Raha na utamu wa kula samaki aina ya Pweza iko wapi?

Raha na utamu wa kula samaki aina ya Pweza iko wapi?

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Hii inawahusu sana Wanaume wa Pwani hasa wale wa Daslam!

Kweli unaweza ukatoka nyumbani kwako ukaenda kununua Pweza na kumla kweli?

Tena kuna wengine wanapeleka zawadi mpaka nyumbani kwao watoto nao wale!

Pweza ana sura mbaya ya hovyo kabisa lakini kuna binadamu wanamla na wanashushia na beer kabisa na tuchumvi kidogo!

Watu wakapime mkojo aisee!
 
Mimi sili pweza sijawahi hata kujaribu ila mleta mada nimeshangaa kwa thread yako. Mtu kununua pweza akapeleka nyumbani kuna ajabu gani si sawa na kununua nyama tu.
Walaji wanasema mtamu sasa sijui wewe unakereka nini
 
Hahahaa. Sidhani kama watakuelewa hasa wale unaowakuta wamemzunguka huyo muuza pweza huku wana vijiti wakila na kumwambia muuzaji ahesabu vipande wanavyokula.

Ila nasikia ana faida mwilini huenda ndio chanzo cha kupendwa mbali na muonekano mbaya alio nao.
 
Kitu kama hupendi wewe acha wanaotumia wajivinjari!
Inaonekana umetokea mkoani huko kuja kula Pasaka unaanza kujifanya unajua mambo ya pwani!
 
Kama kitu hujazoe au upatikanaji wake kwenye jamii ilio kuzunguka huwezi ona raha yake. Mimi Sato, Sangara huwa sioni utamu kabisa nakula inapoteka tu.
 
Nasikia walaji wakidai anavyo virutubisho adimu ambavyo ukila huwezikuulizia vumbi la mkongo.
Anasura mbaya lakini vitamu vingi sura yake huwa haivumiliki
 
Nasikia walaji wakidai anavyo virutubisho adimu ambavyo ukila huwezikuulizia vumbi la mkongo.
Anasura mbaya lakini vitamu vingi sura yake huwa haivumiliki
Hahaaaa hapo kwenye vumbi aiseee hii kitu maridadi sana
 
Hujawahi mla..waache wenye kumla wajue utamu wake
 
Hahahaa. Sidhani kama watakuelewa hasa wale unaowakuta wamemzunguka huyo muuza pweza huku wana vijiti wakila na kumwambia muuzaji ahesabu vipande wanavyokula.

Ila nasikia ana faida mwilini huenda ndio chanzo cha kupendwa mbali na muonekano mbaya alio nao.
Hadi uwe mtu wa pwani...wengine hadi wasimuliwe.
 
Kwan unakula sura ama unakula nyama....?
Hii inawahusu sana Wanaume wa Pwani hasa wale wa Daslam!

Kweli unaweza ukatoka nyumbani kwako ukaenda kununua Pweza na kumla kweli?

Tena kuna wengine wanapeleka zawadi mpaka nyumbani kwao watoto nao wale!

Pweza ana sura mbaya ya hovyo kabisa lakini kuna binadamu wanamla na wanashushia na beer kabisa na tuchumvi kidogo!

Watu wakapime mkojo aisee!
 
Hivi mleta mada, unazungumziaje chakula kwa kukipima kwa sura?
Pweza ana sura gani mbaya ya kuchukiza?
Pweza kwa sura unaweza kumshindanisha na nguruwe?
Lakini nguruwe watu "wanamshindia" tena na kunywa supu yake ya pua na makongoro
 
Back
Top Bottom