Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity)

Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity)

hakuna haja ya vijana kujinasibu na usalama kwa kudhani kuwa wataonekana matawi na mpunga wa nguvu.
Kwa hili upo sahihi. Tupo pamoja. Hakuna haja ya vijana kujipa kazi ambazo sio zao kwa lengo la kutaka kupata misifa pasipo kujua kuwa wanaweza kuhatarisha maisha yao...
 
Sio sahihi kumuita mtu njaa ilhali hajawahi kuja kuomba msaada wa chakula nyumbani kwako.

Heshimu binadamu wenzako...
Samahani kama nimekukwaza mkuu.

Pengine wewe ni katika wao.

Ila sijakusudia kukejeli mkuu.

Nimekusudia kuwa vijana wasione kama kuna mambo mazuri mnooo mpaka kupata gharama ya kujifananisha nao ili jamii iwachukulie vile.

Samahani sana mkuu.

Pengine nimetumia kauli mbaya yenye lengo zuri ndani yake.
 
Pengine wewe ni katika wao.
Hapana mkuu. Mimi sio mtu wa usalama. Mimi ni kijana wa kawaida sana. Siku moja tutaonana ukipenda.

Ninakataa kumuita mtu njaa kwa sababu la kulinda hadhi na utu wa mwingine.

Sio vyema kudhalilisha kada zingine/binadamu wengine...
 
Kwa hili upo sahihi. Tupo pamoja. Hakuna haja ya vijana kujipa kazi ambazo sio zao kwa lengo la kutaka kupata misifa pasipo kujua kuwa wanaweza kuhatarisha maisha yao...
Yah mkuu.

Lengo langu sio kukejeli.

Lengo langu ni kuwaonesha vijana kuwa hii ni kazi kama kazi zingine.

Wanaojidai kuwa ni usalama wanadhani kuwa kule kuna pesa za hivi hivi tu,paaap unachukua pesa zisomana hapana.

Ile kazi ina majungu kama kazi zingine.

Ile kazi ina njaa kama kazi zingine zilivyokuwa na njaa.

Ile kazi ina fitina kama kazi zingine.

Ile kazi ina udhalili kama kazi zingine.

Ila vijana hawajinasibu na kazi zingine wanadhani kwamba kule kuna kitu kiko real special wakati sio sahihi.

Ama wanaojinasibu kwa kupenda tu ile kazi bila kujali maslahi hao watajua wenyewe.
 
Unawaita njaa tupu wakati panya road walivyoibuka mkawa mnaomba msaada wao?

Acha kukejeli kazi za watu.
Panya road iliwahi kuitiwa usalama wa taifa?
Hawa panya road si ni kitendo cha kumpa gongo mjumbe akataja wahuni wote maana wanajulikana kabisa. Kwanza askari polisi wanakuwa wapi mpaka hii kesi iwe ya usalama wa taifa.
 
Hapana mkuu. Mimi sio mtu wa usalama. Mimi ni kijana wa kawaida sana. Siku moja tutaonana ukipenda.

Ninakataa kumuita mtu njaa kwa sababu la kulinda hadhi na utu wa mwingine.

Sio vyema kudhalilisha kada zingine/binadamu wengine...
Okey mkuu.
Bila shaka umeelewa makusudio yangu.

Sikusema kudhalilisha.

Nimesema kuwafananisha na wengine ili waone kuwa ni kazi kama zingine tu.

Wala sijakusudia kukejeli mkuu
 
Upo sahihi sana mkuu.

Mimi hii trend nilianza kuiona muda mrefu sana mkuu, hususan kwa ndugu, jamaa na rafiki zangu ninaokutana nao mara kwa mara.

Unakuta mtu amenyoa kichwani kama askari (Crew Cut) kisha mustache amenyoa kama Police, alafu amechomekea mkanda nje kama boss fulani hivi na kuanza kuwadanganya watu kuwa yupo kwenye system.

Niliwahi kuwaambia kuwa hii ni hatari sana kwa maisha yao na wasidhanie kuwa ni sifa nzuri hata kidogo.
Na Mimi nitawaakumbusha huku uraiani mkuu.
 
Okey mkuu.
Bila shaka umeelewa makusudio yangu.

Sikusema kudhalilisha.

Nimesema kuwafananisha na wengine ili waone kuwa ni kazi kama zingine tu.

Wala sijakusudia kukejeli mkuu
Sawa ndugu yangu. Hii ndio maana ya kuwa na JF. Tunatofautiana kisha tunapatana na maisha yanaendelea. One love brother.
 
Mimi binafsi sipendi kufananishwa nao ila ishanitokea mtaani kwangu ninakoishi nakila ninavyo jaribu kukana ndio wadau wanazid kuamin naficha my cover sina chakufanya zaid yakoenjoy tu the benefits of an economy of the scale that comes along with the title naheshimika na vibaka na maaskari kwenye eneo langu
 
Mimi binafsi sipendi kufananishwa nao ila ishanitokea mtaani kwangu ninakoishi nakila ninavyo jaribu kukana ndio wadau wanazid kuamin naficha my cover
Ikiwezekana kawashtaki hata Police hao wanaokufananisha kuwa wanataka kuhatarisha usalama wako binafsi...
 
Panya road iliwahi kuitiwa usalama wa taifa?
Hawa panya road si ni kitendo cha kumpa gongo mjumbe akataja wahuni wote maana wanajulikana kabisa. Kwanza askari polisi wanakuwa wapi mpaka hii kesi iwe ya usalama wa taifa.

mkuu TISS ni maafisa rasmi wa kazi ya usalama,lakini meno yao yanatoka vyombo vingine.

so usishangae sana mtu anapowanasibisha na kazi zozote za kawaida za kiusalama.
 
Nasikia lisu nae alifananishwa na agent wa ..[emoji116]
JamiiForums-1722209025.jpg
 
Back
Top Bottom