Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Jamani nimesikitika kwa kweli hakukuwa na sababu ya kumpiga kiasi hicho, mbona alianza tu kusogea mwenyewe, mtu amejitokeza kwa mapenzi mema amuage Marehemu anaishia kurudi nyumbani na ngeu khaaa mpaka hata huyo mwenzie hapo kamshangaa. Huyu mlinzi mwendawazimu kweli achukuliwe hatua
 
Aiseee
 
Inauma sana,kulikuwa na haja gani ya kumpiga? Je sheria inasemaje,anaweza kumshitaki kwa kumshambulia? Au wao walinda amani wana certificate ya kutushambulia raia?
Mkuu, ukisema kampiga unapunguza uzito,amemtwanga ngumi nzito sana! Ile ni ngumi unayopigwa ili ama ufe kabisa au ufe kwa muda mfupi.

Bado hadi sasa najiuliza kama huyu mlinzi alikuwa sawa kiakili au ni mambo ya pombe.
 
.kama kweli tuko makini huyu jamaa lazima achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu kulikuwa hakuna sababu yoyote ya yule mlinzi kumshambulia yule muombolezaji mimi niko tayari hata kuchangia gharama za kesi.
 
Kesi bongo,we changa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…