Raha ya kuwa na tume huru ya uchaguzi hakuna mwenye uhakika wa kushinda watu wanamenyana kweli kweli

Nimeshangaa kuona wakenya waishio tz wanapiga kura,ila sisi ukitoka ulipojiandikishia tu huna chako! Ama kweli tunayo safari ndefu!
 
Tanzania tutailaumu tume ya uchaguzi bure tu. Tatizo unajiuliza nimkatae mgombea wa CCM nimpe nani ? Jibu linakuja hakuna. Maana upinzani wa nchi hii hata haueleweki. CCM itaongoza mpaka ichoke yenyewe
 
Unajidanganya mkuu.

Pale wote wanajua anayeshinda nani.

Kauli ya Rais ni kama amri na Tayari ameshachagua upande sasa sijui unadhani mshindi hafahamiki tayari.
Kauli Rais ni Amri Tanzania sio Kenya. Wenzetu Mahakama ilizuia mchakato wa BBI kwamba haukufuata utaratibu japokuwa Rais ndo aliuanzisha. Sisi huku jambo akianzisha Rais tu polisi wanaanza kusimamia utazani ni sheria. Huu ujinga upo TZ tu.
 
Unajidanganya mkuu.

Pale wote wanajua anayeshinda nani.

Kauli ya Rais ni kama amri na Tayari ameshachagua upande sasa sijui unadhani mshindi hafahamiki tayari.
Ujinga huu umebaki Tanganyika tu, nchi huongozwa kwa katiba sio kauli.
 
Tanzania Chama Tawala ni kimoja tu
Hapa hakiongelewi chama kimoja, kinaongelewa USHINDANI wa vyama. Kule Kenya hatusikii kupita bila kupingwa, mawakala wa vyama kuzuiliwa, masanduku ya kura bandia, Polisi kujazana kwenye vituo vya kupigia kura kuisaidia forgery, waandishi wa habari huko wapo vituoni na wanaruhusiwa kupiga picha zoezi la kuhesabu kura linavyokwenda, kila kitu kiko wazi. Sasa Wewe unaleta hoja ya Chama tawala una maana gani?
 
Watu wa tume huku wote ni wa chama fulani
Uchaguz hauna hata mvuto
Ndomana kupiga kura ni kupoteza muda tu

Ova
 
1. umeangalia kwenye katiba ya kenya ukaona mgombea uraisi anaruhusiwa kupiga kampeni miaka miwili + kabla ya uchaguzi?
2. Kwa mtazamo wangu tume hiyo imefeli kwani imeshindwa kuhamasisha watu umuhimu wa kupiga kura. Umeona lini Nairobi waliopiga ni kwenye 10% ya walio jiandikisha na kuna jimbo waliopiga kura sijui ni 5%. kwa kweli hii ni aibu kwa demokrasia!
3. Kwa Nchi yenye ukabila kama hiyo; tume imeacha kila chombo kitangaze matokeo kwa vile kinavyo ona; kama sio bomu inatengeneza?
 
Ndio unataka kulinganisha na utopolo upi?
 
Unaonaje hiyo wanasema ukweli sasa je ile kamati ya ccm mnayoita tume ya uchaguzi ambayo wanapojitokeza wapiga kura 5,000 wanaongeza tena sifuri na kusema waliopiga kura walikuwa 50,000 na mgombea wa chama tawala aliyepita bila kupingwa amepata kura 49,500 na kura 500 zimeharibika.

Ebu Tanzania tusione aibu tujifunze kutoka kwa wenzetu wanaojua nini maana ya uchaguzi. Hatujaona internet ikifungwa wala hatujaona ofisi za vyama vikivamiwa na watu wa usalama na mapolisi na polisi hawahusiki kabisa na maswala ya uchaguzi wakati Tanzania kila RPC anafahamu nani atakuwa mbunge katika majimbo yote ya uchaguzi katika mkoa wake hata madiwani pia anawafahamu hata kabla ya tarehe ya uchaguzi.

Hatukuona pia wabunge wala madiwani wa vyama vya upinzani wakienguliwa ili wa chama tawala wapite bila kupingwa.

Tanzania bado sana, tutakuja kuwa na uchaguzi pale ccm watakapoondolewa madarakani ila kwa sasa tutaendelea kuwa na akina Uganda, Rwanda na Burundi kuendelea kufanya uhuni huku tukiuita 'uchaguzi'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…