SoC04 Raia wenye afya bora ndio nguvu kazi wa taifa la kesho

SoC04 Raia wenye afya bora ndio nguvu kazi wa taifa la kesho

Tanzania Tuitakayo competition threads

Calista Mselewa

New Member
Joined
May 30, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Watu husema afya ni mtaji kwaio ili shughuli binafsi na taifa kwa ujumla zifanyike ipasavyo yahitaji raia wenye nguvu na afya njema.Katika Sekta ya afya changamoto zimekua nyingi ambazo tungetamani zifanyiwe utatuzi ili kupunguza athari kubwa kwa miaka 5-25 ijayo. Changamoto hizo ni kama
  • Wagonjwa kukosa huduma kwa wakati sahihi.
  • Tatizo la udumavu kwa watoto.
  • Vifaa na vitendea kazi kama vile vitanda kua vichache wodini.
  • Ukosefu wa wahudumu wa afya wa kutosha.
Mapendekezo ya kuboresha Sekta ya afya.
  • Kuweka utaratibu wa kumsaidia mgonjwa ambae hana hela au ana pesa pungufu kupata matibabu huku akiendelea kulipa fedha hizo, tumeshuhudia baadhi ya wagonjwa mahospitalini wakikosa huduma mbalimbali sababu ya kutokua na fedha hivo basi zitengenezwe fomu za makubaliano ya malipo kati ya mgonjwa na hospitali ili aweze kulipa taratibu huku akipata matibabu ili kuokoa maisha ya mgonjwa huyu. Fomu hizi zioneshe taarifa zifuatazo kuhusu mgonjwa ambazo ni;
Majina yake kamili .
Mahali anapoishi .
Shughuli anayofanya .
Namba zake mbili za simu .
Ukomo wa malipo hayo.
Wadhimini wanne wawili ndugu na wawili watu wa pembe (ili waweze kutusaidia mahali popote patakapokua na shida kwenye malipo).

  • Upatikanaji wa mashine za mammogram katika kila hospitali ya rufaa kila mkoa kwa ajili yakupima kansa ya matiti kwa wanawake, kansa ya matiti ni aina moja wapo ya kansa hatari zaidi na inaongezeka kwa kasi kubwa hivi sasa ili kuokoa maisha ya wanawake wengi ni vema kuweka kufaa hiki cha kupima kansa kwa umakini na kutoa majibu sahihi zaidi kuliko kupima kansa kwa kumshika mwanamke maziwa pekee pia sio kila mtu ana elimu au pesa ya kuweza kumudu kipimo hiki hivo basi wizara ya afya iweke bei nafuu kwa kila mwanamke kuweza kumudu kupima na itasaidia kugundulika mapema endapo mtu atapatikana na viashiria vya ugonjwa huu na kutibiwa mapema.
  • Kuongeza vitanda vya wagonjwa hasa wodi za wamama waliojifungua, kumekua na malalamiko ya wagonjwa hasa wamama waliojifungua kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja kitu ambacho sio salama sababu inaweza kupelekea kuambukizi ya magonjwa kama kifua,mafua au matumbo ya kuhara na miili ya watoto ua sio mikomavu huweza kupata magonjwa kirahisi kitu ambacho sio kizuri na ni hatari kwa afya zao.kwaio kila wodi iwe na vitanda vya kutosha ili kila mgonjwa alale peke ake.
  • Kuacha kizuia ndugu kuchukua miili ya wapendwa wao waliotangulia mbele za haki, baadhi ya hospitali huzuia miili kisa kudai gharama za fedha zilizotumika wakati wa matibabu kitendo hiki huondoa utu na upendo kati yetu basi sasa ni vema hospitali ipunguze gharama za vitanda na vitu vingine kwa wagonjwa ili mwisho wa siku gharama iwe ndogo au kutumia fomu za makubaliano ya malipo taratibu.
  • Kutokomeza tatizo la udumavu kwa watoto, elimu itolewe kuhusu lishe bora kwa vitendo(maana ya upishi) mama mjamzito na waliojifungua tayari waelekezwe njia sahihi ya kupika vyakula ili virutubisho visipotee. Kuna mikoa kama Iringa na Njombe wazazi huwanywesha pombe inaitwa( ulanzi) watoto wao ili walale mda mrefu kukwepa usumbufu wakiwa wanafanyia shughuli zao kama kilimo kitu ambacho sio sahihi kwaio inabidi wapewe elimu juu ya athari za pombe kwa watoto kuepusha udumavu.
  • Kuboresha huduma za afya hasa vijijini, ni kweli kwa miaka ya sasa baadhi ya vijiji kuna zahanati lakini ni vizuri serikali ikaweka huduma ya oparesheni kwa zahanati za vijijini ili ikitokea mama mjamzito ameshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida badala ya kufuata huduma ya oparesheni mjini ni vema akapata hapo hapo hii itasaidia kupunguza vifo vinavotokea kwa mama wajawazito wanaopoteza maisha njiani pia watoto hao waopoteza maisha wangeweza kua watu wakubwa kwa taifa la badae.
  • Kuajiri wa huduma wa afya wa kutosha hasa vijijini ,kama vile madaktari, afisa lishe, wauguzi wa kutosha ili huduma zipatikane kwa urahisi na kupunguza foleni za wagonjwa.

Afya bora kwa kila mtu ndio msingi imara wa kuleta maendeleo kuanzia jamii zetu na taifa zima.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom