Wanasiasa wa kiafrika wakati mwingine ni aibu tupu hasa wale waliokuwa na madaraka makubwa, kwanini huwa hawapendi kukubali maamuzi ya wapiga kura? Kipi kinachomfanya Raila aamini kuwa ameibiwa kura, huko ku delay kutangaza matokeo?! mi nafikiri ifike mahali akubali tu kwa Amani ya Kenya!
Usimlaumu sana Raila kwani once bitten twice shy. Mimi naamini kabisa kwamba 2007 alidhulumiwa.
Na hata mwaka huu, jinsi ambavyo matokeo yalivyokuwa yanatangazwa, kwa mtu yeyote mwenye kuangalia mambo katika multi-dimensional view ataona kwamba mazingira ya uchakachuaji yalikuwepo.
Wewe fikiria, uchaguzi umefanyika Jumatatu na matokeo kamili yakatangzwa Jumamosi. Kwa nini? Yaani unataka kuniambia kazi ya kuhesabu kura ni ngumu kiasi hicho hadi kuchukua masiku yote hayo?
Mbona Marekani matokeo hutangazwa siku hiyo hiyo tu. Kuna ugumu gani baada ya muda wa kupiga kura kuisha na kuanza kuzihesabu kura papo hapo mbele ya hadhara?
Sasa hawa Wakenya hiyo tume hayo ilinunua sijui limtambo la kielektroniki na baada ya kuanza kuzihesabu hizo kura likabuma. Ni kweli lilibuma au kuna mtu alifanya hujuma za makusudi ili kazi ya kuhesabu icheleweshwe?
Haya tuje kwa wale returning officers au ofisaaz kama anavyowaita Bw. Hassan. Hawa walikuwa 291 na walilazimika kurudi Nairobi kuyaleta matokeo ya vituo yao. Si wote ambao waliweza kurudi katika muda mzuri. Wengine walichukua siku 4 hadi 5.
Kuna uhakikisho gani kwamba humo njiani hawakuweza kufanya ujanja ujanja wao? Na kwa nini imchukue mtu siku zote hizo kurudi Nairobi?
Sasa mazingira hayo changanya na siasa za kikabila pamoja na historia ya nyuma, huhitaji kuwa brain surgeon kutambua kwamba mazingira ya kuwezesha uchakachuaji yalikuwepo.
Ndiyo mnamtaka Raila akubali tu kirahisi rahisi hivyo? No way Jose. Hata ingekuwa mimi nisingekubali kirahisi hivyo.