Raila Odinga ana hoja,Tume imeteleza. Fomu 34A na 34B zipo kisheria

Raila Odinga ana hoja,Tume imeteleza. Fomu 34A na 34B zipo kisheria

Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.

Niliwahi kuanzisha uzi kuhusu 'u-huru' wa tume huru ya uchaguzi ambayo wapinzani wamekuwa wakiililia.

Nadhani sasa labda ambao hawakunielewa wataweza kunielewa.

Kuna dhana potofu kwamba uwepo wa tume 'huru' basi ndo utakuwa mwarobaini wa matatizo wayapatayo wapinzani.

Kama tunavyoona huko Kenya, uwepo wa tume 'huru' si mwisho wa figisu.

Ni dhahiri kabisa kuwa Odinga kafanyiwa figisu na ambaye hakuliona hilo kuwa litatokea atakuwa mbumbumbu wa mwisho kabisa.

Na ndo maana nikasema [kwenye ule uzi wa updates za matokeo ya uchaguzi wa Kenya] kuwa ningeshangaa sana endapo Uhuru Kenyata angeshindwa!

Anayedhani kuwa hiyo IEBC ni huru namwonea huruma😀
 
Kwa Fomu No. 34 Raila na NASA wako sahihi. Je suala la Udukuzi wa tume ya IEBC,huu udukuzi kupataje kama nae hajadukua? Kwa nini aseme leo siku ya kutangaza Matokeo wakati Kifo cha Chris Msando kimetokea juma 1 lilipita?
 
Tume Tume Tume Africa ni Majipu, nimeangalia Taaifa IEBC inasema haya matokeo yanayotangazwa sio officially, sasa kama sio officially mnatangaza ya nini? mnatangazaje matokeo bila kuwa na uhakika kama ni ya kweli au sio ya kweli, yaani mnatangaza tu bila kujua yanatoka wapi na mnatangaza kumfurahisha nani? Tatizo kubwa la hizi tume za Afrika ni njaa, yaani huwa hawasimamii ukweli, hapo wakitishiwa kidogo tu na chama tawala wanalegea, yaani ni mabendera kwa ufupi. Pili walijua ICT director aliuwawa na kukatwa kiganja lakini bado hawakujiongeza kulinda network yao inayotuma matokeo isiweze kuwa hacked? pole kwa vyama vya upinzani hili ni goal tayari haliwezi badilika.
 
Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.
leo umeongea kama binadamu aliyekamilika with all 5 senses of organ
 
Niliwahi kuanzisha uzi kuhusu 'u-huru' wa tume huru ya uchaguzi ambayo wapinzani wamekuwa wakiililia.

Nadhani sasa labda ambao hawakunielewa wataweza kunielewa.

Kuna dhana potofu kwamba uwepo wa tume 'huru' basi ndo utakuwa mwarobaini wa matatizo wayapatayo wapinzani.

Kama tunavyoona huko Kenya, uwepo wa tume 'huru' si mwisho wa figisu.

Ni dhahiri kabisa kuwa Odinga kafanyiwa figisu na ambaye hakuliona hilo kuwa litatokea atakuwa mbumbumbu wa mwisho kabisa.

Na ndo maana nikasema [kwenye ule uzi wa updates za matokeo ya uchaguzi wa Kenya] kuwa ningeshangaa sana endapo Uhuru Kenyata angeshindwa!

Anayedhani kuwa hiyo IEBC ni huru namwonea huruma😀
Ninakubaliana 100% na hoja yako.

Kwa hizi nchi zetu, muda wa wapinzani kupata angalau nafasi kubwa katika ushindi ni katika mazingira ambayo hayana incumbent president katika uchaguzi.

Taasisi zetu hizi kusimamia sheria na kutafsiri sheria hazina uwezo wa kuzuia nguvu za Rais katika kutekeleza matakwa yake hata yale ambayo yako kinyume na katiba/sheria.

Ukijifanya kusimamia Katiba/sheria wanakuweka kando au wanachukua maisha yako kama ilivyotokea kwa Chris Msando.

Hao NASA hata wakienda mahakamani hawawezi kushinda. Huu ndio ukweli.
 
Boss MsemajiUkweli Bora umekiri na kusema kweli. Nimependa hapo pa ....

"Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali".

Ila mbona Marekani sio ngumu? Au Uingereza? Kwanini ni Africa tu?

Hizi ndizo tume zetu ''huru'' za Uchaguzi!

Tume ''huru'' ya Uchaguzi inatangaza matokeo ya Uchaguzi ''huru'' halafu baadaye inatuambia hayo sio matokeo rasmi ya Uchaguzi!

Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali.

Siku alipouwawa yule mkuu wa kitengo cha teknologia ya habari na mawasiliano kwenye tume ya Uchaguzi, Chris Msando ndio siku ambayo uchaguzi Mkuu ulihitimisha mwanzo wa vurugu za Uchaguzi Mkuu.
 
Ngoja nitoe ufafanuzi kidogo hapa.

Sheria ya Kenya ina hatua tatu kuu katika kutangaza matokeo ya uchaguzi...

1/Matokeo kutangazwa kila kituo separately (Na haya ndio matokeo yaliyopo sasa mitandaoni, na hichi kitu kilibishaniwa mahakamani hapo kabla ya uchaguzi ambapo NASA walitaka matokeo ya kura katika kila kituo yatangazwe pale pale kituoni na mahakama ikakubali na taarifa za matokeo hayo ziwe wazi katika mfumo rasmi wa kujumlishia matokeo mtandaoni baada ya kuscan form ya matokeo) Hichi kitu ndio kinaonyesha Uhuru anaongoza mpaka sasa.

2/Matokeo ya urais katika kila jimbo yajumlishwe na jimbo husika baada ya kukusanya fomu za matokeo kutoka kila kituo katika jimbo husika (Hili zoezi ndio kwanza linafanyika sasa, na litachukua muda kidogo). Na hichi ndio Raila anakidai sasa...

3/Tume ya uchaguzi ikusanye matokeo ya vituo vyote vya kupigia kura nchi nzima kwa kupitia fomu maalum za mawakala zilizo sainiwa na kuwekwa matokeo.(Zoezi hili ndio linaendelea katika makao ya tume ya uchaguzi kwa sasa na litachukua siku kadhaa). Pia hichi kitu Raila anakidai...

Wakenya waliweka huo mfumo ili kujiridhisha kwa kila hatua kabla ya kutangaza mshindi, lakini pia kutoa nafasi kwa mgombea asiyeridhika kuhoji au kupinga kisheria hatua yenye matatizo lakini pia tume kutatua tatizo kwenye hatua halisi. Mambo hayo yanakuwa na msingi sana pale kunapokuwa na mchuano wa karibu wa kura.

Mpaka sasa tume ya uchaguzi ya Kenya haijapinga chochote kwa sababu mambo yote ni sehemu ya mchakato uliopo mbele yao. Na wote wanalijua hilo(Ndio maana hata NASA hawajakimbilia mahakamani). Tatizo kubwa ni kwamba kwa hali ilivyojionyesha, namna matokeo yalivyotolewa na tume wakati michakato bado haijakamilika kisheria ni kama matokeo yaliyotolewa ni RASMI kitu ambacho kwa sheria za uchaguzi za Kenya sio sahihi. Lakini yote kwa yote Raila anapinga hayo matokeo kwa sababu tayari yameonyesha anaelekea kushindwa, na kama yangekuwa yanamuonyesha anaelekea kushinda lugha ingebadilika, angekuwa anashinikiza kutangazwa mshindi sasa wakati tume ingekuwa inasema bado wako kwenye michakato ya kumjumlisha!
Binafsi sijaona mantiki ya Raila katika hili kama inaweza kubadilisha matokeo ikiwa kilichotumwa mtandaoni kilitoka kwenye kituo cha kupigia kura regardless ya hizo fomu....

Jambo pekee ambalo binafsi nina muunga mkono Raila katika hoja zake ni kuhusu wasiwasi wa udukuzi katika mtandao wa kujumlishia matokeo, ukweli wa hoja hizo tutauona wakati wa kujumlisha fomu moja moja ya matokeo ya uchaguzi manually.
Na kama kutakuwa na Ukweli mkubwa wenye kuweza kugeuza matokeo ya mshindi, hapo nitamuunga mkono, na straight nitamshauri aende mahakamani kupinga.
 
Kwa Fomu No. 34 Raila na NASA wako sahihi. Je suala la Udukuzi wa tume ya IEBC,huu udukuzi kupataje kama nae hajadukua? Kwa nini aseme leo siku ya kutangaza Matokeo wakati Kifo cha Chris Msando kimetokea juma 1 lilipita?
Udukuzi umefanywa baada ya kukata kiganja cha mkono wa CHRIS MSANDO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss MsemajiUkweli Bora umekiri na kusema kweli. Nimependa hapo pa ....

"Kwa kifupi, kwenye siasa za nchi ''zinazoendelea'' ni vigumu sana kumshinda Rais ambaye anatetea kiti chake cha Urais. Huu ndio ukweli pamoja na kwamba ni vigumu kuukubali".

Ila mbona Marekani sio ngumu? Au Uingereza? Kwanini ni Africa tu?

Africa bado tunatumia tumbo kwa kila kitu tukiweza kufikia uwezo wa kutumia vichwa ndio tutaanza kufanya mambo sahihi. Kwa sasa acha tumbo lifanye kazi.
 
Hoja ya Odinga ni kukosekana kwa Fomu 34A na 34B zinazopaswa kujazwa na kusainiwa,ikiwa ni pamoja na mawakala, kisheria kabla ya kutangazwa matokeo. Fomu 34A hujazwa na kusainiwa katika Kituo cha Kupigia kura. Kimsingi,Fomu 34A hubeba taarifa za kura za kituo kimoja.
Petro E. Mselewa, je umesikiliza maelezo yaliyotolewa na Tume? Mimi nimesikiliza kidogo maelezo ya msemaji wa hiyo Tume ila kwa bahati mbaya niliyakuta nusu. Mapema Tume ilikutana na wawakilishi wa vyama vyote na kuwaeleza utaratibu ulivyo kwenye sheria lakini vyama ndivyo havikuafiki vikitaka matokeo yatangazwe moja kwa moja baada ya kusainiwa bila kuzisubiri hizo fomu kufika kwa tume kwa kuhofia matatizo ya usafiri.

Vyama vilidai hivyo vikiwa na wasi wasi kwamba kusafirisha fomu kunachukua muda mrefu na zinaweza zikachezewa njiani. Hivyo wote waliafiki kwamba matokeo yakishasainiwa na kuthibitishwa na wasimamizi yatangazwe mara moja fomu zikiwa zinasubiriwa. Tume imedai imeshtushwa na tuhuma zinazotolewa hivi sasa kwa sababu vyama vyote viliwakilishwa na vikakubaliana hivyo. Wameituhumu NASA wakisema you cant eat your cake and have it.

Siitetei Tume wala siwatuhumu NASA, naeleza tu nilichosikia which to some extent makes sense. Kama nimekosea kuwakilisha natanguliza samahani, lengo langu si kupotosha kinachojiri.
 
Udukuzi umefanywa baada ya kukata kiganja cha mkono wa CHRIS MSANDO.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawana Mamlaka ya kudukua Kanzi Data ya IEBC! Kwa kifupi ni kwamba Jubilee na NASA wote wamedukua Kanzi Data ya IEBC ila Nasa wamewakuta JP, wakawaacha. Ilipofika asubuhi NASA wakakimbilia kwa Wananchi ooh JP, ooh Jubilee! Upuuzi mtupu
 
Tume huru ya uchaguzi Kenya.. Kina Mbowe utasikia tunataka tume huru
 
Back
Top Bottom