Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Jamani nimesikitika kwa kweli hakukuwa na sababu ya kumpiga kiasi hicho, mbona alianza tu kusogea mwenyewe, mtu amejitokeza kwa mapenzi mema amuage Marehemu anaishia kurudi nyumbani na ngeu khaaa mpaka hata huyo mwenzie hapo kamshangaa. Huyu mlinzi mwendawazimu kweli achukuliwe hatua
 
Kipindi cha jiwe msafara wake ilikuwa mara ya mwisho kupita geita, sasa zile escorts kabla yeye hajapita ilipita cruiser v8 ya wanajeshi ikamfata boda alikuwa anaendesha pembeni ya barabara ikampa kitu, kisha wakashuka kumtizama amesharest in peace walichofanya wakamwita polisi trafic alikuwa pembeni wakamwambia ita gari uondoe huu mzoga, kisha wao wakatoa kipande cha bumper ya mbele kilikuwa kimekatika wakakitupa pembeni ya barabara, kisha hao wakasepa
Aiseee
 
Inauma sana,kulikuwa na haja gani ya kumpiga? Je sheria inasemaje,anaweza kumshitaki kwa kumshambulia? Au wao walinda amani wana certificate ya kutushambulia raia?
Mkuu, ukisema kampiga unapunguza uzito,amemtwanga ngumi nzito sana! Ile ni ngumi unayopigwa ili ama ufe kabisa au ufe kwa muda mfupi.

Bado hadi sasa najiuliza kama huyu mlinzi alikuwa sawa kiakili au ni mambo ya pombe.
 
Kumbe tuwaachie muwe mnazikana wenyewe tuh maana mmetuona viherehere. Watanzania wote Arusha na monduli kwa ujumla jiepushane na msiba wa Lowassa msije mkapigwa ngumi za uso au risasi.

Waachieni kina Nape na Makonda hao ndio waliompenda.

Mwananchi
.kama kweli tuko makini huyu jamaa lazima achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu kulikuwa hakuna sababu yoyote ya yule mlinzi kumshambulia yule muombolezaji mimi niko tayari hata kuchangia gharama za kesi.
 
.kama kweli tuko makini huyu jamaa lazima achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu kulikuwa hakuna sababu yoyote ya yule mlinzi kumshambulia yule muombolezaji mimi niko tayari hata kuchangia gharama za kesi.
Kesi bongo,we changa tu
 
Back
Top Bottom