Raia wa Marekani wapinga vikali watu wa dini kufunga barabara kuswali

Kumbe komenti Kama hizi zinaruhusiwa jf?
 
Hao wanazua taharuki kwa wengine kwani uislam hautaki katika kuliendea jambo la ibada uwakele wengine au mambo ya wengine yasimame.

Walipaswa kujiweka pembeni na bado swala yao ingekuwa imetimia tofauti na kuhalibu taswira ya dini kwa maamuzi yao binafsi.

Kwa wingi wao huo na karibu wote ni wakazi wa hapo PA wameshindwa kupata uwanja au hata parking ili wafanye ibada kwa utulivu tofauti na kuleta hali ya kujionesha kwa wengine namna walivyo watu wa ibada.

Tofauti na hapo labda kama walikuwa na kongamano na wamepata kibali toka kwa mtawala watakuwa sahihi.

Uislam hautaki kuonea wala kuonewa,ni amani na salama mwanzo hadi mwisho.
 
Ukiswali kwa kujificha mungu atakusikiaje?
Ukisali bila watu kukuona wakati mungu yupo mbali hakuoni, nani atakuwa shahidi wako kwamba huwa unaswali?
 
Mjadala ufungwe,umemaliza kila kitu,Kwa kuongezea,Swala ya kwako wewe isiwe maudhi Kwa wengine.
 
Hata hapa bongo huwa mnafunga mabarabara TU mkijiamulia, utaskia sjui maulidi sjui nini barabara zimefungwa.
Inakera sana kwasababu barabara ni za wote na zimejengwa na serikali sio na dini yenu.
Inakera sana inakera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…