Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity)

Raia Mpenda Misifa: Ukiambiwa umefanana na mtu wa usalama usifurahie. Hiyo sio sifa nzuri. Unaweza ukadhurika kwa bahati mbaya (Mistaken Identity)

Upo sahihi sana mkuu.

Mimi hii trend nilianza kuiona muda mrefu sana mkuu, hususan kwa ndugu, jamaa na rafiki zangu ninaokutana nao mara kwa mara.

Unakuta mtu amenyoa kichwani kama askari (Crew Cut) kisha mustache amenyoa kama Police, alafu amechomekea mkanda nje kama boss fulani hivi na kuanza kuwadanganya watu kuwa yupo kwenye system.

Niliwahi kuwaambia kuwa hii ni hatari sana kwa maisha yao na wasidhanie kuwa ni sifa nzuri hata kidogo.

Mtu anaweza kwenda kufanya tukioa akaanza kukuua ww akihisi ni mwanausalama kumbe no Boya flan tu
 
Someone alinifata kukaa na mimi kwenye venue lecture ya asubuhi. Akachukua ID yangu ya chuo kasoma jina akawa na shauku, yake ilikuwa mezani nikaisoma na kupotezea. Sikuhoji lolote ila tulipomaliza akanambia mimi ni kama ndugu yake (kwa kufahamiana ndani ya 80 mins). Akanambia twende kwake nipaone, nikaenda tukakaa mpaka jioni nikarudi chuo yeye hakuhudhuria. Huyu sikuwahi muona wakati tunasoma wote na najua watu zaidi ya nusu kwa majina, sura kama 92% nawajua.

Tukafanya test two yeye hakufanya hata moja. Tukaenda kufanya UE yeye CA zote ni incomplete, kila lecturer anamtafuta. Kwa simu hapatikani kabisa. Alikuwa na mademu wengi sana chuo, nikatafuta wote ninaofahamu wakawa hawajui wala hawana contact nae.

Nikaenda kwake, kumbe hakuna anayepajua. Mademu zake hukutana uko kwingine, marafiki hana kwa kuwa si mtu wa kukaa, group discussion sijui nini hajulikani. Nikaenda kwake nikauliza jirani akasema kaja jana yake, mwenyewe akanizuia kusema kama nimemuona. Akanipa namba mpya ya simu.

Ilikuwa hivi, alikuwa first year, akapigiwa simu kesho yake aende sehemu flani. Alipofika smartphone wakachukua na kumpeleka somewhere alipokaa mpaka tunafanya test 2 na kufikia UE. Alikuwa recruited tokea JKT. Kaacha chuo yupo kwenye mafunzo yao kama si Dodoma ni Arusha.

Sijui kwa nini alinipa namba mpya maana hatukuwahi wasiliana tena. Sijui kwa nini alinipeleka kwake mimi pekee, kwangu sikutaka aje niliona ana kasi sana. Ningekuwa mwepesi nisingejua nini kinaendelea wala asingenambia. Alinambia kwa vile aliona nishatambua. Nyumbani wanajua yupo chuo, yeye hayupo na hajapewa muda wa kusitisha masomo.
 
Sasa mbona hii mbinu mlikuwa hamuitumii badala yake mkawa mnaomba msaada wa Police?
Msaada uliombwa police na sio usalama wa taifa. Kwanza ofisi zao unaendaje kutoa taarifa, tena taarifa zenyewe panya road vitoto vya 17yrs venye marungu na kuiba kwenye vibanda vya chips. Kazi ya sungusungu walio organized inaweza kukamata wajinga wote hao.
 
Mtu anaweza kwenda kufanya tukioa akaanza kukuua ww akihisi ni mwanausalama kumbe no Boya flan tu
Ndio hivyo mkuu. Upo sahihi sana.

Anaweza akahisi mimi ni mwanausalama kumbe boya tu mlala hoi sina mbele wala nyuma.
 
mkuu TISS ni maafisa rasmi wa kazi ya usalama,lakini meno yao yanatoka vyombo vingine.

so usishangae sana mtu anapowanasibisha na kazi zozote za kawaida za kiusalama.
Ukiachana na Director General wa TISS, ni mfanyakazi au agent gani wa hii taasisi anajulikana in public?
Utaenda kushitaki kwa nani ambaye kavaa kiraia, au kiaskari, au kidaktari wakati anakana hiyo tittle na hawezi kuwa responsible kwa hatua unazotaka.

Uliwahi sikia mtu kaenda ofisi ya TISS kutoa malalamiko kama tunavyoenda polisi.
 
Kwani Police sio usalama wa taifa? Wao hawalilindi taifa? TISS ni idara ya ujasusi ambao ni sehemu ya usalama wa taifa...
Mimi nalilinda taifa wakati sio polisi, mgambo wala TISS.
Hii reply yako hapa inafanya uzi wote usiwe na maana. Kwamba kwenye uzi wako ulimaanisha watu wasijifanye askari polisi?

Nakufahamu kwenye nyuzi zako hutaki kukosolewa.
 
Mimi nalilinda taifa wakati sio polisi, mgambo wala TISS.
Wewe pia ni sehemu ya usalama wa taifa kwa maana ulinzi wa taifa hili ni jukumu la kila mtanzania katika nafasi aliyonayo.

Babu yangu analima mahindi kijijini Rorya ekari mpaka 30 kwa mwaka.

Yeye pia ni sehemu ya usalama wa taifa kwa maana analilinda taifa letu dhidi ya adui njaa.
 
Malalamiko yanatolewa Police kisha wao wanawasiliana na TISS pale wanapohitaji msaada wao.
Wakihitaji msaada wao wanawaita ndio lakini sio scenario ya panya road uliyosema. Polisi wana wapelelezi, mwaka jana nilikuta mtu kafa nikaita watu tukashangaa kisha akapelekwa hospitali kupimwa. Nikaenda nyumbani nikajikuta usiku watu wawili wanakuja kuchukua maelezo kwangu. Walisema wametokea Stakishari na ni askari upelelezi. Sikuhitaji ID wakachukua maelezo ambayo bahati nzuri niliyakumbuka vema kabisa wakaondoka.

Now, Stakishari si kituo cha Usalama wa Taifa wala wale watu hawakuwa TISS ila walipeleleza kesi.
Panya road sio kesi ya level za TISS.
 
Wakihitaji msaada wao wanawaita ndio lakini sio scenario ya panya road uliyosema.
Panya road ni kama mfano tu wa matukio ya kihalifu yaliyokuwa yanaendelea katika jamii yetu ya huku Dar.

Kuna ujambazi pamoja na tatizo la drugs...
 
Wewe pia ni sehemu ya usalama wa taifa kwa maana ulinzi wa taifa hili ni jukumu la kila mtanzania katika nafasi aliyonayo.

Babu yangu analima mahindi kijijini Rorya ekari mpaka 30 kwa mwaka.

Yeye pia ni sehemu ya usalama wa taifa kwa maana analilinda taifa letu dhidi ya adui njaa.
Kwa hiyo watu wa usalama wa MOSSAD uliotaja ni sawa na mkulima wa mahindi babu yako.
Sisi unataka tusijifananishe na wanausalama, yani tusijifananishe na wakulima wa mahindi kama babu yako kwa maana majambazi watatudhuru.
Bro kuwa serious na uzi wako.
 
Ukiachana na Director General wa TISS, ni mfanyakazi au agent gani wa hii taasisi anajulikana in public?
Utaenda kushitaki kwa nani ambaye kavaa kiraia, au kiaskari, au kidaktari wakati anakana hiyo tittle na hawezi kuwa responsible kwa hatua unazotaka.

Uliwahi sikia mtu kaenda ofisi ya TISS kutoa malalamiko kama tunavyoenda polisi.

mkuu mbona unaenda tu,kwa kujua au kwa kutojua na unasaidiwa vizuri tu.labda kama hujui ofisi zao ni zipi.

dso,rso wote wanafahamika mpaka wasaidizi wao,labda kama sio mtu unayejihusisha sana na michongo ya ofisi za serikali.

tofauti yao na polisi hawataact moja kwa moja kama polisi baada ya wewe kulalamikia swala fulani,watakusaidia kufika kwa wahusika,au wakupeleke kabisa.
 
mwaka jana nilikuta mtu kafa nikaita watu tukashangaa kisha akapelekwa hospitali kupimwa. Nikaenda nyumbani nikajikuta usiku watu wawili wanakuja kuchukua maelezo kwangu. Walisema wametokea Stakishari na ni askari upelelezi. Sikuhitaji ID wakachukua maelezo ambayo bahati nzuri niliyakumbuka vema kabisa wakaondoka.
Pole sana kwa mkasa ndugu yangu.

Pia hongera kwa kuwa raia mwema na kukubali kushirikiana na Police kwa manufaa ya jamii nzima...
 
Back
Top Bottom