Mgombea wa Urais wa Kenya kupitia NASA,Raila Odinga amejitokeza na kupinga matokeo ya awali ya Urais ya Kenya yanayotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya yakimweka mbele Rais Uhuru Kenyatta.
Hoja ya Odinga ni kukosekana kwa Fomu 34A na 34B zinazopaswa kujazwa na kusainiwa,ikiwa ni pamoja na mawakala, kisheria kabla ya kutangazwa matokeo. Fomu 34A hujazwa na kusainiwa katika Kituo cha Kupigia kura. Kimsingi,Fomu 34A hubeba taarifa za kura za kituo kimoja.
Fomu 34A huwasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo. Taarifa zote za vituo vya Jimbo husika hujazwa kwenye Fomu 34B. Hatimaye,Fomu 34B huwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kutangazwa matokeo rasmi.
Kujazwa kwa Fomu nilizozitaja,ni sharti la kisheria. Lazima kuzijaza na kuziwasilisha. Inataarifiwa kuwa Tume ya Uchaguzi ilitangaza matokeo bila Fomu 34A na 34B. Kwasasa,Tume inakusanya Fomu wakati matokeo yameshatangazwa na kubishiwa.
Hivyo,Odinga ana hoja ya kisheria kuyabishia matokeo hayo. Je,atayapinga matokeo ya Urais kisheria au kisiasa? Matokeo yaliyotangazwa bila fomu husika yanabakije kama halali? Raila Odinga ataamua muda ukifika.Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya,Tume ya Uchaguzi ina siku 7 kumtangaza mshindi wa Urais.
Mkuu, sikusema fomu hazipo. Nimesema, matokeo yalitangazwa kabla ya fomu kuwasilishwa kwa Tume. Ndiyo hoja ya RailaMkuu uliambiwa 34A na 34B hazipo???
Mkuu wewe umesoma lakini siamini kwenye hili kama ulijiridhisha kuwa hizo form hazipo kabla ya kuandika.
Hata tume ya Uchaguzi jana imesema itafanya mahesabu kupiti form hizo sasa hii yako kuwa form hazipo umelitoa wapi?
Mbona nchi nyingine za Afrika wameweza? Nchi kama Ghana, Zambia, Nijeria, Malawi n.k.Hiyo conclusion ibaki tu east Afrika siyo Afrika nzima.Ukweli Ambao Upinzani hawataki kuusikia ndio huu.Huwezi kutenganisha tume ya uchaguzi na Uongozi uliopo madarakani kwa nchi zetu hizi.
Raila hawezi kuwa Rais hata kama ameshinda.Ukweli mchungu kwake.
Sasa kama matokeo yanayotangazwa na tume ni tofauti na yaliyopo kwenye form maanake nini si kwamba either servers na iebc zimeingiliwa au iebc wanafanya makusudi. Tatizo tunarukia tu hoja bila kufuatilia mambo yalivyo!Kwa Fomu No. 34 Raila na NASA wako sahihi. Je suala la Udukuzi wa tume ya IEBC,huu udukuzi kupataje kama nae hajadukua? Kwa nini aseme leo siku ya kutangaza Matokeo wakati Kifo cha Chris Msando kimetokea juma 1 lilipita?
Mkuu, sikusema fomu hazipo. Nimesema, matokeo yalitangazwa kabla ya fomu kuwasilishwa kwa Tume. Ndiyo hoja ya Raila
Naomba niende kinyume na wewe tume huru ni dhana, ila uhalisia wake haupo katika maana/dhana/definition ila upo katika utendaji kazi wake kwa maana uhuru/kutoingiliwa, uwazi, effeciecy ya kumudu majukumu ya kichaguzi, usawa/fairness na mwisho kabisa uundwaji wake/upatikanaji wake na udhibiti wake kwa maana ya vyombo kama mahakama huru au kamati zibiti za ambazo zitakuwa shirikishi za wanufaika wa chaguzi. Tume ikitimiziwa haya inaweza kuwa huru.
Tatizo anataka na wewe utumie akili za bendera kufuata upepo bila kutumia akili yako uliyoipata kutoka kwa Mungu. Huyu jamaa akiambiwa na Lissu avue nguo atembee uchi atafanya hivyo maana akili yake imemuambia kila asemacho Lissu ni sawa. Kuna watu humu wanafanya nijitoe tena JFTatizo nini Mkuu? Punguza jazba na chuki
Usitoke mtani,tuwajibu kwa hoja.Tatizo anataka na wewe utumie akili za bendera kufuata upepo bila kutumia akili yako uliyoipata kutoka kwa Mungu. Huyu jamaa akiambiwa na Lissu avue nguo atembee uchi atafanya hivyo maana akili yake imemuambia kila asemacho Lissu ni sawa. Kuna watu humu wanafanya nijitoe tena JF
Watakuwa walipewa maelekezo na bwana mkubwatume nayo ilikuwa na haraka ya nini kutangaza matokeo bila kusubiri izo form. yale yale ya kibaki kulazimisha atangazwe mshindi bila ya kupata majumuisho ya kura zote.
hawa tume ndo wa kulaumiwa kama kutatokea lolote la hovyo
Sijawahi kuwa na jazba wala chuki ndugu wakili msomi. Ila wakati mwingine arguments zako zinakuwa weak kidogo. Tatizo linakuwa nini?Tatizo nini Mkuu? Punguza jazba na chuki
Kama ipi? Na ingekuwaje strong?Sijawahi kuwa na jazba wala chuki ndugu wakili msomi. Ila wakati mwingine arguments zako zinakuwa weak kidogo. Tatizo linakuwa nini?
Nani amekwambia kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyo tangazwa hayakuwa kutoka ktk hizo form nchi nzima kama tume inavyotakiwa na katiba ya Kenya? Msilete visingizio vya uwongo vya RailaMgombea wa Urais wa Kenya kupitia NASA,Raila Odinga amejitokeza na kupinga matokeo ya awali ya Urais ya Kenya yanayotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya yakimweka mbele Rais Uhuru Kenyatta.