Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Rafiki yangu wa ukubwani kafariki kisa ndoa

Mimi naombeni mnisaidie kujua hili swala

Hivi mimi nikioa saiv na huyo mwanamke akanikuta nimali zangu za kutosha ambazo nimezipat kabla yakuwa nae
Je tukiachana hizo mali tutazigawana wote japo nilitafut pekee yangu.
Issue ni child support wakati huna kipato kizuri. i.e. Huna ajira wala biashara.
Inabidi uuze vitu ili utoe huduma kwa watoto wako.
 
Angelipa kisasi angekua na amani na wala asingekua na huo ugonjwa wa akili.
Mtu kakufanyia unyama namna hiyo na bado wewe tena ndio uteseke yeye akila raha kwa pesa zako. Mpe pigo tuu hamna namna .
 
Kwani nani alikudanganya ku sex kuna hitaji ndoa, unaelewa maana ya ndoa?

Kwako wewe ndoa ni sex?

Msaidizi ndio nini? na msaidizi kwani ni lazima awe mke?

Siku zote unashauriwa kutokua muoga kufanya jambo kwa kufikiria negatively effect, yani uoga wa kuumwa ndio unifanye nioe kwa kuhofia naweza nikatingwa usiku nikiwa peke yangu?

Labda nikuulize kipindi ambacho uko single uliwezaje kuishi bila uoga wa kuumwa? Au we mwenzangu baada ya kuhitimu masomo ukiwa chini ya wazazi ukapa mke ukiwa hapo hapo kwenu hujawahi ishi maisha ya geto?

Katika hustling basi we ni coward, kwasababu kuna muda mwanaume unaweza ukaenda bush mbali na makazi ya watu kuweka kambi, huko ukakaa miezi kadhaa una fight ukiwa umezungukwa na wanyama wakali.

Matatizo hayachagua pakukukuta, sehemu yeyote unaweza kupatwa na tatizo na watu waliokuzunguka wakawa helpless. Majuzi nilishuhudia ajali bajaji ilifinywa na gari kubwa, nilitegemea wingi wa watu eneo lile wawe msaada lakini huwezi amini watu walikua wanashangaa na kusema "mungu wangu sijui watapona"
Una umri gani mkuu? Isije ikawa nabishana na watoto wa chuo mwaka wa kwanza.
 
Alijikuta mahaba Niue, akabadilisha documents zotee sababu ya mbunye tu so called NDOA.

Angekua kauzu kama Mimi muda huu angekua kwenye gari yake anaenda kula bata mjini.

F*ck so called NDOA.

#YNWA
Kwahiyo umeogopa kuoa?
 
Una umri gani mkuu? Isije ikawa nabishana na watoto wa chuo mwaka wa kwanza.
umri wa kutosha kuweza kuyajua mambo mengi na ya msingi, pengine hili swala ningeongea na baba yako angenielewa vyema

Angekushangaa kuona mtoto wake anaoa mke kama backup ya yeye kuendelea kuwa salama akitingwa usiku
 
Wajumbeeeeeee...

SIKIA hiiii......

Mwaka 2012 nilikutana na Dav (sio jina lake halisi) akiwa mkuu wa kitengo fulani ofisi kubwaa Morogoro.

Kipindi hicho mi nilienda ofisini kwao kufanya field.
Kwasababu yeye alikua mkuu wa kitengo nilichopangiwa field then nilimkubali sanaa mwana.

Alikua mchapa kazi balaaa na mtafuta hela hasaaa.

Kitengo kiling'ara kwasababu yake.

Maisha yake binafsi yalikua mazuri huku akimiliki nyumba na gari (simply kijana mwenye chenji zake).

Field ikaisha na Mimi nikasepa.

Ila urafiki uliendeleaa then ukapotea ghafla.

Baada ya muda bila kuwasiliana siku moja (mwaka jana) ghafla nikamkuta njiani.

Alikua kachoka balaaa, halafu ANATAFUTA KAZI..!!!

Dah ikabidi nisimamishe tukituki yangu ya miguu 4 apande kwenda sehemu kuongea.

Alikua kama kachanganyikiwa.

Nikampa lunch then nikampeleka gheto.

Alikaa gheto kama wiki hivi, then akasepa Dar.

Alichonihadithia....
1. Mwaka ule wa field yangu (2012) alioa.
2. Mkewe alimkuta Dav ana nyumba, gari, mashamba na Mali kibaoo.
3. Baada ya ndoa, miaka iliyofata maisha nyumbani yalianza kuwa magumu, kampuni ilikua ya wazungu. Then mkataba uliisha, wazungu wakarudi kwao, Dav akakosa permanent income.
4. Mkewe akachepuka na kuhamia kwa jamaa mpya mazima.
5. Mkewe alipeleka kesi mahakamani kuomba talaka.
6. Huko nako Dav alichosikia, mkewe alitembeza mbunye na pesa mpaka talaka ikatolewa.
7. Ilibidi gari na mashamba yauzwe iliwagawane na ndoa ivunjwe..!!!

Nikashangaa....

""Mbona hizi Mali ulizipata kabla ya ndoa??""

Alinijibu "hata sijui nini kilifanyika, na vile kuokoa watoto wangu (wawili) ilibidi nikubali liuzwe gari na mashamba ndio tugawane halafu nyumba abaki nayo akae na watoto"

Mwana alikua kama kachanganyikiwa.

Tuliongee akasema anaenda Dar kutafuta ajira na anashukia kwa Steve (sio jina lake halisi).

By accident Steve namjua sanaa (classmate).

Then siku ilivyofika nikampeleka stend akapanda ndinga huyoo Dar.

Yote haya yalitokea February/2021.

Leo yaani alifajiri hii napata taarifa kuwa "Davi kafariki kwasababu ya ugonjwa wa akili"

Steve anasema......
1. Dav alikuwa mwana Sana, tulicheza na kukua wotee kitaa
2. Kwasababu tupo field moja ya Kazi then tuliunda kama team ya kusaidiana kimawazo ya fani yenu.
3. Kila jambo, liwe jipya au gumu tunashirikishana.
4. Ila tokea aoe na kuanza matatizo ya ndoa performance ilishuka.
5. Kazi zikaisha
6. Mali zake zikauzwa
7. Alivyofika Dar alikua kama chizi, kutwa kuwataja wanae, mara aropoke majina ya mkewe kwa hasira na vitu kama hivyo.
8. Tarehe 01/08 hali ilikua mbaya hasa, akakimbizwa hospital.
9. Na leo 07/08/2021 Dav KAFARIKI kwasababu ya matatizo ya akili.

Dah....
1. Watoto wawili hawana baba Tena.
2. Kuna wazazi wamepoteza mpendwa wao mtoto wa kiume PEKEE.
3. Kuna sisi tumepoteza role model wa Kazi na rafiki.
4. Tasinia yetu ya science imepoteza MTALAAMU.
5. Tanzania imepungukiwa na GDP

Yoteee haya eti kisa mbunye..!!!
1. We unadhani angeamua kuwa single kama Mimi ANGEKUFA na NDOA?
2. We unadhani angeamua kum-HIT AND RUN huyo mkewe YANGETOKEA HAYA?
3. We unadhani ...........

Alidhani kuoa ni kuzuri KUMBE KUMEMTAFUTIA KIFO MAPEMA AKIWA NA MIAKA 39 tuuu.

Tafuta hela kijana kuoa ni upuuzi kwa dunia ya sasa.

Hawataki penzi lako ila WANATAKA HIZO MALI ZAKO.

They are GOLD DIGGERS, they need kuchimba dhahabu yotee kutoka kwenye huo mgodi wako then wauache empty.

Leo nipo gheto kusikiliza nyimbo alizozipenda Dav tuu...

RIP BROTHER.

""If you think money can't buy happiness, nenda kaulize ajira mpya walimu wiki hii walivyolipwa HELA ZAO KUJIKIMU na Halmashauri zao WALIJISIKIAJE""

View attachment 1883485

View attachment 1883489

Tafuta HELA kijana.

#YNWA
Pumba tupu.
 
Usioe uishi milele.

Matukio ya vifo sababu ya ndoa miaka ya nyuma labda usikie mke kamchukua mume msukule au kapewa sumu. Wanaume walikuwa majasiri.

Sasa hivi wanaume wanaendesha ndoa zao kwa kutumia Moyo kama wanawake. Hofu ya kugongewa kila kona.
Siku hizi kugongewa /kugonga imekuwa rahisi sana, technologia inakuja na mengi, wajukuu wetu wataweza ku adapt, siyo sisi
 
Back
Top Bottom