Raila Odinga akataa matokeo na ameahidi kufikisha malalamiko Mahakama Kuu.

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2010
Posts
1,948
Reaction score
1,238
Source: BBC

Raila Odinga amekataa kukubali matokeo ya urais yaliyompa ushindi wa asilimia 50.03 mpinzani wake bwana Uhuru Kenyatta. Ameahidi kuwa atafikisha malalamiko yake mahakamani.

My take: Mwaka 2007 bwana Odinga alikataa kupeleka malalamiko juu ya matokeo ya urais mahakamani kwa sababu kuwa mahakama hazikuwa na usawa wa kuwezesha haki kutendeka..je mahakama zimekuwa za kuaminika sasa wakati ambao yeye ni mmoja wa serikali iliyo madarakani?

Lets wait and see..





 
Last edited by a moderator:
dah jamaa mtata ....kwani matokeo hayo hawaendi round ya pili?
 
Hiyo kwa Kenya inawezekana sana kwa sababu baada ya kupata Katiba mpya kuna Supreme Court ambayo ina mamlaka ya kusikiliza mashtaka yanayomhusu Rais na uchaguzi wa Rais pia
 
dah jamaa mtata ....kwani matokeo hayo hawaendi round ya pili?

Hakuna round ys pili kwa maana mshindi anatakiwa awe amepats angalau 50% ya kura + kura moja na awe ameshinda country votes 24 hivyo vyote ameshapita.
 
kama ana uthibitisho wa kutosha aende mahakamani ila kama hana awaache wakenya kwa amani
awaachie rais waliyemchagua - vinginevyo heshma yake itashuka sana
 
Kukubali kushindwa baada ya kufanya jitihada kubwa na kuona dalili za mafanikio is a process. Sasa hivi yuko katika hatua ya kuwa excited na kutokukubali anachokiona, itafika wakati anakubali tu.
Uhuru ameshinda...
 
lakini si hata cnn walisema kenya wamejiaandaa kwa vita halafu wakaomba msamaha hata hili naona ni porojo tu za bbc kumjaza ujinga raila..
 
alionesha dalili mapema, kwa kuanza kutoa matamko ya ajabu tu. Uhuru kamzidi akubali yaishe.
 
mimi ni mpenzi sana wa odinga lakini naamini wakenya wamemchagua kenyatta kuwa raisi wao na mzee wangu odinga kubali matokeo na nina amini tume ijafanya hujumaa kabisa ni kweli mzee wangu odinga umeshindwa nakutakia maisha mema ya kupumzika na ushauri mzuri achana na siasa tena kapumzike ila nacho amini mtoto wako wa kuzaa uwenda akaja kuwa raisi wa kenya...na kikubwa waambie wajaluo wazaliane kwa wingi kwa sababu ukabila ndio umekuangusha.
 

Katiba waliyonayo sasa (Katiba ya mwaka 2010) imeweka wazi juu ya suala la kupinga matokeo ya Urais na taratibu zinazotakiwa kufuatwa. Ibara ya 140 (1-3) ya katiba hiyo inasomeka hivi;
140. (1) A person may file a petition in the Supreme Court to
challenge the election of the President-elect within seven days after the
date of the declaration of the results of the presidential election.

(2) Within fourteen days after the filing of a petition under clause
(1), the Supreme Court shall hear and determine the petition and its
decision shall be final.
(3) If the Supreme Court determines the election of the President elect
to be invalid, a fresh election shall be held within sixty days after
the determination.


 
Nilitegemea hilo lakini kama kuna element ya usanii katika utangazaji matokeo haya, ni kama Uhuru alikuwa ameandaliwa ashinde hata kwa kura moja inavyosema katiba.
 
@Prisoner 46664:
je mahakama zimekuwa za kuaminika sasa wakati ambao yeye ni mmoja wa serikali iliyo madarakani?
Jibu laweza kuwa 'NDIO', si wana katiba mpya?
 
Hakuna round ys pili kwa maana mshindi anatakiwa awe amepats angalau 50% ya kura + kura moja na awe ameshinda country votes 24 hivyo vyote ameshapita.

Hivi wanaposema apate kura 50%+1. hyo Plus one ina maana gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…