Habari za asubuhi wana MMU.
Nafikiri hili ni suala linalozua gumzo sana, hasa hivi karibuni kwenye hiki kizazi chetu cha dijitali ambapo wanawake pia hawapo nyuma kwa kutaka kufanya mambo yanayofanywa na wanaume pia.
Kwa hali hiyo basi siku hizi hata baadhi ya wadada hawaoni hatari kumtongoza mwanaume wanayeona anawasumbua akili yao, wengine wanamwambia moja kwa moja, wengine wanatumia mitego mbalimbali mpaka mwanaume anajikuta kaingia laini, wengine wanatumia marafiki wa karibu kufikisha ujumbe kwa mwanume husika yaani la msingi ujumbe umfikie mhusika.
Lakini jambo hili limekuwa na uvutano kwa pande zote mbili yaani me na ke,wapo wanaoona ni sawa tu kwa ke kumtongoza me na wapo wanaolipinga hilo kwa nguvu zao zote.
Kwa mtoto wa kike kumtongoza mwanaume kuna hasara kama tatu hivi ninazozijua mimi:
1.Wanaume wengi hulichukulia hili kama ishara ya kukosa aibu ya kike na hivyo kumchukulia mwanamke huyo kama kicheche.
2.Wanaume wengi wakiingia kwenye ndoa na wanawake waliowatongoza,mwanamke anakuwa hana sauti,wala hawezi hata kumtisha mwanaume kuwa anaondoka na kumwacha,majibu yao huwa hivi ``we nenda tu kwanza sikukupenda wewe ndio ulinilazimisha/ulinitongoza, kwa hiyo hata muda wa kukubembeleza anakuwa hana na hata akikubembeleza huwa ni kidogo sana na majibu ya kukatisha tamaa hufuata akiona umeshikilia msimamo wako.
3.Wanaume wengi huwa na huruma kuelekea wanawake na hivyo kujikuta wakiwakubalia ombi lao hata ikiwa kwa kweli hawajavutiwa nao au kuwapenda na yote hii hutokana na huruma ya kuwakatalia, na hilo hutokeza mume kuingia kwenye ndoa bila kuwa na lepe la upendo kwa mkewe? Unajua ndoa isiyo na lepe la upendo kwa upande mmoja ikoje? Simuliwa tu wala usiombe yakukute.
Kwa binafsi yangu nafikiri raha na haiba ya mtoto wa kike kutongozwa banah,mwanaume akuhangaikie,akubembeleze,akupigie misele mpaka akupate au mnasemaje wadada?
Na kwa wanaume mnasemaje?Mnaonaje mdada anapokusarandia ili uwe wake? Ungependa utongozwe au wewe ndo utongoze? Ni fahari kwako kutongozwa au kutongoza? Ukitongozwa na ke unajionaje/jihisije?
Wana MMU hayo ni maneno yangu tu na maoni yangu tu ambayo wala si sheria kwa hiyo karibuni wote tutoe maoni yetu kuhusu suala hili.
=========
View attachment 1370059
Kutongoza ni kitendo cha mtu kumshawishi mwingine au kueleza hisia zake za kimapenzi kwa mtu anaempenda au kumuhitaji kimapenzi ili waweze kuanzisha mahusiano ya kimapenzi.
Kwa upande wa wanaume wao kutongoza ni jambo la kawaida kabisa na limekuwepo tangu enzi hivyo haitashangaza dunia kuona mwanaume anamtongoza mwanamke, ila ni jambo la fedheha pale mwanaume anaposhindwa au kukosa ujasiri wa kumtongoza mwanamke anaemtaka au kumpenda.
Zifuatazo ni njia zinazoweza kuwasaidia wale wasioweza kutongoza
1. Kuwa na sababa za uhakika
Kabla ya kuanza chochote, inafaa kujiuliza kwa nini unataka kumtongoza huyo mwanamke /mwanaume. Najua hautaki kumtongoza kwa sababu ya muonekano wake ama kwa sababu unataka kujionyesha kuwa wewe ni bingwa wa kutongoza zaidi, maana yake ukifanya hivyo utakuwa umejidhalilisha mwenyewe. Pia usijaribu kutongoza ili kumuonyesha mpenzi wako wa zamani kuwa hatoshi mboga.
Pili unafaa kufahamu japo kidogo tabia ya mtu unaye mtongoza, yaani kuyajua maisha yake, vitu anavyovipenda, na pia je mkiwa pamoja mnaweza kuunganika. Ukihakikisha kuwa sababu zote unazo za kumtongoza mwanamke huyu, basi sasa unafaa kuruka kwa step ya pili.
2. Kuwa mtu unaejiheshimu mbele za watu
Ni lazima utumie ujanja wa kuwa mnyenyekevu kwa kila mmoja. Usiwe mtu ambaye unaropoka na kutusiana na watu ovyo ovyo. Inafaa ujaribu kadri uwezavyo kuheshimu kila mtu. Hii itamfanya mtu unaemtaka kuona kuwa wewe unadalili za kuwa mpenzi au mchumba bora zaidi kwake.
3. Kuwa mcheshi
Wanawake na wanaume hupenda watu wacheshi, yaani mtu ambaye anaweza kumfurahisha na kujisikia ana furaha wakati wote.
Najua kwa upande wa wanaume wapo ambao ni vigumu wao kumchekesha mtu lakini hiyo si sababu ya kuwa hautakuwa na nafasi ya kumpata mwanamke wa ndoto zako.
Hakikisha hata kama ni mara moja unahifadhi baadhi ya vitu ambavyo kwa hakika vitachekesha. Na amini usiamini, wakati ambapo utakuwa ukimfurahisha, itakuwa rahisi kwako kuwa na nafasi rahisi ya kuuteka moyo wake.
4. Kuwa karibu naye
Hapa simaanishi kuwa kila mahali atakapokuwa unamfuata nyuma nyuma, la. Kile ambacho namaanisha hapa ni kuwa uhakikishe kuwa atleast una company na yeye. Hii inaweza kufanikishwa kiurahisi kama wewe ni rafiki wa rafiki yake.
Unaweza kuitisha kikao na rafiki yako halafu umwambie amkaribishe rafiki yake (huyo mnayemzimia). Hapo itakuwa rahisi kwako kueneza mbinu ya 3 hapo juu kwa urahisi.
Onyo: Usianze kumtongoza papo kwa papo...anza na kumfanya akuzoee halafu mengine yatakuja baadae.
5. Kujiamini
Kujiamini ni lazima bila kujiamini huwezi kufanikiwa... Wewe unatakiwa kumchukulia kama binadamu wa kawaida japo unampenda ili uwe na ujasiri mbele yake inabidi umuone wa kawaida sawa na watu wengine. Ukishafanya hivyo, itakuwa rahisi kwako kwani utakuwa umejitenga na wale wengine wanaompenda ila ni waoga hivyo kujipunguzia mashindano.
6. Muonyeshe uzuri wako
Hapa lazima umuonyeshe talanta yako yeyote ambayo unayo. Aidha unaweza kuwa unakipawa cha kuimba, kuchora, kudensi, kubenjua maungo nk. Ooo utajiuliza kwa nini unafaa umuonyeshe talanta yako.
Jibu ni rahisi wewe hautakuwa peke yako kumtamani ama kumtongoza, so lazima uje na kitu ambacho kitakutofautisha na wengine ili asikusahau. Ukimwonyesha kipawa chako labda anaweza kukukubali na akapenda mambo yako na kumfanya kutamani kuwa na wewe mara kwa mara.
7. Tafuta udhaifu wake
Kila mtu anaudhaifu wake katika vitu na mambo tofauti tofauti. Hakikisha umejua udhaifu wake vizuri. Kama anampenda mwanamziki flani, sehemu fulani ama chochote kile, hakikisha umejipatia nafasi ya utafiti ili wakati mwingine utakapokutana na yeye unazua stori kuhusu jambo analolipenda.
Atachangia na wewe ujazie. Hii itakufanya wewe kuweza kukupenda kwani ataona kuwa kuna mfanano kati yenu kwa vitu mnavyopenda.
8. Makinika na akili yake na wala si muonekano wake
Kile ambacho unachohitaji kushungulikia zaidi ni kumsifu kwa mambo ambayo anayoyafanya na kupitia akilini mwake. Baada ya kuongea na yeye katika maongezi tofauti tofauti, atakufungulia moyo wake kwa urahisi ambapo hapo utatumia nafasi kumjua kiundani kumhusu. Akitaja kitu ambacho kimekupendeza unaweza kutumia nafasi hio ya kumsifu na kumwambia kuwa umependezwa sana kwa kutaja au kugusia swala fulani.
9. Jaribu kuja na kitu tofauti
Kama imetimia ule muda wako ambao unaona kuwa umefikia level ya kumfungilia moyo wako na kumwambia kuwa unampenda, jaribu kufanya kitu tofauti ambacho hajawahi kufanyiwa na yeyote.
Usijaribu kumpelekea maua kwani hio inaweza kuwa si mara yake ya kwanza kupokea maua so kama ni wewe ungefanya uchunguzi na kitu ambacho bado unaona hajawahi kuletewa so ukifanikiwa kumsaprize vizuri, una nafasi kuu ya wewe kufanikiwa kumpata yule aliye ndotoni.
Ukitumia ujanja ambao ni tofauti na watu wengine una nafasi kubwa ya kufaulu. Kutumia ujanja wako vizuri na kujiamini ni kama mkuki kwa unaemtaka, ukiurusha haukosi kutoboa.
Michango ya wadau:
----
----
----