Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 12,297
- 18,156
Hili jambo ni changamoto kuu,Watanzania wenzangu ngoja niwakumbushe ukweli ambao nadhani kila mtu anaujua: Viongozi wa nchi ni reflection ya ya wananchi. Na hapa sizungumzii tu kuwa ''kwa kuwa viongozi wanatoka kwenye jamii, basi ni ''sample'' ya jamii. Hoja yangu ni hii.
Viongozi wa nchi utendaji wao wa kila siku ''hutengenezwa'' na tabia ya wananchi. Yaani viongozi wakifanya boko na wananchi wakikubali na kukaa kimya, basi hujijenga na kuwa tabia ya viongozi wote. NI kama ule msemo usemao kuwa ''ukali wa mbwa, hutegemea msasi (mwindaji). Mwidaji akiwa moto, na mbwa wake nao wanakuwa moto.
Sasa tatizo letu watanzania nikudhani kuwa viongozi wazuri hushuka kutoka mbinguni. Yes, unaweza kupata bahati ya kuwa na kiongozi mmoja au wawili wazuri, lakini kanuni ni kwamba tabia na utendaji wa viongozi hutegemea sana ''ukali'' wa wananchi.
Msidhani nchi zilizoendelea zilipata maendeleo kwa sababu tu Mungu aliwashushia viongozi hodari hapana. Maendeleo na uongozi bora ulitokana na wananchi kujitambua na kuwa wakali na tayari kuhoji pale viongozi wanapoharibu.
Na sehemu ya haraka ya kuanzia ni kwa madiwani na wenyeviti