Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Kumbe tuwaachie muwe mnazikana wenyewe tuh maana mmetuona viherehere. Watanzania wote Arusha na monduli kwa ujumla jiepushane na msiba wa Lowassa msije mkapigwa ngumi za uso au risasi.

Waachieni kina Nape na Makonda hao ndio waliompenda.

Mwananchi
 
Mlinzi anatembea na hasira kichwani ,unafikiria kuzungushwa juani hapo unakimbia wanapenda.

Palikuwa hamna haja ya kumshambulia mtu, Ukweli jamaa alionyesha upendo kutaka kushika hata gari iliyobeba mwili wa mpendwa wao
Ndiyo maana sipendagi kiherehere kwa hawa watawala nabaki tu nyumbani kuangalia kwenye tv kama jitu limekufa walizike tu huko wenyewe watajijua lakini Watanzania tunapenda kujitia kiherehere hiyo ndiyo faida yake.
 
Inasikitisha Askari huyo kufanya hivyo mbele ya jeneza la Marehemu Mh. Lowassa. Na muombelezaji Hana silaha yoyote ya kutisha uhai wa mtu..

Apewe adhabu au aachishwe kazi.. na walinzi wengine hata kumcheki jamaa.. walimlipie matibabu 100% na pesa za kumjeruhi..
 
Inasikitisha Askari huyo kufanya hivyo mbele ya jeneza la Marehemu Mh. Lowassa.

Apewe adhabu au aachishwe kazi.. na walinzi wengine hata kumcheki jamaa.. walimlipie matibabu 100% na pesa za kumjeruhi..
Siku mbili hizi tulianza kuaminishwa wema wa Lowasa lakini kwa haya tunaanza kuhisi kuwa labda ndivyo alivyoishi na wanyonge wakati wa uhai wake
 
Ngumi kama imerushwa kizembe ila ukiizoom na kuitafakari inakoelekezwa ni ngumi ya kitaalam sana. Sumbwi limeelekezwa kupiga maeneo ya kimkakati ili jamaa asirudie tena.

Mlinzi angempiga mtama tu huwezi kulinda maiti kwa kuhatarisha uhai wa wanaopumua
 
Hakutakiwa kuusogelea misafara kapata posho yake

Kubugia Viroba vya pombe huyo vimemponza pombe sio chai Ona Sasa kilichomkuta angelewa akabaki nyumbani yasingemkuta
Watu kama wewe pengine mmekulia kwenye familia za kishenzi, ambazo hazina uastaarabu na mtu anapokosea kipigo cha mbwa ndiyo suluhisho. Na mbaya zaidi huna exposure yeyote, umezaliwa na kukulia sehemu moja na hujui dunia ilipo sasa hivi. Unatia huruma.
 
Back
Top Bottom