Kuna kitu kinaitwa mazoea. Ngoja nikumegee sehemu ya siri yangu, naweza kuonekana wa maajabu kidogo ila ndivyo nilivyo. Binafsi nikifuga nywele huwa naziwekea " record " labda nimekaa mwaka 1 na miezi 5 pasipo kunyoa zaidi ya kuchonga tu. Hiyo kwangu mimi ni " record " na huwa naitunza, kinachofuta ni namna ya kuivunja hiyo "record". Kwa hiyo, nanyoa nywele zote nabakisha za "brush" tu naanza tena safari nyengine.
Kwa mantiki ya hapo juu, ukinyoa nywele ambazo umekaa nazo kwa takribani mwaka 1 watu lazima watakuona kama kituko tu. Ila baadae watakuzoea na lile jina ulilikuwa unaitwa la HB linarudi tena.
Wakati mwengine ni vizuri kuusikiliza moyo wako na kufanya kile unachopenda maadam hakina madhara.