Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
keshasema anaenda mahakamani. sasa mbona anatoa hukumu na kuita watu criminals.
hayo ndo maneno ya uchochezi ambayo siku ile ya debate ya kwanza na ya pili wote kwa kauli moja walikubali hawayataki.
you wonder how kenneth is still my choice (shhhh!)
Hata akitiwa ndimu hatafaa kwa kulumangia na akiungwa tui la nazi hatafaa kutowezea....
🙂 asalam aleykum
Uwapo?
Dingi sasa anaharibu
Ivi hana washauri?
Wanasiasa wa kiafrika wakati mwingine ni aibu tupu hasa wale waliokuwa na madaraka makubwa, kwanini huwa hawapendi kukubali maamuzi ya wapiga kura? Kipi kinachomfanya Raila aamini kuwa ameibiwa kura, huko ku delay kutangaza matokeo?! mi nafikiri ifike mahali akubali tu kwa Amani ya Kenya!
Usimlaumu sana Raila kwani once bitten twice shy. Mimi naamini kabisa kwamba 2007 alidhulumiwa.
Na hata mwaka huu, jinsi ambavyo matokeo yalivyokuwa yanatangazwa, kwa mtu yeyote mwenye kuangalia mambo katika multi-dimensional view ataona kwamba mazingira ya uchakachuaji yalikuwepo.
Wewe fikiria, uchaguzi umefanyika Jumatatu na matokeo kamili yakatangzwa Jumamosi. Kwa nini? Yaani unataka kuniambia kazi ya kuhesabu kura ni ngumu kiasi hicho hadi kuchukua masiku yote hayo?
Mbona Marekani matokeo hutangazwa siku hiyo hiyo tu. Kuna ugumu gani baada ya muda wa kupiga kura kuisha na kuanza kuzihesabu kura papo hapo mbele ya hadhara?
Sasa hawa Wakenya hiyo tume hayo ilinunua sijui limtambo la kielektroniki na baada ya kuanza kuzihesabu hizo kura likabuma. Ni kweli lilibuma au kuna mtu alifanya hujuma za makusudi ili kazi ya kuhesabu icheleweshwe?
Haya tuje kwa wale returning officers au ofisaaz kama anavyowaita Bw. Hassan. Hawa walikuwa 291 na walilazimika kurudi Nairobi kuyaleta matokeo ya vituo yao. Si wote ambao waliweza kurudi katika muda mzuri. Wengine walichukua siku 4 hadi 5.
Kuna uhakikisho gani kwamba humo njiani hawakuweza kufanya ujanja ujanja wao? Na kwa nini imchukue mtu siku zote hizo kurudi Nairobi?
Sasa mazingira hayo changanya na siasa za kikabila pamoja na historia ya nyuma, huhitaji kuwa brain surgeon kutambua kwamba mazingira ya kuwezesha uchakachuaji yalikuwepo.
Ndiyo mnamtaka Raila akubali tu kirahisi rahisi hivyo? No way Jose. Hata ingekuwa mimi nisingekubali kirahisi hivyo.
Ni sawa hata mimi naamini 2007 Raila alidhulumiwa ushindi lakini hiyo sasa ni hadithi japo inasaidia katika kueleza mazingira ya sasa, the question is wale observers wa Cord waliokuwa huko kwenye polling stations walisign karatasi za matokeo kuashiria kuwa wamekubali matokeo au la! if yes then it means Cord wamesalitiwa na watu wao wenyewe na if not then how come IEBC iliweza tangaza results? hilo la kura kupigwa Jumatatu na matokeo kutangazwa Jumamosi bado linawezekana hasa ukizingatia (inabidi kwa sasa tuamini tu hivyo sababu hatuna ushahidi mbadala) kuwa mashine za kuhesabu kura ziliharibika! maafisa kuchelewa kufika Nairobi inategemea na walipokuwa! All in all nimesikia Kilonzo anasema wanakwenda court wakiwa na full confidence wish them luck! Haraaaaaambe! Haraaaaambe! kenyans jengeni Nyayo yenu, sisi wana East Africa tuko anxious kuona the first Disney land in Africa (Mji wa kielectronic )
Nyani Gabu
Mwaka 2007 ni kweli R(uto)aila waliibiwa kura lakini, mwaka huu Ruto kawithdraw kura zake na kuzipeleka kunakostaili, Raila kwenye huu uchaguzi kashindwa kama uchakachuaji si lazima wachakachue u-Rais hao waliochukua siku 7 kufika Nairobi walikuwa buzz kuchakachua ubunge na ugavana kwanini tusione ktk mtazamo huo.
Kwa muono wangu, zile mashine hazikuharibika ila zilikuwa attacked na vijana wa west baada yakuona mambo kijana wao maji ya shingo yanamwelekea, na ndiyo maana pia ukitazama picha zima kwa darubini pana zaidi si IEBC ndo wali-resort kuhesabu manual, bali ni CORD hao hao ndo waligundua kuna tatizo ambalo limeweka constant ya kura 600 na software, na ni CORD ndo waliwaambia IEBC wahesabu kwa manual.
Jinsi CORD walivyotambua hiyo software kuna uwalakini mkubwa sana, hii nafikiri cord waliambiwa na vijana wa magharibi baada ya ku attack hizo server.
I am not going to put anything past anybody. Chaguzi za Afrika zina mambo mengi ambayo huwa hayaingii akilini.
Kura mnapiga Jumatatu kuzihesabu inachukua siku sita! Amazing!!
Na urais ndiyo the biggest prize. Hivyo it makes all the sense in the world kwamba wezi wa chaguzi hulenga kuchakachua matokeo yake.
Binafsi sina hakika sana kama Uhuru kashinda fair and square kwa sababu ya hayo mazingira ya utata utata kuhusiana na uhesabuji wa kura.
Kwa mfano tu, hivi unadhani kweli kabisa kwamba Museveni na Mugabe huwa wanashinda kihalali kabisa?
Dada king'asti,kikuyus uwezi kuwashinda kwa ubishi,na ndio wamejaa humu.hawa jamaa ni ma trouble makers sana.haki ya nani cord wakishinda kesi utaona jeshi lao la mungiki litakavyo fanya.yaani wao wanaona kwamba wao ndio the choosen tribe ambao wanafaa kuongoza.alafu ni wabaguzi sana.angalia utawala wa kibaki nafasi nyeti kwenye taasisi za serikali ni mkikuyu tu.
mungiki landlord wao mpya ni muungano wa CORD, FYI!
The dejected leader might be in cord bt surprisingly enaf Raila faired dismally in capturing their votes. A sign Mungiki when it comes to elections they revert back to their tribal enclave. So i wouldnt assume mungiki is in cord, even the leader failed in his supposedly to be 'stronghold' too.