Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Raia muombolezaji apigwa ngumi na mlinzi wa msafara wa Lowassa

Hiki ni kiburi cha hali juu. Mwili wa Lowassa una thamani kuliko mtu aliye hai. Kwanza kuna mantiki gani ya kukimbia pembeni ya gari utadhani wamebeba kitu cha thamani sana? Kwa upande wa pili wa shilingi. Na sisi raia tumezidi ukondoo. Watu kama hawa wanapofariki kwa nini tusijikalie nyumbani ili wajue kuwa hatuwathamini kama wasivyotuthamini?
Yawezekana ni protokali za kijeshi mkuu.
 
Very nice comment. Angefanya hivyo lingekuwa jambo la busara. Hili tukio limeniuma sana.
Mkuu wakati mwingine hata sisi raia tunakuwa wajinga. Kilichotokea wakati wa kifo cha Magufuli kilinifanya nifikirie mara mbili kuhusu mazishi ya viongozi. Wale waliokufa kwa kukanyagana walikuwa wengi kweli kweli lakini serikali ikadanganya idadi. Kuna jamaa alikwenda kumcheki ndugu yake vyumba vya maiti vya hospital za Muhimbili na Amana akasema kulikuwa na maiti nyingi sana. Na serikali haikujali hata kidogo ilifanya kama ni mbwa wamekufa. Imefika wakati kwa raia kuacha kujipanga au kwenda kwenye mazishi ya hawa viongozi.
 
Back
Top Bottom