anaejielewa dunia ya sasa ni KIPENGELE.
Binadamu tumekuwa ma "master" kuficha uchafu we.

Humo kwenye ndoa ndio balaa.
Nina kaka angu alioa mke mwenye tabia njema ila kufika kwenye ndoa bana, mke ni mbabe, anajua kila kitu.

Kumuuliza bro anasema "urafiki na uchumba wa miaka 3 hakua hivi kabisa, sijui kalogwa"

Yaani bro/cousin huwa haelewi haelewi siku hizi mkewe kawaje..!!!

Kabla hujawaoa wanakua understanding balaaa, OA SASA UONE...!!!
Think about living a happy life thats all.
Yap the goal is not money, the goal is HAPPY LIFE.

And with money happy life is reachable.!!!

#YNAA
 
kuipaka tope taasisi ya ndoa kisa mwanamke mmoja ni ujinga..
Mwamba siku hizi watu kulalamikia ndoa limekua jambo la kawaida.
Makazini wanalalamika.
Mtaani wanalalamika.

Siku hizi raia wanalalamika sanaa na ndoa zao.

Wapo wanaoishi kama misukule kwenye ndoa zao, ukiwauliza kwanini, eti kisa ""watoto wataishije tukiachana?""

Juzi nilipanda Costa umbali la Km 100, siti ya nyuma alikaa mmama, huyo mmama kuanzia safari inaanza mpaka inaisha ye anamuhadithia mwenzio jinsi mumewe anavyo chepuka na kumfanyia mambo ya ajabu kwenye ndoa yao.

Nikajiuliza "Huyu talaka haijui?""
Hata chuo wanafunzi wanadisco, je tusisome?

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
If you can't stand the heat, stay away from the kitchen.

#YNWA
 
Jamaa hakuwa amepata mke alikuwa amepata shetani na muuaji wake upo mkono wa huyo mwanamke katika kifo chake RIP DAVE
 
Sku hizi watu pia wanalalamika hela hamna ila huwaoni wakiacha kuhasso

sku hizi watu wanalalamika kwenda chuo imekua fashion, wanafunzi wanaishia kuuza sura tu.. ila huoni watu wakiacha kusoma


siku hizi watu wanalalamika mabando hayakai, ila huoni watu wakiacha kununua MB

siku hizi mashoga wamekua wengi, ila huoni mzazi akitamani mtoto wake awe mchicha mwiba

Ukiishi kwa hizo kauli zako za siku hizi hutafanya jambo.

Na pia ndoa sio mbaya ila zina joto lake.. sasa kama ulivosema, "if you cant stand the heat stay away from the kitchen"

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…