Rafiki yangu yuko njia panda

Rafiki yangu yuko njia panda

Ukiona ndugu wanakulazimisha uoe mwanamke wanao mtaka wao kataa kwani huo ni mtego alafu kaa na mwanamke unaye mjua udhaifu wake usiende kuokotewa mwanamke na ndugu shauri yako mjinga hashauriwi huyo mwanamke anayekunywa pombe endelea nae na wewe anza kunywa kidogo kidogo kumpa kampani atakupenda kichizi ataacha pombe stress zake zikiisha.

Kwanza mwanaume gani hunywi pombe yani hata bia moja tuu. Hizo ela unatafuta za nini
 
Nina rafiki yangu yeye amekuja kuniomba ushauri, iko hivi;

Yeye (rafiki yangu) aliamua kuondoka kwenda mkoa x kujitafuta baada ya kumaliza kidato cha nne na kukaa mtaani kwao bila muelekeo wowote.

Anasema Mungu si Athumani alipofika huko alijichanganya na kufanya shugli mbali mbali akafanikiwa kufungua kigoli (biashara) x, na katika mihangaiko hiyo alikujaga kupendana na mwanamke mmoja ambae ni single mother wa mtoto mmoja na wame hustle wote kwa muda wa miaka mitatu.

Wwaliamua kuishi pamoja ili kupunguza bajeti ya kila mtu kupanga chumba chake, ingawa hajawahi kwenda kujitambulisha kwao na mwanamke pamoja na mwenzake kumsumbua kuhusu hilo.

Jamaa anadai huyo mwanamke yuko vizuri na anampenda kwa sababu wamekuwa wanasaidiana na kuvumiliana kwa vingi isipokuwa huyo mwanamke amekuwa na tabia ya kutumia pombe na jamaa hapendi na amekwisha muonya na kumshauri aache lakini mwanamke hasikii, na jamaa anashindwa kumpiga chini kwasababu mwanamke anampenda sana na wamesota sana mpaka jamaa kusimama kiuchumi si haba.

Sasa issue imekuja baada ya jamaa majuzi kutembelea nyumbani kwa wazazi wake anadai wamemsakama sana kuhusu kuoa wanadai amekuwa sasa, na amewaficha kama anaishi na mwanamke kwasababu anahisi hatoweza kutimiza ahadi za kumuoa kwa sababu kadhaa pamoja na hilo la pombe. Kibaya zaidi wameamua kumtafutia mchumba kabisa anadai ni kabinti kazuri tuu.

Sasa anaomba ushauri, atumie njia gani yakumuacha huyo mwanamke bila kumsababishia maumivu?

Najua kuna watu humu wameshawahi kuyapitia haya.

Karibuni kwa maoni yenu.
Kibaya zaidi wameamua kumtafutia mchumba kabisa anadai ni kabinti kazuri tuu.

Bila ubishi Hii story ni yako mwenyewe,
 
Kwahiyo single mother ana handicap ya (1) au (+1.5), ili jamaa ashinde inabidi afunge goli na mwishoe iwe full time (2-1)...hapendi mnywa pombe Kwanini asiwe direct Ili baadae asije akarudi tena kuomba ushauri. Mambo ya kutoambiana ukweli ndiyo hufelisha mambo.
 
Asimuache mnywa pombe aisee bali amtafutie dawa tu anaacha mazima uzuri zipo na watu wameacha na tunaish nao mitaan kwasabab haya mambo ya utafutaj kipato yana mambo mengi sana unaweza kumuacha mtu mmesota nae kumbe uwepo wake kwako ndio sabab ya maendeleo unayoyaona leo ukaja jikabidh kwa kabint kana laana za ukoo huko maisha yako yakarud ya enzi za mwalimu kisa tu wazaz wamesema jamaa yako akumbuke walipotoka na chapombe wake akitafakar jibu atakuwa nalo na kama atahitaj dawa ya mtu wake kuacha anicheki akipenda
 
Back
Top Bottom