Raia Mwema: Wanawake 40 wajitokeza TAKUKURU kutoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono na ubakaji wa Ole Sabaya

Raia Mwema: Wanawake 40 wajitokeza TAKUKURU kutoa ushahidi wa unyanyasaji wa kingono na ubakaji wa Ole Sabaya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa kutoka Takukuru zinaonyesha kwamba mpaka muda huu Jumla ya Wanawake 40 wakiwemo wanafunzi wa vyuo na Sekondari wamejitokeza kutoa ushahidi wa namna walivyobakwa na kufanyiwa ukatili mwingine wa Kingono na Mtukufu Ole Sabaya (namba inaweza kuongezeka).

Inadaiwa kwamba Sabaya akishalewa kwenye Bar yoyote alikuwa anang'ang'ania mwanamke yeyote aliyemtaka na kuondoka naye kwenye Hotel yoyote na kumfanyia ukatili alioutaka huku akilindwa na Polisi na Mabaunsa wake.

Tutaendelea kuwaletea uhalifu wa huyu jamaa kwa kadri unavyotufikia bila kuedit chochote .

Endelea kututegea sikio.
---
Sabaya.jpg
 
Mkuu hii kesi kwanini iko TAKUKURU na siyo polisi? Kwa maoni yangu TAKUKURU haihusiki hata chembe na hii kesi.
Taarifa kutoka Takukuru zinaonyesha kwamba mpaka muda huu Jumla ya Wanawake 40 wakiwemo wanafunzi wa vyuo na Sekondari wamejitokeza kutoa ushahidi wa namna walivyobakwa na kufanyiwa ukatili mwingine wa Kingono na Mtukufu Ole Sabaya ( namba inaweza kuongezeka )

Inadaiwa kwamba Sabaya akishalewa kwenye Bar yoyote alikuwa anang'ang'ania mwanamke yeyote aliyemtaka na kuondoka naye kwenye Hotel yoyote na kumfanyia ukatili alioutaka huku akilindwa na Polisi na Mabaunsa wake .

Tutaendelea kuwaletea uhalifu wa huyu jamaa kwa kadri unavyotufikia bila kuedit chochote .

Endelea kututegea sikio .
 
"Moja kati ya tuhuma zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ni unyanyasaji wa kingono. Sabaya anadaiwa kulazimisha ngono wanawake mbalimbali, kuwachukua kwa nguvu anapokutana nao kwenye klabu za usiku, na kuwapeleka hotelini kufanya nao ngono kwa lazima. Jumla ya wanawake 40 wamejitokeza kutoa ushahidi TAKUKURU.

Kati ya wanawake hao wapo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika mikoa ya Arusha na Kilimnjaro. Kati ya wanafunzi hao wawili wanadai kulawitiwa baada ya kutekwa na walinzi wa Sabaya walipokutana nae night club. Mmoja kati ya walinzi amekiri kuwapeleka wasichana hao kwa Sabaya lakini amekanusha tuhuma za ulawiti.

"Tuliagizwa kuwachukua lakini sikujua mahusiano yao na Mhe.Sabaya wala sikujua kama walikubaliana kukutana. Nakiri kuwapeleka kwake lakini kuhusu kulawiti siwezi kutoa ushahidi maana sikuwa naye ndani" mmoja wa walinzi wa Sabaya ameieleza timu maalumu (task force) inayochunguza suala hilo kwa kushirikiana na TAKUKURU.

Sabaya anadaiwa kufanya vitendo hivyo katika hoteli mbalimbali za kifahari jijini Arusha na amekuwa akiondoka bila kulipa. Baadhi ya hoteli zimekiri kumdai Sabaya baada ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo malazi na chakula lakini amekua akindoka bila kulipa. CG Hotel wanamdai 8.7M, Grand Melia 14.8M, Melvis Hotel 3.4M, na Massai Land 9M.

Sabaya ambaye yupo mahabusu tangu May 25 mwaka huu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote ikiwa ataonekana anazo tuhuma za kujibu.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni jana alisema "Ni kweli tunamshikilia tangu jumanne ya wiki iliyopita kwa mahojiano ya tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya madaraka na rushwa. Akionekana ana kesi ya kujibu atafikishwa mahakamani". "

Copied and paste from Malisa GJ Facebook page

Swali langu:-
Hivi ni kweli JPM hakujua hizi tuhuma za Sabaya?

Kama alijua akakaa kimya basi na yeye si sehemu ya tatizo hili?

Asanteni sana Wakuu.
 
Back
Top Bottom