Someone alinifata kukaa na mimi kwenye venue lecture ya asubuhi. Akachukua ID yangu ya chuo kasoma jina akawa na shauku, yake ilikuwa mezani nikaisoma na kupotezea. Sikuhoji lolote ila tulipomaliza akanambia mimi ni kama ndugu yake (kwa kufahamiana ndani ya 80 mins). Akanambia twende kwake nipaone, nikaenda tukakaa mpaka jioni nikarudi chuo yeye hakuhudhuria. Huyu sikuwahi muona wakati tunasoma wote na najua watu zaidi ya nusu kwa majina, sura kama 92% nawajua.
Tukafanya test two yeye hakufanya hata moja. Tukaenda kufanya UE yeye CA zote ni incomplete, kila lecturer anamtafuta. Kwa simu hapatikani kabisa. Alikuwa na mademu wengi sana chuo, nikatafuta wote ninaofahamu wakawa hawajui wala hawana contact nae.
Nikaenda kwake, kumbe hakuna anayepajua. Mademu zake hukutana uko kwingine, marafiki hana kwa kuwa si mtu wa kukaa, group discussion sijui nini hajulikani. Nikaenda kwake nikauliza jirani akasema kaja jana yake, mwenyewe akanizuia kusema kama nimemuona. Akanipa namba mpya ya simu.
Ilikuwa hivi, alikuwa first year, akapigiwa simu kesho yake aende sehemu flani. Alipofika smartphone wakachukua na kumpeleka somewhere alipokaa mpaka tunafanya test 2 na kufikia UE. Alikuwa recruited tokea JKT. Kaacha chuo yupo kwenye mafunzo yao kama si Dodoma ni Arusha.
Sijui kwa nini alinipa namba mpya maana hatukuwahi wasiliana tena. Sijui kwa nini alinipeleka kwake mimi pekee, kwangu sikutaka aje niliona ana kasi sana. Ningekuwa mwepesi nisingejua nini kinaendelea wala asingenambia. Alinambia kwa vile aliona nishatambua. Nyumbani wanajua yupo chuo, yeye hayupo na hajapewa muda wa kusitisha masomo.