kinje ketile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 5,089
- 9,664
Hii ni Rai kwa wanywa 'thupu' Yanga kuwakemea baadhi ya Wachezaji kwani nidhamu inaonekana ni Tatizo
Hili ni angalizo La Mapema kwa Yanga. Eneo La nidhamu Limeonekana kulegalega katika Michezo ya hivi karibuni kwa baadhi ya Wachezaji wameonyesha Kiwango cha chini Sana cha Nidhamu.
Jambo hilo Limeanza kuiathiri timu katika Kiwango hata Marefa Wameshtukia nidhamu mbovu ya wachezaji na hivyo Kisaikolojia waamuzi Wanajipanga kuikabili hali hiyo ya nidhamu mbovu baadhi ya Wachezaji.
Mechi ya Yanga na Azam ni Kielelezo tosha. Mchezaji mmoja alilimwa Red kwa kuwadandia Wenzie kutokea nyuma akiamini Refa atafumba macho,haikuwa hivyo.
Kuna mwingine ni Kipa alitokea golini huku anafoka foka kufata refa, refa hakuwa na hiana akampokea kwa yellow card.Kiranga kikamuisha.
Halafu kuna yule aliyekuwa kwenye benchi nje yeye alikuwa anajifanya Kocha msaidizi wa Gamondi rusha rusha sana mikono kama Trafiki na mineno inamtoka sijui alikuwa anasema nini labda mitusi,naye akazawadiwa haki yake Ya yellow card.
Kwa kuwa Michezo sio uhasama na uadui, Michezo ni bururdani na Upendo hivyo tunawapa huu mchongo mapema mchukue tahadhari La Sivyo kiranga Chao kitawatokea puani.