Rai kwa vyama vya upinzani Tanzania: Daini Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2020!

Hutakaa usikie wapinzani wakienda mahakamani kudai mambo ya msingi kikatiba wala kuitisha maandamano ya mambo ya msingi kama tume huru na katiba mpya. Tatizo sisi mashabiki ndio tunaowalea. Tunawaimbia mapambio hata kwenye mambo ya kijinga.
 
Hutakaa usikie wapinzani wakienda mahakamani kudai mambo ya msingi kikatiba wala kuitisha maandamano ya mambo ya msingi kama tume huru na katiba mpya. Tatizo sisi mashabiki ndio tunaowalea. Tunawaimbia mapambio hata kwenye mambo ya kijinga.
Ndugu yangu unafikiri kuna Chama cha Upinzani chenye lengo la kwenda Ikulu? Mnapoteza bure kura zenu! Wapinzani hawana lengo hilo!!
 
ACT wazalendo wameanza kazi hii kwa kutaka kufufuliwa kwa mchakato wa katiba mpya...ambayo ina kipengele cha tume huru ya uchaguzi.

Kwa kuwa chama chenyewe ni kidogo basi hata hoja zao hazina nguvu.
 
Unataka wasuse, kwani hawana macho! Unadhani hawakuona kilichotokea ZnZ.
 
Haya wasisusie...ila ndo hivo daima wataendelea kuwa wasindikizaji wa CCM huko ikulu na bungeni.
 
Ebana eeh umesema ukweli ulio mchungu mno.

Hapo kwenye viongozi wa kudumu umeua mbaya.

Na ni kweli, wanaoumiaga zaidi baada ya kushindwa ni wafuasi.

Too much truth!
Mfano hai kiduchu...

Mgombea wa UKAWA aliwaaminisha wapiga kura wake kuwa.

Pigeni kura mimi nitazilinda.

kinyume chake akaja na sababu ya kuibiwa kura na Tume ya Uchaguzi najua walioumia ni wafuasi wake.
 
Kwenye mabadiliko yeyote huwezi kuruka stage hata siku. Wakumbukeni Wakenya japo hatuombei haya mambo ila sidhani kama CCM watakubali hata kidogo.
 
Haya wasisusie...ila ndi hivo daima wataendelea kuwa wasindikizaji wa CCM huko ikulu na bungeni.
Inatakiwa watumie mbinu nyingi sana kuanzia bungeni tuoate Tume Huru ya uchaguzi then mchakayo wa Katiba moya uendelee kuanzia pale Tume ya Warioba na siyo ike katiba ya ccm the poorest constitution proposal.
Tu
 
Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco
Pasco,unaujua ukweli.Kubadilisha katiba kunahitaji kura za kutosha bungeni.Wapinzani wanazo?
 
Mfano hai kiduchu...

Mgombea wa UKAWA aliwaaminisha wapiga kura wake kuwa.

Pigeni kura mimi nitazilinda.

kinyume chake akaja na sababu ya kuibiwa kura na Tume ya Uchaguzi najua walioumia ni wafuasi wake.
Wa kuonewa huruma ni hao wafuasi wake waliomwamini kuwa atazilinda kura zao.

Naamini hao wafuasi ndo waliumia zaidi kuliko hata alivyoumia yeye [ingawa nahisi ye mwenyewe alijua hatashinda].
 
Hakuna viongozi wa upinzani wenye nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania,wote wasanii na matapeli
Rejea bandiko lako liliouliza kama kuna watu wanaendelea kuiamini chadema
 
Vyama vya upinzani vinadai kua uchaguzi wa 2015; walipata majimbo mengi kuliko chaguzi zilizopita! Si walishinda hayo majimbo kwa tume hii hii inayolalamikiwa sio huru? Au tume ilikua huru katika Yale majimbo waliyoshinda na haikua huru katika majimbo waliyoshindwa? Mfano mdogo hapo Kenya! Tume yao ni huru lakini bado kulikua na malalamiko ya Rafu mbali mbali! Binafsi naamini kua kamwe haitawahi tokea tume guru hapa duniani, maana binadamu ni hawa hawa, na daima upande ulioshindwa utakua na malalamiko! Tutapoteza muda na fedha kwa kitu ambacho hakitawahi kiwe na uhalisia!
 
Hutakaa usikie wapinzani wakienda mahakamani kudai mambo ya msingi kikatiba wala kuitisha maandamano ya mambo ya msingi kama tume huru na katiba mpya. Tatizo sisi mashabiki ndio tunaowalea. Tunawaimbia mapambio hata kwenye mambo ya kijinga.
Kwa mfano hili la tume huru watu tumelipiga kelele kabla hata ya 2010.

Na sijawahi kuona viongozi wakuu wa upinzani wakianzisha kampeni ya kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa kuwa na tume huru ya uchaguzi.

Badala yake kila chaguzi wanashiriki. Wakishindwa ndo wanaanza kugomba ati tume si huru.

Baada ya muda wanaacha kabisa hata kuyazungumzia mambo ya tume huru hadi uchaguzi unaofuata unapoisha.

Just pathetic.
 
ukawa wamekuwa na tabia ya kususia vikao vya bunge la katiba na vikao vya bunge la kawaida... lkn hamna walichopata baada ya kufanya ivyo...

wajifunze kwa cuf kule zanzibar baada ya kususa wakapoteza haki zao.

katiba iliyo pendekezwa na tume ya warioba ndio katiba huru ya wananchi.
 
Upo sahihi, ila kwenye nchi changa kama Tz ambayo elimu ya uraia, demokrasia na uzalendo vipo chini ya asilimia zero nadhani hilo tusubiri kwanza kwa sababu:
1. Tz kuna mtu/kikundi kinaweza kununua chama fulani cha upinzani
2. Tz kuna watu/chama/kikundi kinaweza kuwanunulia watu viroba na kuwaambia wadeki barabara
3. Tz kuna mtu mwenye hela anaweza kununua ajenda za wapinzani kwa bil 10 na kuwabadilisha ajenda yao
 
Naunga mkono hoja. Wapinzani wetu wako bize na mambo mengine mpaka kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 zitakapo tangazwa.
Pasco
Wakili msomi huwa unapata muda wa kuwashauri hao mabwana?
 
Hapo ndipo
Hapo ndipo wengi tunashangaa, kwenye kampeni wanatuambia ''safari hii CCM hawatoki na kura haziibiwi'', uchaguzi ukiisha wanaanza kulalamikia tume ya Uchaguzi wakimaliza wanakaa kimya tena kwa miaka mitano husikii chochote zaidi ya maandamano yasiyo na kichwa wala miguu hadi uchaguzi mwingine unafika.
 
Pasco,unaujua ukweli.Kubadilisha katiba kunahitaji kura za kutosha bungeni.Wapinzani wanazo?
Sio lazima kubadili katiba, ni kupigania mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa Tume huru yenye wajumbe wenye divedified compositions.

Wanatakiwa kupigania the level playing field,
Wenzetu Bunge likiishavunjwa mali zote za umma zinarudishwa na wagombea wote wanakiwa na equal status. Huku kwetu magari yanabadilishwa tuu number na kuwekwa za kiraia, rais anaendelea kugombea na presidential status, 2015 timu yote ya Ikulu including the press unit ilikuwa nyuma ya Magufuli na fedha za kampeni ni fedha za serikali! .

Mnagombea kisu cha makali kuwili, mwenzako ameshika mpini wewe unapewa kushika kwenye makali ukitegemea kushinda! .

Pasco
 

From the offensive to the defensive... leverage walitoa wao wenyewe
 
wapinzani wetu wanafanya mambo nusu nusu kama sio wanafanya mambo ili waonekane tu kwa muda na baada ya hapo hamna muafaka wake. ukiangalia kwa umakini mimi nilidhani jambo la kwanza kulipigania kwa awamu hii ingekua katiba mpya ile waliyokuwa wakiihitaji lakini cha kushangaza na kustajaabisha wameishia msituni sijui wameelekea wapi katika hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…